SoC01 Magereza nchini siyo dili tena: Tuyabadilishe kuwa viwanda vya uzalishaji na kukuza uzalishaji wenye tija kwa maendeleo

Stories of Change - 2021 Competition

Akwinox_Nico

New Member
Jul 15, 2021
3
0
Naweza onekana mwendawazimu na nisiwe na akili kabisa kwa walio wengi. Lakini kwakuwa hii nafasi imejitokeza acha niandike mambo ambayo yamekuwa yakinisumbua kwa miaka zaidi ya miaka 15 sasa. Hadi nakuwa kijana nayejitambua kwa maana ya kuwa na akili zangu timamu ambazo nimezipata kwa shule mbalimbali sijawahi kuona umuhimu wa kuwa na kitu kinaitwa JELA. Hili jina limekuwa likiniumiza sana tokea mdogo na nimekuwa na ndoto za kutamani liwe na jina la tofauti kabisa.

Msomaji najua unaweza usinielewe muda huu lakini kwa haya maneneo 1,500 niliyopewa kuandika andika langu naamini hutatoka mkavu kuna kitu lazima utajifunza tu. kwangu kitu kinachoitwa JELA huwa naona kama ni kitu fulani cha kizamani/kikoloni sana ambacho tumekirithi kwa wakoloni na kwakuwa tumeamua kukikumbatia basi ndo hivyo tena hatuna namna ya kujinasua.

SWALI KUU, jiulize tu kuna haja gani ya kumfunga mtu JELA miaka 40 lakini siku ametoka tu JELA anafanya tena tukio dogo la kuiba kuku wa elfu 5, kufanya mauaji ya kikatili na kurudi tena JELA miaka 15?. Tujiulize tu kuna shida gani hadi mtu atamani tena kurudi JELA wakati kama ni mateso yote ashayapa (kulala chini, kuumwa na mbu,kunguni achilia mbali matendo ya kudharirishana ambayo kila mtu anayasikia kwenye vyombo vya habari kila siku? Ni kweli milioni 5 ni nyingi sana kushindania ndani ya mwezi mmoja na mtu akaweza hata kununua gari lililotumika (used) na akaweza kuonekana wa maana sana.

Kwangu mimi sio pesa tu, naona huu ndo wakati wangu wa kuchagiza maendeleo na kuwatoa nje walioko kwenye maamuzi na sehemu nyeti kwenye maeneo yao ya kujidai (comfort zone) - hakuna kazi ngumu na ya lawama kama kumtoa mtu kwenye eneo lake la kujidai ambaalo siku zote limekuwa likimpa heshima yake. Unaweza hata poteza maisha yako kwa urahisi sana, mimi leo nimeamua kuwatoa baadhi kwenye maeneo yao ya kujidai. Hili ni andishi la kimashindano basi ngoja na mimi leo nishindane hakuna namna.

HAYA SASA JELA KUWA KIWANDA. Hakuna asiyejua kuwa Tanzania ina JELA nyingi sana (zaidi ya 40) ambazo kwanza ziko katika maeneo nyeti sana na pia ziko sehemu nzuri ambazo ni za kimkakati kwa ajili ya kuzalishia nchi na wakati huo zikiwasaidia wahalifu kujiona wakosaji na wabaya sana kukubali kuwepo maeneo yale kwa ajili ya kuzalishia wengine. TARATIBU SANA twende pamoja na kwa upole,kwani kuna shida gani JELA zote Tanzania tukaamua kuziita VIWANDA vya uzalishaji? SWALI KUU, KWANINI VIWANDA VYA UZALISHAJI? kwa kutumia tu hili neno Kiwanda cha uzalishaji mtuhumiwa atakuwa anajua kuwa nakwenda kuzalisha kwa ajili ya wengine na sio kwamba nakwenda kupewa adhabu ya kulima na kukata magogo.

HII INA MAANA GANI? kama mtuhumiwa ameiba mfano milioni 10 basi atakwenda kuzalisha milioni 30 au 40 ili awe ameipa Serikali faida ya milioni 20 au 30 kutokana na makosa yake aliyoyafanya na hapo inakuwa faida kwa Serikali. KWANINI FAIDA? Anakuwa amezalisha hiyo hela ya ziada bila kupewa hela yoyote ile hata kama amefanya kazi miaka 20.

KUNA MTU ANAULIZA HAPA TUTAFIKA VIPI KUWA KIWANDA? Jamii Forum wametoa maneno 1,500 tu ila naamini nitajitahidi niyatumie 1,499 kufikisha ujumbe wangu na ukamfikia kila mwenye uwezo wa kuyafanya haya mawazo kuwa kweli. Hata balbu ya taa ilianza kama utani tu lakini lei hii tunajivunia akili iliyowekezwa kwenye kutengeneza bulb za umeme. HAYA TWENDE SAWA...JELA kubwa zote ziko nje ya miji mikubwa na zina wafungwa wengi sana na zina maeneo makubwa sana. Serikali ifanye yafuatayo ili kuendana sawa na haya mawazo ya kimapinduzi yanayoweza kuwa sio mazuri kwa kila mtu:-

i] Kuyatambua MAJELA yote yenye maeneo makubwa na yapo katika maeneo ya kimkakati. Maeneo ya kimkakati ni yale yenye ardhi nzuri sana ya uzalishaji na yenye kukubali mazao mengi sana kwa wakati/msimu

ii] Kuwahamisha wafungwa wote ambao wako Jela za MIJINI kwenda kwenye hizo JELA kubwa kwa ajili ya kuanzisha uzalishaji na kubadirisha matumizi ya neno JELA kuwa VIWANDA VYA UZALISHAJI.

iii] Serikali kuyabadirisha MAJELA yote yaliyoko mjini kuwa viwanda vya kupokea malighafi zinazozalishwa katika MAJELA ya mbali ambayo kwa hili andiko tunayaita VIWANDA namba 1. Hivi ni viwanda ambavyo vitaunganishwa na miundombinu ya kimkakati kwa ajili ya kusafirisha bidhaa zenye ubora zaidi kwenda nje ya nchi.

KUNA FAIDA GANI JELA KUWA VIWANDA; kuna faida nyingi san za jela kuwa viwanda kwa maana itafanya waharifu wasione kama wako jirani na jehanamu na kwamba kuwepo kwao kule kunawafanya pia waweze kuwa na maarifa mapya hata kama hakuna pesa wanayoipata kwa muda huo lakini wakishatoka nje ya VIWANDA watakuwa raia wema na hawatakuwa wakatili kama hali ilivyo sasa kwakuwa huduma zote muhimu watapewa ila itawalazimu wafanye tu kazi bila kupewa malipo kipindi hiko chote ambacho wanatumikia adhabu zao

WAPI USHAONA JELA IKAWA NAMNA HII? kuna mifano mingi sana duniani ambayo inajaribu kumfanya mtu aliyoko JELA asijione hata kama yuko jela na akapunguza sana ukatiri baada ya kutoka. Nchi kama Uswisi (Switzerland) ina JELA chache sana na inaonekana kuwa moja ya nchi salama sana hapa dunia na bado inaendelea kupunguza matukio mabaya ya kiharifu ya kibinadamu ambayo kama tukiamua tunaweza kuibaridisha na kuwa mfano mzuri sana kama tukiamua kufanya haya yanayopendekezwa kwenye andiko.

NINI SASA BAADA YA JELA KUWA VIWANDA? Jela ikishakuwa kiwanda maana yake ni kwamba jela zote za nje ya miji mikuu zitakuwa ndo sehemu za uzalishaji na zile za mjini zitakuwa zinapokea mizigo/bidhaa na kuziboresha zaidi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi. Ikumbukwe kuwa viwanda hivi viwili vitakuwa na miundombinu ya moja kwa moja ili bidhaa ikifika ifanyiwe kazi kwa haraka sana kwa ajili ya kuendelea na hatua nyingine. Mfano tu wa haraka ni JELA ya Keko Dar es salaam inabadirika na kuunganishwa na huduma ya reli kwani iko jirani na bandari kwa ajili ya kuboresha bidhaa (VALUE ADDITION) kwa ajili ya kwenda nje ya nchi kupitia njia ya bandari.

FAIDA KWA WENGINE ITAKUWEJE? Mawazo haya yatakuwa na faida sana kwa vijana wa Tanzania hasa waliosoma elimu mbalimbali. Hivi viwanda vyote vilivyoko nje ya miji na vilivyiko ndani vyote vitakuwa kama VIWANDA HATAMIZI (INCUBATIONS INDUSTRIES) kwa maana vitakuwa na wataalamu wa aina zote kwa maana ya sekta zote ambazo ziwezi zitaja hapa maana zitazuia idadi yangu ya maneno 1,500. Hawa watakuwa ni wanafunzi waliohitimu vyuo mbalimbali wakiwa wamehimu vyuo mbalimbali kwa ajili ya kutoa utaalamu wao waliojifunza mashuleni/vyuoni kwenda kwenye vitendo huku wakipata ajira za moja kwa moja kupitia huu mradi. Watakuwa wanatoa ujuzi wao na wafungwa watautumia katika kuzalisha na wakati huo wao wakipata kipato na kupunguza utegemezi kwa Serikali.

Ikumbukwe kuwa Tanzania ni moja ya nchi zenye mapungufu makubwa sana ya ajira wakati huwa ikiwa na vijana wengi sana wanaomaliza vyuo vikuu na kuingia mitaani na kuishia kuwa bila ajira kwa miaka mingi sana. Fursa hii ya kuandika mawazo yanayotoka mtaani inaweza kuwa njema kwao kwa maana ya kujaribu kubadirisha mifumo iliyozoeleka na ambayo haikuwazwa kubadirishwa kwa ajili ya kuongeza uwigo wa ajira ambazo zimeonekana kuwa kitendawili hizi siku za karibuni.

NJIA NYEPESI SANA KWA VIJANA KULIPA MIKOPO YA ELIMU WALIYOLIPIWA NA SERIKALI. Hii inaweza kuwa ndo njia nyepesi sana kwa vijana kulipa mikopo waliyolipiwa na serikali kwa maana kuwa wanachotakiwa ni kuingia kwenye mfumo huu kwa kulipwa 40% na huku serikali ikichukua 60 kutoka kwenye kazi walizofanya. ULIPAJI HUU UKOJE? kijana aliyepewa mkopo wa kusomeshwa chuo kikuu kwa mfano atafanya kazi za ziada (part-time) ili angalau kupunguza deni analodaiwa na serikali.

Kama kazi ilikuwa ya malipo ya milioni 1 basi atalipwa laki 4 ili laki 6 apunguze kwenye deni analodaiwa huku akiendelea kufanya shughuli zake bila kuathiriwa na chochote kile. Mdaiwa anaweza kutumia siku zake za mapumziko kufanya kazi kwenye hivi vituo hatamishi ili kupunguza madeni yake bila kuguswa mshahara anaolipwa kazini kwake. Ulipaji wa madai ya mikopo umekuwa mgumu sana maana mdaiwa anaweza hata kukaa miaka 6 bils kuwa na ajira na bado anatakiwa kulipa malimbikizo ya madeni. Ndo maana andiko hili linapendekeza mtu afanye kazi za kujitolea kwenye hivi Vituo Hatamishi kwa kulipwa 40% ili 60% itumike katika kulipa deni lake la kusomeshwa na serikali bila kusikia uchungu wa kufyekwa mshahara lakini wakati huo deni husika likiendelea kupungua bila kuwa na athari kubwa kama ilivyo sasa.

NIMEBAKIWA NA MANENO 148 TU, Nihitimishe kwa kusema kuwa sio lazima kuendelea kufuata utaratibu wa kikoloni kwa kufungia nguvu kazi ndani na kuifanya isizalishe. Pia sio lazima kumpa adhabu kali sana binadamu akaweza kukuelewa na kukuona umemsaidia sana badala ya kumafanya ajione yuko shimoni.

Mwenye uwezo wa kujua stahiki za adhabu zetu ni mwenyezi Mungu PEKE YAKE. Naomba Tanzania tuwe nchi ya kwanza kufuta majela na kuweka JELA VIWANDA angalau tukumbukwe kwa hilo maana tunaoneka tupo nyuma kwenye kila kitu. Ninaandika hili andiko sio kwa ajili ya pesa tu ila naandika nikiwa nalia sana maana naona huu ndo wakati pekee wa kuishangaza dunia na kujiwekea alama ya kudumu kama alama ambazo WAZUNGU wamekuwa wakiweka. Hatuwezi kutengeneza MAGARI tumekubali kiroho safi kabisa,basi tuwe nchi ya kwanza duniani kubadirisha MAJELA kuwa viwanda kwa ajili ya KUTENGENEZA AJIRA MPYA NA KUACHA KUMBUMIZI YA MILELE HAPA DUNIANI.

Ndimi Mwanahabari/Journalist wa MTAANI_Nico

ASANTENI.
 
Back
Top Bottom