magereza ingekuwa na elimu lazima kwa wafungwa

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Iwapo magereza yetu yangeamua kuanzisha program za elimu na iwe lazima kwa kila anaeingia mle, naamini tusingekuwa hapa tulipo leo, maana naona ama kujiaminisha wengi wa wafungwa hujiona wasio na thamani kwenye jamii, hivyo kama kila mfungwa mmoja mmoja angechagua kozi na kuisoma mle ndani ya magereza basi tungekuwa na idadi ndogo sana ya wafungwa mwaka hadi mwaka
 
Naomba nikujuze kwa uhakika Magereza inatoa elimu kwa njia nyingi tofauti na study za darasani kwa njia ya ufundi. Lengo kuu la Magereza ni urekebishaji wa wafungwa.

Magereza ina viwanda ambavyo wanaowafundishwa kazi za study mbalimbali ni wafungwa na wengine wanapomaliza vifungo vyao huwa mafundi kamili ambapo ufundi huo wanakuwa wameupata jela.

Hali kadhalika Magereza pia inajishughulisha na kilimo, na mfano yapo Magereza mbali mbali ya kilimo ambapo wafungwa hufunzwa kilimo bora ili baadae wakitoa wanaweza kukitumia huko waendako.

Tatizo kubwa linaonekana kwa wafungwa wetu ni ambukizo la tabia mbaya ambalo baadhi hupata wakiwa jela. Mfano jela kubwa kuna wafungwa wa kila aina yaani vifungo virefu na vifupi ambapo hawa wa vifungo vifupi huweza kupata ambukizo la tabia mbaya au usugu katika uhalifu kwa kubalishana mawazo na wahalifu wazoefu ambapo wengi wakitoka kujikuta wakishindwa kutumia mafunzo mazuri waliyoyapata jela na kujikuta wakiendelea na tabia zao za kale ambapo saizi huwa mbaya zaidi kutokana na kutohofia tena jela kwani tayari anajua mazingira yote.

Changamoto nyingine ni kuwa kilimo hakilipi sana hata kama utamfundisha mtu na aka qualify lakini akitoka nje changamoto anazokutana nazo wengi huona wanapoteza muda na badala yake hurudia shoti cuti zao za uwizi na ujambazi na Magereza kuonekana ni chuo/sehemu inayokomaza watu uhalifu au uteasaji tu.

Mitaji kwa wafungwa hasa wale wanaomaliza vifungo vyao baada ya kupata ufundi huwa shida sana na wengi kuishia mtaani ambako wanashindwa kuendeleza ujuzi walionao.

Mwisho elimu nyingi za wafungwa ni duni sana kwa maana hivyo hata ufundishwaji wake huchukua muda mrefu na ile mentality ya kufanya kazi au kufundishwa kitu ambacho hukuwa na option nacho huondoa molarity ya wao kujifunza kwa moyo mmoja.

Nikiachana na hilo Magereza hivi karibuni ilitoa mfungwa mmoja aliye gratuate sheria kwa njia ya Open Univeristy na hilo kuthibitisha Magereza unaweza kujiendela kama una msingi wa elimu.

Hata hivyo nasikia humo jela bado kuna programme za kufundisha wafungwa wasiojua kusoma na kuandika kwa kutumia wafungwa wenzao ambao hawakukimbia umande.

Nadhani utakuwa umepata picha fulani mkuu. Hiyo ni kwa jinsi niijuavyo Magereza kupitia vyanzo vyangu.
 
Naomba nikujuze kwa uhakika Magereza inatoa elimuvkwa njia nyingi tofauti na study za darasani kwa njia ya ufundi. Lengo kuu la Magereza ni urekebishaji wa wafungwa.

Magereza ina viwanda ambavyo wanaowafundishwa kazi za study mbalimbali ni wafungwa na wengine wanapomaliza vifungo vyao huwa mafundi kamili ambapo ufundi huo wanakuwa wameupata jela.

Hali kadhalika Magereza pia inajishughulisha na kilimo, na mfano yapo Magereza mbali mbali ya kilimo ambapo wafungwa hufun2wa kilimo bora ili baadae wakitoa wanaweza kukitumia huko waendako.

Tatizo kubwa linaonekana kwa wafungwa wetu ni ambukizo la tabia mbaya ambalo baadhi hupata wakiwa jela. Mfank jela kubwa kuna wafungwa wa kila aina yaani vifungo virefu na vifupi ambapo hawa wa vifungo vifupi huweza kupata ambukizo la tabia mbaya au usugu katika uhalifu kwa kubalishana mawazo na wahalifu wazoefu ambapo wengi wakitoka kujikuta wakishindwa kutumia mafunzo mazuri waliyoyapata jela na kujikuta wakiendelea na tabia zao za kale ambapo saizi huwa mbaya zaidi kutokana na kutohofia tena jela kwani tayari anajua mazingira yote.

Changamoto nyingine ni kuwa kilimo hakilipi sana hata kama utamfundisha mtu na aka qualify lakini akitoka nje changamoto anazokutana nazo wengi huona wanapoteza muda na badala yake hurudia shoti cuti zao za uwizi na ujambazi na Magereza kuonrekana ni chuo/sehemu inayokomaza watu uhalifu au uteasaji tu.

Mitaji kwa wafungwa hasa wale wanaomaliza vifungo vyao baada ya kupata ufundi huwa shida sana na wengi kuishia mtaani ambako wanashindwa kuendeleza ujuzi walionao.

Mwisho elimu nyingi za wafungwa ni duni sana kwa maana hivyo hata ufundishwaji wake huchukua muda mrefu na ile mentality ya kufanya kazi au kufundishwa kitu ambacho kuhuwa na option nacho huondoa molarity ya wao kujifunza kwa moyo mmoja.

Nikiachana na hilo Magereza hivi karibuni ilitoa mfungwa mmoja aliye gratuate sheria kwa njia ya Open Univeristy na hilo kuthibitisha Magereza unaweza kujiendela kama una msingi wa elimu.

Hata hivyo nasikia humo jela bado kuna programme za kufundisha wafungwa wasiojua kusoma na kuandika kwa kutumia wafungwa wenzao ambao hawakukimbia umande.

Nadhani utakuwa umepata picha fulani mkuu. Hiyo ni kwa jinsi niijuavyo Magereza kupitia vyanzo vyangu.

Kweli kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom