Magenius wa Bongo: Jengo la gorofa 7 hatarini kuanguka kariakoo

Wakuu........nina swali kidogo.......hivi tunayo Building Code yetu?....
............otherwise kwenye masuala haya ujenzi.........ethics mbovu zinaangusha sana umakini wa kazi hizi za kiufundi............

Hatuna mkuu! TBS angalau wamejitahidi kudevelop, kilichomo ni copy na paste ya british!-na haina nguvu yoyote kisheria
 
Hatuna mkuu! TBS angalau wamejitahidi kudevelop, kilichomo ni copy na paste ya british!-na haina nguvu yoyote kisheria

Duuh thats whay we are doomed kwenye hii fani ya ujenzi wa nyumba.............

Wanasiasa nao badaal ya ku-emphasize mambo ya policy........wanakimbilia kufukuza wahandisi (ili wawe polplar).........kumbe chanzo cha udhaifu hawakijui/hawataki kukishughulikia.......na ndio sababu tunaishia kuwalipa pesa nyingi victims wa mambo kama hayo...........
 
crb walienda wakauliza nani anaesimamia wakaonyeshwa jamaa mmoja wa darasa la saba

wakaulizwa engineer wakaonyeshwa jamaa mmoja anadai alimaliza ftc dit mnaokumbuka

wakachoka walipoangalia docs wakakuta zote ni halali

na zimepigwa muhuri yoote inayotakiwa mmiliki akajifunguia ndani

hiyo ndio tanzania

mi ningekuwa mkuu wa wilaya huyop wa darasa la saba mnampeleka

veta akaongezee ujuzi,...mtu muhimu sana kwa kiwango kilichopo cha gorofa kwa darasa la saba

hongera zake

Niliwahi kuongea na rafiki yangu mmoja tuliyesoma naye sekondari. Ni tajiri sana na ana kampuni yake ujenzi; eti yeye mwenyewe ndiye injinia wa kampuni ile. Nilimpinga kuwa uzoefu wake hawezi kuulinganisha na utaalamu wa mhandisi, na ili kumthibitishia nikumwuliza maswali madogo sana katika structural engineering ambayo alishindwa. Ni wazi kuwa mtu wa aina hiyo akipewa mradi wa kujenga ghorofa, atalivaa bila kutambua kuwa kuna details nyingi za kihandisi zinazotakiwa kufuatwa ambazo huzijui; matokeo yake ndiyo hayo hapo juu.
 
kichuguu.. kitu kimoja ambacho huwa pia kinatokea sana ni suala la "njia za mkato".. tumejifunza kutumia njia za mkato kiasi kwamba tumezoea mno hata ile njia ndefu tumeshaisahau..
 
kichuguu.. kitu kimoja ambacho huwa pia kinatokea sana ni suala la "njia za mkato".. tumejifunza kutumia njia za mkato kiasi kwamba tumezoea mno hata ile njia ndefu tumeshaisahau..

LOL! Mpaka ile njia ndefu imeota manyasi!! una pita mahali kuna kibao kabisa 'usipite hapa' lakini unapita hapo hapo!
 
Hapa wakuu Mwanakijiji na Waberoya mmegonga kwenye mzizi hasa wa matatizo yetu katika Tanzania. Wote tumelemaa kuamini kuwa kuna njia ya mkato kwa kila jambo: katika kutafuta utajiri, watanzania tunafikiria kuiba au kupata dili la rushwa; katika kupata elimu, watanzania tunafikri kununua PhD online; katika kupata madaraka, watanzania tunafikiria takrima; katika kutupa takataka, watanzania tutatupa popote bila kutafuta sehemu maalumu ya kutupa takataka. Ili mradi tu iwe ni njia ya mkato.

Sijui kama kweli kuna siku tutabadilika kimawazo na kuanza kufuata ile njia sahihi ambayo ni ndefu. Kwanza sijui kama kweli tutakumbuka kuondoa manyasi kwenye njia hiyo.
 
Back
Top Bottom