Magenius wa Bongo: Jengo la gorofa 7 hatarini kuanguka kariakoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magenius wa Bongo: Jengo la gorofa 7 hatarini kuanguka kariakoo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Timtim, Mar 11, 2010.

 1. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Jengo la gorofa 7 hatarini kuporomoka Kariakoo barabara ya Swahili/Mafia. Jengo lenyewe bado halijamalizika ujenzi wake. Hali ya hatari imewekwa kwa kuondolewa majirani wote karibu na jengo hilo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. William Lukuvi, mchana huu, alitembelea jengo la ghorofa saba lililopo Mtaa wa Mafia na Swahili, Kariakoo jijini Dar, lililopigwa marufuku na Halimashauri ya jiji, kuendelea kujengwa kutokana na ujenzi duni unaotishia usalama wa wakazi wa enoe hilo. Mh. Lukuvi akiwa na Bodi ya wakandarasi wa Halmashauri ya jiji walilitembelea jengo hilo na kulikagua sehemu mbalimbali. Baada ya ukaguzi huo, nyumba zaidi ya tano zenye miradi mbalimbali ikiwemo Hoteli na maduka na wakazi wake walitakiwa kuhama mara moja kuepuka jengo hilo linalotishia kuanguka wakati wowote. Je, katika suala hili, nani wa kulaumiwa iwapo jengo hilo litaanguka na kuwadhuru wengine na pia gharama za kuhama na usumbufu wake kwa majirani, nani atazibeba? Ni baadhi ya maswali tata yakujiuliza katika kadhia hili..!

  [​IMG]
  ...hili ndilo Jengo linalotishia usalama

  [​IMG]
  ...Mh. lukuvi akishuka ghorofani baada ya kulikagua.

  [​IMG]
  ..Mh. Lukuvi (katikati) na ‘mainjinia' wa Halmashauri ya jiji wakiziangalia nyumba za jirani na jengo hilo ambazo wamewapiga stop wakazi wake kuendelea kuzitumia.

  [​IMG]
  ...Nyumba hizi tatu za mbele zote wakazi wake wametakiwa kuhama mara moja.

  [​IMG]
  ...Umati wa watu ukilitazama jengo hilo.

  [​IMG]
  Nyumba hii nayo wakazi wake wametakiwa kuhama mara moja.

  [​IMG]
  mpaka jengo linafikia hatua hii, mamlaka husika zilikuwa wapi?

  PICHA: Richard Bukos/GPL
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hayo mabiskuti ya kariako6 very soon yatatuliza jiji wapo lkn ujenzi usio na viwango umeshamiri
   
 3. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Concrete Jungle...
   
 4. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Walau picha basi tuone.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Toba yarabi.. tukubali tu yaishe..
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  crb walienda wakauliza nani anaesimamia wakaonyeshwa jamaa mmoja wa darasa la saba

  wakaulizwa engineer wakaonyeshwa jamaa mmoja anadai alimaliza ftc dit mnaokumbuka

  wakachoka walipoangalia docs wakakuta zote ni halali

  na zimepigwa muhuri yoote inayotakiwa mmiliki akajifunguia ndani

  hiyo ndio tanzania

  mi ningekuwa mkuu wa wilaya huyop wa darasa la saba mnampeleka

  veta akaongezee ujuzi,...mtu muhimu sana kwa kiwango kilichopo cha gorofa kwa darasa la saba

  hongera zake
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Yaani bongo tunakabiliwa na majanga kila upane..Janga la uwajibikaji katika kazi,nidhamu ya raslimali,janga kubwa kuliko yote ya uongozi na uadilifu.

  -Mkuu Waberoya hapa tunahitaji mchango wako
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  as if ma injia wa kweli hawapo! nchi ikiendeshwa na genge la wahuni ndo matokeo yake hayo
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Darasa la saba? Kweli ana kipaji.kakabidhiwa dhamana kama hiyo?

  -Nadhani Tanzania matatizo yetu ni makubwa kuliko tunavyofikiri
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Hilo jengo mtoa maada una hakika lilianzia chini? naona kama watu wameongeza illegal storey kwenye existing structure!

  Majengo kama hayo kupata solution ni mpaka ufanye investigation ya kutosha sana ndio uamu eufanye nini, lakini gharama la restoration wakati mwingine ni kubwa kuliko ujenzi huo ulipofikia.

  Still we have big problem in the walls, unaona mimatofali ilivyojaa ukutani; that is a simple indictator kuwa hatufanyi utafiti wa kutafuta materials yaliyo light but durable kwa ajili ya kuta.

  Mkuu, hakuna issue ya u-genius hapo, kuna vitu ukivikosea kuanzia mwanzo solution ni kubomoa na kuanza mwanzo!

  Kama ukimwi vile, kama uliupata kwa uzembe wako, ndio nitolee!

  Still ukifdananisha na wengine, duniani bado majengo yetu mengi hayahanguki wakati wa ujenzi kama nchi zingine, hata south africa tumewaacha mbali sana.

  However, tishio pekee ambalo linahitaji immediate attention ni majengo yote ya kariakoo kuwa yawekwe katika majengo ya hatari kwani kwa standard ya Tanzania hayajajengwa kuhimili MATETEMEKO ya ardhi, ndio maana ni cheap na yeyete yule anajenga kilaini! likitokea tetemeko ambalo lina ritcher scale zaidi ya 5! maafa,
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tuna matatizo wabongo!!! sasa nasubiri kuambiwa hili nalo limesababishwa na JK.

  Maana hatukosi pa kupeleka lawama... badala ya kuanza na sisi wenyewe na taaluma zetu.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  una hakika wametumia wataalamu? kuna wa darasa la saba wanasimamia majengo haya!

  hapa ni kwa wenye fedha, wanapenda shortcut
   
 13. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Yes, nina uhakika wametumia wataalamu kwa sababu vibali wamepata Halmashauri ya Jiji, hivyo wataalamu wa Halmashauri ya Jiji walistahili kuangalia development ya hilo Jengo...

  Alafu kwa nini unashangaa hilo? Yule aliyechora ramani ya barabara ya Mandela kuwa exactly ile ile iliyochorwa miaka zaidi ya 20 iliyopita alikuwa naye darasa la saba?]

  Muda wa kuacha kuwatupia kila kitu wanasiasa umepita... hili ni la Halmashauri na Mhandisi wao.... Hivyo vibali vya ujenzi sio vibali vya kuingiza pipi nchini ... maendeleo ya jengo lazima yafuatiliwe kadri kila ghorofa zinapoongezeka.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Mkuu hakuna sehemu niliyosema wanasiasa wanahusika, mimi kwa knowledge yangu nina hakika owners wa hayo majengo ndio wanahusika. Vibali?? watu Tz wanaishi kwa mihuri ya wanahandisi fulani

  Kinachoendelea ni kuwa watu wana wa approach wahandishi wenye vibali, hao jamaa wanapiga mihuri document zote zinapozenda kwenye hizo halmashauri zinakuwa clean, ERB na halmashauri kitu wanacholaumiwa kila siku ni kutofanya ukaguzi wa mara kwa mara katika haya majengo wakiwemo personel wanaosimamia huo ujenzi, wanachajitetea wao ni wana watu wachache!

  Kama kweli owners wa nyumba, wanazipata fedha kihalali, wakawatafuta archtects wazuri, sidhani kama hao archtects wanawatafutia wahandisi wabovu.

  Haiwezekani majengo mazuri kama ya BOT, PPF tower mafuta, n.k yawe designed na watanzania na mengine kama hili nayo yawe designed na watanzania.
  My argument hapa sio taaluma, kama ulivyosema hapo awali, maana ushahidi tunao wa wahandisi waliofanya kazi za kutukuka!

  Tatizo ni usanii, kuruka taratibu, shortcut, ufisadi wa hapa a pale, ambao liko katika ethics na sio utaalamu. labda kama sikukuelewa

  hao halmashauri na mhandisi wao kutosimamia vizuri na kutoa vibali vizuri, siyo utaalamu, ni ethics zemye element za ufisadi.

  utaalamu nilivyokuelewa hapo awali ni kuwa mtu anashindwa kukadiria nondo ziwe ngapi kwenye nguzo! tukifikia sehemu tuna wataalamu ambao wanashindwa kufanya mahesabu sawa sawa na kusababisha majengo yaanguke, basi huo ndio utaalamu!
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Bongo inamalizwa na mambo makuu matatu.
  1. Siasa
  2. Rushwa
  3. Kupenda mteremko/mterezo (slope - dy/dx)

  Siasa - Kila mwanasiasa anajifanya anajua kila kitu na hata kuingilia maamuzi ya wataalam wakiona yanaenda kinyume na wao kukosa KULA (Kura). Mtu anajifanya Engineer, Daktari, Mwanasheria kwa kuwa tu amepewa dhamana ya kufanya maamuzi kwa kuchaguliwa kushika nafasi ya kisiasa.

  Rushwa - Kutokana na kila mtu kutaka mafanikio ya haraka haraka basi watu wapo tayari kuacha professional zao kuruhusu vitu kufanyika kinyume na taratibu ili mradi tu amepewa kitu kikubwa

  Kupenda mteremko/mterezo - Mtu anaona kumuajili mtaalam aiyequalify ni gharama kubwa na kuamua kutumia watu wenye utaalam wa chini bila kujali usalama wa raia ili mradi afanikishe kile anachihitaji. Utamaduni huu unaanzia kwa wanasiasa wetu ambao hawapo tayari kuona mtaalamu wa ndani analipwa kiasi kikubwa kwa kazi anayodhani itafanyika kwa kiwango cha kuwadanganyia wananchi tu ili achaguliwe.


  My take: Umefika wakati sasa Siasa kukaa pembeni kwenye mambo yanayohusu usalama wa raia na mali zao, na pindi mwanasiasa anapoingilia hayo basi likitokea janga abebeshwe mzigo yeye siyo tu kwa kulaumiwa kwani lawama kwa Tanzania hazina hasara bali kwa kushitakiwa na kufungwa kwa kosa la uzembe. Nafikiri hii itawafanya waache ujuaji wasiokuwa nao.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Yes, at a glance, the problem here is rushwa na kupenda mteremko;

  Ukiona jengo lolote mtu anamlaumu mhandisi basi ujue, tayari kuna stage ilirukwa , client anatakiwa awe close na archtect, wasanifu ndio wanatafuta wahandisi!
  sidhani kama kuna archtect mzuri atatafuta mhandisi bomu.

  onwer anaambiwa ukifuata procedure na kuajiri wataalamu, utatumia milioni 1000, ila ukitumia njia za panya unatumia milion 600! na huku tuna rekodi majengo yetu hayahanguki sana, yako mabovu kabisa yamesimama na yanaoperate!

  client anaona ni bora atumie milioni 600, ajenge haraka na rudishe mkopo wake etc. siku ukitembea uchi ndiyo unakutana na mkweo, kama hapa !

  wahandisi wanaopiga mihuri ovyo ili watu wapate vibali, ni makosa, halmashauri na ERB kutosimamia vyema ni makosa, owners kutofuata procedures ni makosa!


  kwa kifupi -ETHICS-

  kama una ethics kwenye uhandisi haijalishi mwanasiasa atasema nini! stick to what you know, kinyume na hapo hatutamwangalia mwanasiasa utaangaliwa mhandisi!
   
 17. rajab

  rajab Member

  #17
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 27, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nasema mamangu eeeehh
  hiyo ndo gunia mbilli saruji na pick up moja mchanga
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi wakati wanajenga hadi imefikia hapo.. ina maana kila mtu alikuwa anaombea kuwa nyumba itakuwa imara?
   
 19. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wakuu nimeona hii thread na naamini tusijekuwa sidetracked!
  Tatizo ya majengo haya yanayo anguka ni kutokana na sababu tatu--
  1)rushwa
  2)Rushwa
  3)RUSHWA!!!!!

  Je tume wahi jiuliza maswahili haya?
  a) Kwa nini majengo karibu yote yanayo naguka wenye mali ni Waasia na wafanyabiashara?
  b)Je umewahi kusikia mejengo ya ghorofa ya serikali/umma yakianguka?(achilia mbali
  majengo ya shule yaliyogubikwa na rushwa ya kutisha)
  c)Kwa nini majengo haya kati kati ya mji hayana ukaguzi hata wa wahandisi wa Jiji, miradi ambayo iko mbele ya macho yao?

  Uzoefu unaonyesha kuwa wenye mradi(Waasia/wafanyabiasara) wengi wao ambao si wasomi wa fani yoyote ile, wanapuuzia ushauri wa kitaalam kwa kuwalipa wakaguzi(wa Jiji) ili mabo yao yaende fasta.
  Majengo karibu yote yaliyo Kariakoo yanahitaji ukaguzi wa kina ili kuthibitisha kama yanafaa kwa makazi ya binadamu.
  Tukirudi myuma zaidi na kujiuliza kwa nini mambo haya yanatokea?
  Idara za uhandisi za Jiji na halmashauri hazifanyi kazi kitaalam na zimekaa kisiasa zaidi kuliko kuwa idara zainazojitegemea na kufanya kazi kitaalam.
  Culprit hapa ni ufutaji wa City/Town Councils miaka ya nyuma na bado hatujaweza kurudisha ufanisi waliouacha wenzetu mara tu baada ya uhuru.
   
 20. O

  Ogah JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wakuu........nina swali kidogo.......hivi tunayo Building Code yetu?....
  ............otherwise kwenye masuala haya ujenzi.........ethics mbovu zinaangusha sana umakini wa kazi hizi za kiufundi............
   
Loading...