Magazeti yatia aibu kupotosha hukumu dhidi Mwanahalisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti yatia aibu kupotosha hukumu dhidi Mwanahalisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 13, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Magazeti yatia aibu kupotosha hukumu dhidi Mwanahalisi

  Kuna habari kwamba baadhi ya wahahariri wa vyombo huru vya habari wameomba Jukwaa la Wahariri litoe tamko kuhusu upotoshwaji wa kimakusudi wa vichwa vya habari katika baadhi ya magazeti ya leo kuhusu “Order” iliyotolewa na Mahakama Kuu chini ya Jaji Robert Makaramba tarehe 30 April kuhusu kesi ya madai aliyoifungua Rostam Aziz dhidi ya gazeti la Mwanahalisi.

  Habari ambazo nimezipata kutoka baadhi ya wahariri wa magazeti zinasema kuwa magazeti yanayomilikiwa na Rostam (Mtanzania na The African) pamoja lile linalomikiwa na serikali (Habari Leo) yamepotosha aliyoagiza jaji Makaramba kwa kusema kwamba mahakama imemsafisha Rostam – kitu ambacho si kweli – Mahakama haikusema hivyo.

  Wahariri wanadai kwamba alichofanya Jaji Makaramba ni ni kutoa amri tu ya kuridhia madai ya Rostam katika shauri alililipeleka – bila kusikiliza upande wa Mwanahalisi – kwa sababu ya mawakili wa Mwanahalisi hawakuwapo Mahakamani. Kwa maana nyingine shauri halikusikilizwa kabisa, hivyo si kweli Rostam kasafishwa kuhusu madai ya umiliki wa kampuni ya Richmond.

  Wahariri wanadai kuwa uandishi wa habari wa magazeti hayo yanakwenda kinyume cha maadili ya uandishi na yametia aibu medani nzima ya taaluma hiyo muhimu kwa umma.

  Wahariri pia wamemuomba Jaji Makaramba kuyakemea magazeti hayo kwa kuandika kile ambacho hakukisema katika “Order” yake.
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Na inasikitisha kuwa miongoni mwa magazeti yaliyo 'Shout' kwa sauti kuu kwenye kurasa zao za mbele kuwa 'Mahakama yamsafisha Rostam' ama 'Rostam hana hatia' ni yale ya serikali!! Angalau 'Tanzania Daima' lilisema tu kuwa 'Mahakama yasema MwanaHalisi Limemkashifu Rostam Aziz'! Kweli, Njaa hizi zitatuua jamani!
   
  Last edited: May 13, 2009
 3. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umetaja Mtanzania, The African na Habari leo. Wewe unapata picha gani hapo? USHABIKI!


  Hapo usitegemee KUCHUKULIWA HATUA WALA MTU KUINUA MDOMO. HIZO ZOTE NI state newspapers. Tena subiri na Rai kesho watatoa na nakala ya hiyo hukumu
   
 4. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Habari leo,TBC1 kulikoni?
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Kinachonisikitisha zaidi Habari leo linaendeshwa na hela yangu. My God PAYE
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hivi RA kanunua na vyombo vya habari vya serikali? Hii aibu sasa mbona imezidi? Juzi yule mjinga nani sijuwi alipotoa lile tamko lililokosa mashiko alionya itv lakini hakuonya tbc kwa kitendo kile kile kilichofanywa na vyombo vyote viwili. Alipobanwa alidai waandishi waufuate uongozi wa tbc, kinachonichefua sijuwi kwanini pia issue ya itv hakusema waandishi waufuate uongozi wa itv bali aliishia kutoa hukumu? So for how will this go on mbona hii hali inatapisha jamani?
   
 7. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi naona kama vinamilikiwa na mafisadi=serikali
   
 8. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,585
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Tanzania ina matatizo, watu hawaelewi kuwa kichwa cha habari tu cha kwenye magazeti kiaweza kupotosha kundi kubwa sana la wananchi?

  Inabidi tufike mahali tuwe serious kidogo, asilimia kubwa ya magazeti ya leo yameandika kuwa mahakama imemsafisha Rostam kwenye ishu ya Richmond.....hivi kweli tutafika huko tuendako???
   
 9. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Kukika tutafika ila na tutafika katika hali gani!
   
 10. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii kama ni kweli wamefanya jambo la maana kwani kilichorepotiwa ni kuwa upande wa pili (MWAHAHALISI) haukutoa maelezo. Hivyo bado kuna uwezekana wa kesi kupelekwa mahakama ya juu zaidi.

  Ukiende kwenye website yao gonga hapa Gazeti la Mtanzania utaona kichwa cha habari RA ASAFISHWA. Sasa sijui kasafishwa kwa vidhibiti au maneno. Nafikiri inabidi muda ufike watu sheria kali ziwekwe ili kuzuia uhandishi wa kupotosha.

  Kesi kama hizi zinapotolewa maamuzi, je huwezi kufile upya ili upande wako usikilizwe (wale wanasheria watusaidie)? Marando ni mwanasheria mkubwa nafikiri atatoa maelezo kuwa nini kilitokea mpaka wakachelewa kupeleka utetezi.

  TIME WILL TELL HAWEZI KUKIMBIA MADHAMBI YAKE KIRAHISI HIVI.
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kinachoonekana hapa si kingine bali ni ku discredit serikali yoooote na mahakama. Vyombo vyote vya dola vimeshakosa credibility kwa wananchi, hata kama wana-bunduki na risasi, ila wajue kuwa "hearts and minds" of most Tanzanians are not with them. Hakuna hatari kubwa katika usalama wa nchi kama wananchi kukosa imani na serikali yao, hili muungwana anatakiwa kulikataa kwa kuwaweka kando wale wote wanaoonesha ushabiki wowote katika utendaji kazi wao serikalini.

  Mahakama imeshaonekana nayo ni "toilet paper" ya mafisadi jambo linaloweza kukataliwa na mahakama yenyewe kwa kutenda haki kwa kusikiliza pande zote husika kwenye shauri. Jaji Makaramba amekwisha onesha ulegevu kwenye hii hukumu yake kwani ili ufikie maamuzi yenye haki lazima usikilize pande zote husika, Natumai mahakama ya juu ita repudiate madudu ya makaramba, ili wananchi tuwe na imani kuwa Tanzania mahakama haiangaliwi wewe ni nani bali ni haki tupu inayofanyika. Kumbuka "mahakama haitakiwi tu kutenda haki bali kuonekana kuwa inatenda haki". Jaji atoe order ingine kwa watu wanaotumia hukumu yake kujisafisha yaani kumfanya jaji na mahakama ni toliet paper.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na hayo magazeti wala hawalitambui hilo jukwaa la wahariri
   
 13. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli hawalitambui basi ni kwakuwa CCM=GT=RA n PARTENERZ so UHURU=DAILYNEWZ N HABARI LEO=HABARI CORPORATION NEWS PAPERZ
   
 14. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #14
  May 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  shame on you kikwete and ur government!
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Well hata wasipo litambua, lakini hoja yake je? Ni kweli habri imepotoshwa ama ndivo ilivo?
   
 16. u

  urithiwetu Senior Member

  #16
  May 13, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RA ndiye "mwenye" nchi hii. Ndio maana mawaziri walishindana kumtetea. Inaonekana kuwa vyombo vya habari vya Serikali na vya CCM vyote "vinawajibika" kumtetea kwa nguvu zote. Wote wanajipendekeza tu kwa RA. Mkuchika kamsakizia Mzee Bendera kusema pumba; anamsema jasiri Mengi wanamuogopa fisadi Rostam, Wanaisema ITV wanaiacha TBC.
  Viongozi serikalini wanamuogopa vibaya RA, ati ana ubavu na vibarua vyao.
  Masikini Tanzania!
   
 17. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna mtu alisema yeye ni serikali na serikali ni yeye!
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  DR. SLAA next PRESIDAA
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  WOULD THIS DREAM COME TRUE?

  Dunia ingekuwa mahali pema kabisa pa kuishi...
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hii kitu inawezekana kabisa. Unafahamu, ukisema tuiondoe CCM, inaleta ugomvi sana. Ila ukisema Dr Slaa for PRESIDAA, hata wana CCM watetezi wakubwa humu ndani wanakubali hilo. Nina uhakika wengi wataweza kumkubali Dr. kuliko Mbowe. Mbowe anafaa kuwa Boss wa chama na sanasana mbunge. Tanzania siyo Madascar.

  Mie nshajitangaza MPIGA DEBE wa SIKONGE namba 1 wa Dr. Wenzangu nakusubirini huko mliko na nyie muanze. Inabidi tutengeneze MTANDAO mkubwa sana na kutumia means zote za KISASA/KISOMI. Kwa nini akina RA wawe wanatuwekea watu wao?

  YES DR. SLAA NEXT PRESIDAA.
   
Loading...