Magazeti yanayoongoza kwa kusomwa nchini

mhalisi

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
1,181
320
wadau ninapenda kujua magazeti mawili yanayoongoza kwa kusomwa sana na watu hapa nchini?
 
Unge-specify category ya gazeti. Magazeti serious au ya udaku? Kwa ujumla, magazeti ya udaku ndo yanaongoza kwa kusomwa zaidi. Sababu kubwa ya kuongoza ni kwamba, magazeti hayo yanasomwa na kila mtu, hayabagui(non selective) na hayamfanyi mtu atafakari sana na kuumiza kichwa. Tofauti na magazeti serious ambayo yanasomwa zaidi na watu makini, wasomi, wanasiasa etc. Mfano ni vigumu kumkuta mtu wa kijiweni akisoma rai, financial times au majira ila ni rahisi kumkuta akisoma sani au ijumaaa
 
Kwa mujibu wa utafiti ambao sio rasmi,magazeti yanayoongoza kwa kusomwa kila siku ni Mwananchi likifuatiwa na Tanzania Daima. Alafu Nipashe linafuatia.
Kwa magazeti ya kila wiki ni Mwanahalisi likifuatiwa na Raia Mwema.
Na kwa gazeti la Michezo na Burudani ni Mwanaspoti.
Ukitaka kugundua ni magazeti gani yanasomwa sana jaribu kutembelea mahali panapouzwa magazeti au yule mtu anayetembeza magazeti,na utazame ni nakala ngapi anazo kwa kila gazeti. Au umuulize kwa kila gazeti anauza nakala kiasi gani. Nadhani utapata majibu.
 
Unge-specify category ya gazeti. Magazeti serious au ya udaku? Kwa ujumla, magazeti ya udaku ndo yanaongoza kwa kusomwa zaidi. Sababu kubwa ya kuongoza ni kwamba, magazeti hayo yanasomwa na kila mtu, hayabagui(non selective) na hayamfanyi mtu atafakari sana na kuumiza kichwa. Tofauti na magazeti serious ambayo yanasomwa zaidi na watu makini, wasomi, wanasiasa etc. Mfano ni vigumu kumkuta mtu wa kijiweni akisoma rai, financial times au majira ila ni rahisi kumkuta akisoma sani au ijumaaa

very sure..
1. mwananchi - 24,000 kwa siku
2. Tz daima - 21,000 kwa siku
3. nipashe - 18,000 kwa siku
 
Unge-specify category ya gazeti. Magazeti serious au ya udaku? Kwa ujumla, magazeti ya udaku ndo yanaongoza kwa kusomwa zaidi. Sababu kubwa ya kuongoza ni kwamba, magazeti hayo yanasomwa na kila mtu, hayabagui(non selective) na hayamfanyi mtu atafakari sana na kuumiza kichwa. Tofauti na magazeti serious ambayo yanasomwa zaidi na watu makini, wasomi, wanasiasa etc. Mfano ni vigumu kumkuta mtu wa kijiweni akisoma rai, financial times au majira ila ni rahisi kumkuta akisoma sani au ijumaaa
sikubaliani nawe kuwa magazeti ya udaku yanasomwa NA KILA MTU. Mimi siyasomi. Ulichomaanisha ni kwamba magazeti ya udaku YANAWEZA KUSOMWA NA KILA MTU nikimaanisha kuwa kuna watu ukimpa Raia Mwema au Mwanahalisi asome ni kama umempa kitabu cha Quantum Physics akisome.
 
hahahaaaaaaaaaaaaa! kua mtu niliwahi kumpa ndani ya sekund 20 baada ya kumpa akanirudishia, nikamuuliza vp, akadai yeye sio mwanasiasa
 
Kiu, Ijumaa, Uwazi..Haya ya Udaku.

Mwananchi, Nipashe, Tanzania Daima..Haya kila siku.

Raia Mwema, Mwanahalisi, Kila Jumatano
 
  1. Mwananchi
  2. Mwanahalisi
  3. Mwanaspoti
  4. Tanzania Daima
  5. Raia mwema
hata unazungumzia per issue au per week au??

nijuavyo mimi mwanahalisi na raia mwema yanasomwa zaidi dar kwa kutokua na good distribution strategy and representation
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom