Uchaguzi 2020 Magazeti yanatumia hekima gani kuandika Habari katika kipindi hiki cha Uchaguzi?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
2,886
2,000
Nimepita juzi kwenye Meza ya magazeti nikastaajabu kidogo.

Habari kuu za magazeti yote ni za Mgombea wa CCM.

Rangi ya kijani imetapakaa Meza nzima yani kama ukiangalia kwa mbali unaweza kudhani ni Meza ya muuza mbogamboga.

Nikajiuliza mbona twitter na JF Mpambano ni kama umebalance hivi japo kuna siku Habari kuu za JF zote pale kuu zilikuwa ni za CCM.

Kiukweli watu wanapenda kusoma Habari za upinzani maana zinaleta vitu tofauti maana za CCM zipo tangu 70s.

Je, wameshinikizwa?

Habari za CCM msimu huu zinauza kuliko Wapinzani?

Wapinzani hawana ushawishi humo kwenye media houses?

Wapinzani wamegomewa mgomo baridi?

Hawana cha maana cha kuongea?

Au mgombea wa Upinzani Jana yake alikuwa mapumziko?

Nimewaza tu hivyo, nikaamua Nile zangu Kona lakini niilete humu kwa wajuzi.
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
2,886
2,000
Hili suala liko sehemu nyingi sana (sio mitandaoni) mpaka mitaani, barabarani, vijijini n.k. unaweza kudhani mgombea no ccm tu. Hata posters hamna, bendera zimekuwa adimu ..kuna tatizo mahali sio bure!
Nashukuru na wewe kugundua hilo.
Kila siku zote uchaguzi ambao rais aliyeko madarakani anagombea na ule ambaye mgombea wa chama tawala ni Mpya huwa unaradha tofauti.

Huu wa sasa unagap Kubwa sijawahi kuona. Na isingekuwa lissu jamaa angekula kama asilimia za kagame 98+%
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,234
2,000
Chadema hawana hela ya kuweka matangazo
Mji ninaokaa mimi waliweka mabango na bendera za CHADEMA nyingi tu. Kesho yake tukaamka hakuna hata kimoja. So bora waache tu wasiweke. Pia kwenye billboards wameambiwa walipie TRA otherwise hakuna kuweka. Ila likiweka halitashinda hata walilipia TLB.
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
2,886
2,000
Mji ninaokaa mimi waliweka mabango na bendera za CHADEMA nyingi tu. Kesho yake tukaamka hakuna hata kimoja. So bora waache tu wasiweke. Pia kwenye billboards wameambiwa walipie TRA otherwise hakuna kuweka. Ila likiweka halitashinda hata walilipia TLB.
Nakumbuka Mwanza uchaguzi uliopita kulikuwa na vita vya kuweka bendera jijini.
Lkn chadema walikomaa.

Ila hiyo spirit haipo msimu huu. Chadema nchi nzima jasiri ni Lissu tu, naye kwa sababu labda anabackup ya mabeberu au amewahi kukoswakoswa na Israel hivyo hana cha kuogopa tena.
 

goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,162
2,000
Maagizo kutoka juu hayo, zinatakiwa kuandikwa/kuoneshwa habari za yesu wa chatoo tuu na sio vinginevyo. Umechelewa sana kugundua hilo mkuu.
 

maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
920
1,000
Nimejiuliza sana kuhusu hilo, lakini nafikiri ni hofu iliyowajaa wapenzi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA kutokana na matukio mbalimbali wanapoweka bendera zao, kumbuka tukio la kushushwa bendera za CHADEMA Chato.
Maeneo kadhaa ya vijiwe ambavyo vimeweka bendera za CHADEMA wahusika wamekuwa wakipata usumbufu, cha kushangaza bendera za vyama vingine hazina tatizo.
Watu wamebaki kuibeba CHADEMA mioyoni.
 

Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
5,860
2,000
Iko wazi, kila mtu anajua nini kinaendelea kwa wahariri. Kuna uzi uliwekwa humu unaonyesha vichwa karibia 6 vya magazeti vyote vina tittle moja.

Wenye nchi yao ndo wanaamua story gani iwe published. Taaluma haina nguvu tena mkuu.
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
979
1,000
Matokeo ya Sheria zilizotungwa ,kupitia miswaada ya hati za dharura,kwa malengo mahsusi .Nayenye mirengo Fulani.
 

Mr Mvua

Member
Aug 29, 2020
88
125
Hao wrote watatafuta pakutokea.acha wawe waoga.ila niwakuwahurumia sana.maana miaka mitano ya bani c nchezo.

Ila wakumbuke wanayoyafanya vitakuwa ushahidi one day.

Kijani atapigwa hivyohivyo.mapenzi hutoka moyoni na machoni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom