Magazeti yahaha kutafuta Skendo za wabunge vijana Dodoma

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Uvumi kuhusu skendo za wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa Dodoma, sasa unaweza kupatiwa jibu lililonyooka kutokana na kazi makini ya kuwakagua iliyofanyika kwenye hoteli walizofikia.

The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko lilitinga Dom wiki iliyopita na kuzunguka chumba kwa chumba ndani ya hoteli ambazo wabunge wameweka kambi na kujionea hali halisi ya maisha ya waheshimiwa hao.
Ripoti ya jumla ya kila mbunge aliyekaguliwa na gazeti hili ipo kama ifuatavyo;
Mkosamali, Mhambwe.
FELIX FRANCIS MKOSAMALI
Jimbo: Muhambwe
Chama: NCCR-Mageuzi

Gazeti hili lilimtembelea mbunge huyo kijana Alhamisi iliyopita majira ya saa 3:00 asubuhi. Lilimkuta akiwa kwenye pirika za uwakilishi wake bungeni.
Katika kuthibitisha kuwa hakuwa na shaka yoyote ya maisha yake Dom, aliongozana na mwandishi hadi chumbani kwake kwenye Hoteli ya Kitemba, Barabara ya Saba mjini humo.
Mkosamali mwenye umri wa miaka 24 alisema kuwa ingawa yeye ni mdogo zaidi bungeni lakini atathibitisha uwezo wake kwa hoja nzito, zitakazolenga kuwatetea wananchi wa Buhambwe, pia kuiokoa Tanzania.

“Kama kuna watu wana shaka na mimi, nakaribisha mijadala hata na maprofesa, sina shaka. Bungeni hakuna kubeba mawe, hapa ni kuonesha uwezo wa kichwa, hilo najiamini na nitasimamia zaidi hoja ya elimu kwa sababu Tanzania tumelala sana,” alisema Mkosamali.
attachment.php
Sugu, Mbeya mjini.
JOSEPH OSMUND MBILINYI ‘SUGU’
Jimbo: Mbeya Mjini
Chama: CHADEMA
Jumanne iliyopita majira ya saa 11 jioni, paparazi wetu alishika kasi ya kumtafuta Sugu ili kufunua maisha yake Dom.

Baada ya kuelezwa kwamba anaishi kwenye Hotli ya Desert, Area C, moja kwa moja alibisha hodi na kukaribishwa hadi ndani.
Sugu (pichani) alikuwa peke yake akiwa ameuchapa usingizi. Alisema: “Dah umeshtukiza unafikiri kuna kitu? Nimelala tu napunguza uchovu wa safari na pirika za bunge tangu asubuhi.

“Nawaheshimu sana wapigakura wangu wa Mbeya Mjini, wamenituma kufanya kazi na siyo kustarehe. Kama ni starehe mimi nipo kwenye game (muziki) zaidi ya miaka 20, huko ndiyo kuna starehe, hapa ni kazi tu.”

VICKY KAMATA ‘MADAME V’
Viti Maalum, Geita
Chama: CCM

Gazeti hili lilimshtukiza kwenye hoteli aliyofikia ya Royal Village, Area D na kumkuta akiwa ‘bize’ akitengeneza nywele, ilikuwa Alhamisi mchana baada ya kutoka kwenye kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, kilichoketi kupitisha jina la Anna Makinda kuwa mgombea wa uspika.
Vicky alikuwa na ndugu yake chumbani kwake akimtengeneza nywele na alipokutanisha macho na paparazi wetu hakuwa na shaka ya aina yoyote.
Msigwa, Iringa mjini.
MCH. PETER MSIGWA
Jimbo: Iringa Mjini
Chama: CHADEMA
Paparazi wetu alimkuta mbunge huyo kwenye Hoteli ya Desert, alikuwa ‘busy’ na kompyuta yake ndogo (laptop).
Mayenga, Viti maalum.
LUCY MAYENGA
Viti Maalum, Shinyanga
Chama: CCM
Gazeti hili halikufanikiwa kunusa mahali alipo lakini liliweza kumnasa mbunge huyo akiwa ‘busy’ na kipima joto chake, akitafuta kitu ambacho paparazi wetu hakuweza kujua mara moja.

Hiyo ilikuwa Jumatano iliyopita, majira saa 6 mchana kwenye viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
CLUB 84

Wabunge wawili wapya, mmoja wa CHADEMA na mwingine CCM, pia mwingine aliyeongoza moja ya wizara nyeti walijirusha club mpaka jirani na majogoo lakini waliondoka kila mtu kwa nafasi yake bila ‘vimeo’.
 

Attachments

  • 8.jpg
    8.jpg
    50.7 KB · Views: 259
  • 7.jpg
    7.jpg
    56.7 KB · Views: 279
  • 6.jpg
    6.jpg
    50.2 KB · Views: 276
  • 12.jpg
    12.jpg
    69.8 KB · Views: 264
Bwana mdogo Mkosamali nasikia warembo wa mjengoni wanammendea kwa kasi ya ajabu mwaka huu kwa kweli tutasikia vituko kibao toka hili Bunge la MA-kinda
 
Mheshimiwa sugu tafadhali, can U put on a shirt!, inabidi wengine tuangalie huku tumefumba macho!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom