Magazeti ya Tanzania na takwimu za wakuu wa Wilaya, ndio maana serikali huyafungia

Hebu angalia waandishi wetu wanavyotofautiana kwa takwimu yupi tumwamini .

Je kutoa takwimu zisizo sahihi kisheria likoje hilo wataalamu wa takwimu ??
 

Attachments

  • 1467034350434.jpg
    1467034350434.jpg
    43.1 KB · Views: 33
Kati ya vitu ambavyo Tanzania ina uhaba navyo ni Investigative Journalist, kama kwa jambo dogo kama hili tu wanakosa data za ukweli ni kipi watakiweza, huwa nawachukulia sana wanahabari kama chombo ambacho kinaweza kutufikisha mbali sana na hasa hawa waandishi wa habari za kichunguzi.. Mfano katika vita vya madawa ya kulevya hawa jamaa wangetusaidia sana, Tunajua kwamba kuna watanzania wengi wamefungwa magereza huko ughaibuni hususani China, tulitegemea waandishi wangefunga safari mpaka huko wakachukue data kwa hao wafungwa halafu waje watoe kinagaubaga, hii ingesaidia sana kujua mapapa wanaohusika na ishu ya madawa ya kulevya, yapo mengi sana ambayo hawa jamaa wangeweza kututatulia lakini ndo hivyo tena....Nilikuwa na hamu ya kuja kuwa mwandishi ila nikakimbilia uhandisi leo nimebaki tu kama mshabiki wa habari baada ya kukosa role model wakuni inspire
 
Mkuu cheguevara ukisema tuwafunge hawa kwa makosa kama haya utawafunga waandishi wote, si mara ya kwanza kutokea kwa mkanganyiko kama huu, kuna yale mapigano ya askari na majambazi Mwanza, kila gazeti lilikuja na muda wake lingine linasema majibizano ya risasi yalidumu masaa 72 lingine 36 lingine vile, yaani elimradi yauze tu
 
Mtoa mada inaonekana huwa hauko makini kwenye kusoma. Hivi nikikwambia nimeacha wanafunzi 10 na nikakwambia nimeacha wanafunzi 7 wa mzee juma , je inamaanisha ile kauli ya kwanza ya wanafunzi 10 si sahihi? Inawezekana kabisa waliachwa wa3 wa mzee Hassan na saba wa mzee Juma
 
Mtoa mada inaonekana huwa hauko makini kwenye kusoma. Hivi nikikwambia nimeacha wanafunzi 10 na nikakwambia nimeacha wanafunzi 7 wa mzee juma , je inamaanisha ile kauli ya kwanza ya wanafunzi 10 si sahihi? Inawezekana kabisa waliachwa wa3 wa mzee Hassan na saba wa mzee Juma
usiwe mbishi, kuna shida ya kukurupuka hapo
 
Back
Top Bottom