Magazeti ya MwanaHALISI na Tanzania Daima kiini macho pia????

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
771
1,000
Mimi nadhani humu JF watu wengi tumeingia katika kupalilia mgogoro mkubwa ulio ndani ya CHADEMA ili hali tunajua hali itakuwa mbaya sana kama tutaamua kumwangamiza kiongozi mmoja na wengine kuendelea...

Mimi namfahamu Zitto kama mwanasiasa machachari na ambaye anatafuta too bright future ahead.. Lakini pale CHADEMA kuna watu kama Komu aliyeshindwa ubunge Moshi na ambaye ana miliki gazeti la mwanahalisi na Bosi wa fedha CHADEMA... Kusema kweli hili gazeti linamchafua Zitto kwa Say ya huyu jamaaa... Zitto kutaka uenyekiti ni kweli lazima lilikuwa chanzo cha tatizo lakini Zitto bado ana nafasi kubwa CHADEMA aachane na hiyo post... Haya tuachane na Komu na MwanaHALISI lake!!

Pia kuhusu Zitto kutokufika bungeni kabisa siku ile ni contraversial sana kwa kuwa hakuna ambaye amejua exactly what did he meant... Kitendo kile binafsi kiliniudhi saana japo justification yake ya kusema JK alisaidia Kigoma sio sahihi kama yeye aliandamana pale Kigoma Ujiji kupinga matokeo ya ndugu Serukamba... Huu ni ukweli kwamba yeye pia aliamini na anaamini kuwa CCM ni wachakachuaji wakubwa saaana.. Mimi sitaki kuelewa mazungumzo ya Zitto na Lowassa yalikuwaje kwa kuwa hata mimi yamenistua saana.. Pia wengine wanasema kwamba Zitto ana Political idol wake Mzee Salmin lakini tukumbuke hata Mbowe idol wake ni Mzee Nyerere kwa hiyo kusema kuwa kila aliye CCM ni mdhambi si sahihi na ni batili...

Hoja yangu hapa itajikita kuhusu Mwanahalisi ambayo imepania kumpoteza Zitto kabisa lakini ikumbuke kuwa Zitto katoa mchango mkubwa saana kuikuza CHADEMA apewe nafasi ili ajirekebishe kwa kuwa bado mdogo na ndio kwanza anaanza kuijua siasa ya Tanzania.. Pili naomba kutoa hoja ya CHADEMA kuamua moja tuuu...Zitto na Mbowe wote watolewe madaraka ili kila mtu akae pembeni na CHADEMA iendelee kukuzwa na wengine... Hawa ndio chanzo cha majungu yoote.. Sio kweli kwamba CHADEMA bila ZITTO na MBOWE si kitu??? Watu pale CHADEMA ni wengi na ni wakati wa kuwapa nafasi hasa Dr. Slaa ambaye mimi ni Political idol wangu apewe uenyekiti na wengine majukumu mengine... Kuna wakati kama chama tuamue mambo kwa msingi madhubuti vinginevyo hali itakuwa mbaya saana hasa ukiona gazeti kama MwanaHALISI na Tanzania daima zikimwandama mwanachama mmoja wakati woote wakati tunajua fika haya ni magazeti ya vigogo wa CHADEMA... Niliwahi kusoma Tanzania Daima likiituhumu kimajungu Mwananchi kuwa linamkuza Zitto kisiasa... Jambo ambalo mimi nina mashaka nalo kabisa!!! ::::: DIVIDE AND RULE TECHNIC!!???

Pili, tuache kupotosha UMMA kwa mambo tusiyoyajua kabisaa... Kusema kama Zitto ni mbaya au mzuri haijalishi lakini ifike wakati tukubaliane kwa Zitto ni mtata na hatabiriki toka akiwa chuoni pale Dar.. Huwa anapenda sana kujiridhisha kwa anachofikiri ili mradi anaona hivyo ndivyo sawa... Lakini ni mwepesi wa kukubali baya kama amefanya.. WanaJF nyinyi ni mashahidi kuwa Zitto amewahi kukiri hapa kuwa uamuzi wa kutokuingia bungeni hakuwa sahiihi na alikosea saana... Ameapa kusikia ya walio wengi (wananchi) ili afike safari yake ya kisiasa katika hatua bora na thabiti...

Nukuu kuidhihisha hoja hapo juu:
Nobody grows old merely by living a number of years. We grow old by deserting our ideals. Years may wrinkle the skin, but to give up enthusiasm wrinkles the soul. ~~~Samuel Ullman

A man's age is something impressive, it sums up his life: maturity reached slowly and against many obstacles, illnesses cured, griefs and despairs overcome, and unconscious risks taken; maturity formed through so many desires, hopes, regrets, forgotten things, loves. A man's age represents a fine cargo of experiences and memories. ~~~Antoine de Saint-Exupéry, Wartime Writings 1939-1944,


Tafakari chukua hatua...!!!
 

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
195
Eliesikia...nimekusoma. Namini unahoja unataka kuiweka hapa mbele ya JF lakini ulivyoileta hii haina mashiko...umesummarise yoote yalisyokwisha zingumzwa na kuandikwa kuhusu huyu mwananchi Zitto na hivyo haivutii.....

Tunamsubiria yeyebinafsi aje hapa ukumbini au via KITABU USO- Facebook maana hakuna siri...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom