Magazeti ya Leo na Kutekwa, kushambuliwa kwa Dk Ulimboka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti ya Leo na Kutekwa, kushambuliwa kwa Dk Ulimboka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Jun 28, 2012.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  gazeti la mwananchi
   
 2. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Gazeti la Tanzania Daima
   
 3. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Gazeti la Nipashe:
  Huu ni unyama
  Na Mwandishi wetu
  28th June 2012

  [​IMG] Dk. Ulimboka atekwa apigwa nusu kufa
  [​IMG] Muhimbili, KCMC Madaktari wataharuki  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka, akiwa ametapakaa damu baada ya kutekwa na kupigwa vibaya na watu wasiojulikana akiwa katika gari akipelekwa Hospitali ya Muhimbili.


  Mgomo uliotangazwa na madaktari katika hospitali zote za serikali nchini umeingia katika hatua nyingine, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, kutekwa na watu wasiojulikana ambao wamempiga na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili, ikiwa ni pamoja na kumng'oa meno na kucha.

  Tukio hilo la kinyama ambalo limepokewa kwa hisia tofauti na madaktari na wananchi, limetokea majira ya saa 6:00 usiku wa kumkia jana, ambao watu watatu wanaodaiwa kuwa na silaha aina ya Short gun na bastola walimteka eneo la barabara ya Tunisia, Kinondoni.

  Kufuatia tukio hilo, utoaji wa huduma katika hospitali za serikali za jiji la Dar es Salaam za Muhimbili, Amana, Temeke na Mwananyamala zimezidi kudorora na kuathiri wagonjwa kufuatia madaktari wachache waliokuwa wakiendelea na kazi kukimbilia Taasisi ya Mifupa (MOI) kumuona mwenzao aliyejeruhiwa.

  Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitage, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za (MOI) jana, alisema Dk. Ulimboka alitekwa na watu hao mmoja akiwa amevalia nguo za kijeshi ambao walimchukua na kumpeleka kusikojulikana na kisha kuanza kumpa kipigo.

  Alisema mazingira ya kutekwa Dk. Ulimboka yana utata kwani alipigiwa simu na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Abeid ambaye inadaiwa alijitambulisha kuwa ametoka Ikulu na kumweleza kuwa ana maelezo ya msimamo wa Serikali kuhusu mgomo wa madaktari.

  Dk. Chitage alisema kwa kuwa ilikuwa usiku, Dk.Ulimboka alimtafuta daktari mwenzake Dk. Deogratius Michael ambaye alimsindikiza hadi eneo la barabara ya Tunisia Kinondoni ambako walikubaliana kukutana na mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ametoka Ikulu.

  Alisema Dk. Ulimboka na Dk. Deo hawakumtilia shaka mtu huyo aliyempigia simu kwa sababu tangu mgomo uanze, amekuwa akiwapa taarifa mbalimbali ya kinachoendelea hata baadhi ya vikao vya serikali na madaktari alikuwemo.

  Aliongeza kuwa baada ya kufika eneo hilo walimkuta mtu huyo (Abeid) akiwa peke yake na ghafla walijitokeza watu wengine watatu kati yao wawili walikuwa na bastola na mmoja na Shortgun ambao walimzonga na kumteka na kumpakiza katika gari yenye namba za IT (International Transfer).

  Watu hao walimchukua Dk. Ulimboka na kumpeka kusikojulikana huku wakimuacha Dk. Deo eneo la tukio.

  Alisema baada ya tukio hilo usiku huo Dk. Deo alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Oysterbay ambako hakupata ushirikiano wowote na kuamua kwenda kuripoti tena kituo cha kati cha polisi ambako alielezwa na askari waliokuwa zamu kwamba atapata taarifa za tukio hilo asubuhi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo-Bisimba, alisema alipigiwa simu saa 9:00 usiku na mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) aliyempa taarifa kuwa Dk. Ulimboka ametekwa na watu wasiojulikana.

  Alisema baada ya kupata taarifa hizo, juhudi za kumtafuta zilianza usiku huo na ilipofika saa 12:30 asubuhi alipata taarifa kutoka kituo cha polisi Bunju kwamba wakamchukue Dk. Ulimboka na kwamba hali yake ni mbaya sana.

  Kijo-Bisimba alisema baada ya kufika kituoni hapo alipewa maelezo na askari walikuwepo kwamba Dk. Ulimboka ameokotwa na msamaria mwema maeneo ya Mabwepande akiwa katika hali mbaya huku ametapakaa damu.

  Alisema baada ya kuelezwa hivyo alipiga simu Muhimbili kuomba gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) lakini hakupata ushirikiano wowote na hivyo kuamua kumchukua katika gari yao aina ya Harrier yenye namba T 319 BKR na kuanza safari ya kumpeleka MOI.

  Mkurugenzi huyo alisema wakiwa njiani kwenda MOI, walikutana na vikwazo vingi ikiwemo foleni na pia gari moja isiyojulikana ambayo ilikuwa inawazuia kwa mbele ili kuwachelewesha kufika hospitalini.

  Alisema kutokana na vikwazo hivyo waliomba msaada wa gari la wagonjwa la Shirika la Afya la AAR lenye namba za usajiri T 151 AVD ambayo ilimchukua Dk. Ulimboka katika eneo la TMJ Mikocheni na kumpeleka MOI.

  Dk. Ulimboka alifikishwa MOI na kupokelewa saa 4:48 asubuhi ambapo baada ya kumshusha katika gari hiyo baadhi ya madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine waliangua vilio baada ya kumuona katika hali mbaya huku waandishi wa habari wakizuiwa kumpiga picha.

  Baada ya kushushwa alipelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha huduma ya dharura na kuanza kupatiwa huduma ya kwanza na baadaye kupelekwa kwenye kipimo cha CT-Scan.

  Wakati Dk.Ulimboka akiendelea kupatiwa matibabu MOI, kulizuka tafrani baada ya mtu mmoja aliyesadikiwa kuwa Ofisa wa Usalama wa Taifa alisikika akiongea kwa simu chooni akitoa taarifa kwa watu wasiojulikana kwamba ‘huyu mtu hajafa' akimaanisha Dk.Ulimboka.

  Mtu mmoja aliyekuwepo karibu na eneo la choo baada ya kumsikia alitoa taarifa kwa madaktari ambao walikwenda kwenye choo hicho na kumtoa nje na kuanza kumpiga kabla ya kuokolewa na askari waliokuwepo eneo hilo na kumkimbiza Muhimbili kitengo cha dharura kupata matibabu kutokana na kujeruhiwa.

  Muda mfupi baada ya mtu huyo ambaye anadaiwa kuwa ni Ofisa Usalama huyo kupigwa, askari watatu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika MOI na kiongozi wao mwenye namba E 8342 alianza kutoa tangazo kwa kwamba wamekuja kufuata redio call iliyoangushwa na mwenzao.

  "Tumekuja kufuata redio call yetu iliyodondoshwa na staff mwenzetu mliyempiga aliyechukua aturudishie," alisikika akisema kiongozi wa askari hao.

  Hata hivyo, alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa madaktari ambao walianza kumzonga na kutishia kuwapiga askari hao watatu wakihoji ni kwa nini wamekwenda na silaha hospitalini hapo wakati hairuhusiwi.

  TAMKO MAT NA JUMUIYA YA MADAKTARI

  Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi, akizungumza na waandishi wa habari alisema chama hicho kinalaani kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka akieleza tukio hilo kuwa ni la kinyama, linafadhaisha na linavunja mioyo ya wafanyakazi wa sekta ya afya.

  Dk. Mkopi aliunganisha tukio hilo na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyoitoa Bungeni jana asubuhi ya kwamba ‘serikali itachukua hatua yoyote na liwalo na liwe' katika mgomo wa madaktari.

  Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Edwin Chitage, alisema tukio hilo limewafanya madaktari kuwa imara zaidi katika kupigania haki zao na kwamba watasimama kwa gharama yoyote hata ikibidi kutoa uhai wao.

  Dk. Chitage alisema jumuiya hiyo inalaani juhudi zilizofanywa na watu waliokuwa wakizuia gari lililomchukua Dk. Ulimboka ili achelewe kufika hospitalini.

  TAMKO LA SHIRIKA LA SIKIKA, LHRC

  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utetezi wa sera na utawala bora katika sekta ya afya (Sikika), Irenei Kiria, alisema tukio la kupigwa Dk. Ulimboka linadhihirisha kauli ya Waziri Mkuu, Pinda aliyoitoa bungeni.

  Kiria alisema pamoja na kauli hiyo ya Pinda ambaye ni kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni, lakini cha kusikitisha Naibu Spika, Job Ndugai hakuchukua hatua zozote kumkanya.

  Naye Mkurugenzi wa LHRC, Kijo-Bisimba, alisema kutokana na tukio hilo serikali ifanye uchunguzi wa kimataifa kuhusu mazingira ya tukio hilo ili kujisafisha kufuatia madai kuwa imehusika moja kwa moja.

  MBEYA WALAANI


  Madaktari waliogoma katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wamechukizwa na kitendo cha kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Dk. Ulimboka hali iliyofanya wakusanyike na kutoa msimamo wa kuendelea na mgomo.

  Wakizungumza na NIPASHE jana walisema kuwa kitendo alichofanyiwa kiongozi wao ni sawa na kuweka mafuta ya taa kwenye utambi unaowaka ili uendelee kuwaka zaidi, hivyo wako tayari kwa lolote.

  Aidha madaktari hao wameitaka Serikali kutoa tamko kuhusiana na kitendo hicho na kuhakikisha wale waliofanya ukatili huo wanachukuliwa hatua za kisheria.

  Kufutia tukio hilo, madaktari katika hospitali hiyo walionekana wakiwa wamekusanyika kwa pamoja nje na kujadili mkasa uliomkuta kiongozi wao, huku wagonjwa waliolazwa wakiendelea kusubiri huduma mawodini.

  PINDA: LIWALO NA LIWE

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jana bungeni alisema kwamba serikali itatoa tamko la hatua itakazochukua kuhusiana na mgomo wa madaktari nchini na litakalokuwa na liwe.

  Pinda akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi, aliyesema pamoja na jitihada za serikali katika kutatua madai ya madaktari wameendelea kugoma na kuhoji serikali inachukua hatua gani ingawa jambo hilo liko mahakama kuu, divisheni ya kazi.

  Akitoa maelezo, Pinda alisema baada ya kutoridhiana katika baadhi ya mambo na madaktari katika majadiliano yao, walikwenda katika Tume ya Usuluhishi (CMA).

  Alisema CMA iliamua jambo hilo liende Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi: "kwa hiyo tumekwenda huko na kwamba Juni 22 mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa agizo madaktari wasitishe mgomo huo na waende katika vyombo vya habari na kuelezea kuhusiana na hatua hiyo."

  Hata hivyo, Pinda alisema juzi walirudi tena Mahakama Kuu ambapo walitaka amri iliyotolewa Juni 22 mwaka huu, itekelezwe na watangaze katika vyombo vya habari.

  Pinda alisema wameona aliarifu Bunge hilo jana kuhusiana na hatua walizoamua kuchukua, "waswahili wanasema "liwalo na liwe."

  Pamoja na maelezo ya Pinda, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, akitumia kanuni ya 68(8), na kutoa taarifa kuwa serikali imekishitaki Chama cha Madaktari Nchini (MAT) wakati waliotoa tamko la mgomo ni Jumuiya ya Madaktari Nchini.

  Mnyika alishauri ni vyema Bunge likapokea taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii ya Bunge, ambayo ilikwenda kuchunguza jambo hilo na kuzifanyia kazi taarifa zilizokamilika.

  Kwa upande wake Mbunge wa Nzega, (CCM), Dk. Khamis Kigwangalah, alisema amesikitishwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa ndani ya Bunge kuhusiana na mgomo huo.

  Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema mtu aliyepigwa Muhimbili ni ofisa wa polisi ASP Mokili wa kituo cha Salender Bridge, ambaye alikwenda hospitalini hapo kuonana na madaktari kuhusiana na kutekwa kwa Dk. Ulimboka na kwamba alikuwa ametumwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Suleiman Kova.

  Alikanusha madai kwamba ofisa huyo alipigwa baada ya kusikika akiongea na simu chooni badala yake alisema alitekwa na kupigwa baada ya kuonana na madaktari.
  Wakati huo huo, Kova ametangaza kuunda timu ya kuchunguza tukio hilo.
  Alisema jeshi lake limeunda jopo la wapelelezi wa fani mbalimbali chini ya Mkuu wa Upelelezi kanda maalumu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi, kushughulikia tukio hilo.

  KCMC WASITISHA HUDUMA

  Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, wametangaza kusitisha kutoa huduma kufuatia tukio la kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kiongozi wao Dk.Ulimboka.

  Msimamo huo wameutoa baada ya kukutana kwenye kikao cha dharura jana saa 4 asubuhi, kilichowashirikisha madaktari 100 .

  Baada ya kutoa tamko hilo madaktari hao walianza kutembelea idara, wodi na kliniki za hospitali hiyo na kuwaondoa madaktari waliokuwa wakiendelea na kazi katika hospitali hiyo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk. Moshi Ntabaye, hakuweza kupatikana kuelezea hali hiyo kwa kuwa alikuwa hoteli ya Salsalnero kuhudhuria mkutano wa kimataifa.

  Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Samson Fridolin, Raphael Kibiriti, Ninaeli Masaki na Gwamaka Alipipi, Dar; Emmanuel Lengwa; Mbeya, Sharon Sauwa na Gaudensia Mngumi; Dodoma na Salome Kitomari; Moshi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 4. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante Katulanda ntarudi baadaye ndefu sana, mho'la ibhu'hongwa?
   
Loading...