Magazeti ya Kenya na dhihaka kwa Rais wetu

Mkuu najua kwamba Nation Media Group haimilikiwi na Wakenya nadhani inamilikiwa na Aga Khan kama sikosei na sikuwa na nia ya kupotosha. Ila tu nikuambie kwamba Kenya hakuna uhuru wa Habari kama hapa kwetu. Soma tena hiyo makala uone, mbona hawajasema kuhusu Kibaki alivyong'ang'ania madaraka na kupora ushindi wa Odinga na kuapishwa wakati bendera imeshushwa!!

Mkuu, Nation Media inamilikiwa na Aga Khan lakini Wakikuyu wana stake kubwa sana katika hiyo Media House; in fact, hawa ndio wanaloliendesha, na mara zote wameitumia kuyumbisha siasa za Kenya.
Inaelekea hamuifahamu Kenya vizuri, fuatilia hata Wakenya wanaofanyia Mwananchi hapa kwetu au hata Daily Monitor kule UG, utakuta ni Wakikuyu na mara zote wana agenda zao wanazosimia.
 
acha mambo ya ajabu wewe! umeandika ujumbe huu kwenye giza halafu unaleta uzandiki!
 
Sasa, Citizen waandike nini kuhusu rais wa Kenya?? Uchumi wao unaelekea 'Uchumi kati' Sisi tunahangaika na kina Rostam, Chenge na EL....!! Wacha wamwandike maana nadhani ulimwengu haujui kuhusu huyu mswahili; Nchi imemshinda kabisaa alafu yeye wala hajali!!!!!
 
Tusikatae ukweli, Mkuu anasafiri nje mno, Anakumbatia mafisadi hadi:-
Alishawahi kusema hawa ni watu hatari wanaweza kutikisa nchi,
amebaki kuwaomba walipe hiyo hela who knows how much was paid back,
baada ya kuishiwa sera amewaomba wavue magamba na bado wamekataa mbali zaidi wanaiita serikali yake legelege haiwezi kufanya maamuzi, ataachia madaraka ktk miaka 4 kwa kifupi tukiyakataa haya regardless yamesemwa na nani tutaonekana kama yeye.

Uzalendo kukumbatia mambo haya? Itakuwa ni kumpotosha rais wetu!!!!
 
Hata mimi haya maneno yamenikera, ni sawa na kumsikia jirani anajadili mapungufu ya ndoa yako wakati hata ya kwake inaning'inia

Wee PJ, unasema abadilike ili aone kama watamchafua?, kumbe ni wanamchafua tuu?, ukiimaanisha ni msafi ila anachafuliwa?!. The EA ni gazeti la 'A Spade is a Spade!'.

Mbona gazeti la Mwananchi ama the Citizen hawaandiki kuhusu viongozi wa Kenya na maluweluwe yao kwa njia ya dhihaka kama alivyoandika Obbo?

magazeti yetu sio lazima yaandika habari kwa visasi, kama yanajua kuna mapungufu ya raisi wa kenya na wao wanaweza kuandika laki je, kwa hali waliayonayo watanzania kwa sasa wanatakujua mwaikibaki anawafanyia nini wakenya?
huu ni msaada tutani mwandishi wa hii habari katufanyia kama kuna mtu ananunu basi amnunie kikwete maana ndivyo halivyo na huu ni ukweli dhairi.
huyu mwandishi anastahiri tuzo kwa kumyumbulisha kikwete kwa undani kwa maneno machache safi sana

Watanzania tuna malivyo na neno utaifa eti ikifika wakati wa kutete nchi tuwe wote wakati wa kuchafua kila siku ni wao viongozi ndio wanao chafua nchi kisha wanataka utaifa kutete uozo wao.
mbona media za kimataifa kama kuna tatizo nchini kwao wanasema tena kwa nguvu
na bado subiria al jezeera wakija hapo nairobi
 
Huu ni ujinga wa majirani zetu, wanadhani kwa kumtandika na mjungu ndio watamdhoofishia nuru jk, sidhani majungu ndio njia sahihi ya kum address jk, all in all majungu humjenga anaepigwa jungu. Daima naamini ukweli hujitetea wenyewe hautaji defence.
 
hoja ni je wameandika uongo hapo kuhusu kikwete?
hayo mambo ya hositori na stori hayana mpango tuwekana sawa wameandika uongo?

Mkuu, Nation Media inamilikiwa na Aga Khan lakini Wakikuyu wana stake kubwa sana katika hiyo Media House; in fact, hawa ndio wanaloliendesha, na mara zote wameitumia kuyumbisha siasa za Kenya.
Inaelekea hamuifahamu Kenya vizuri, fuatilia hata Wakenya wanaofanyia Mwananchi hapa kwetu au hata Daily Monitor kule UG, utakuta ni Wakikuyu na mara zote wana agenda zao wanazosimia.
 
Huu ni ujinga wa majirani zetu, wanadhani kwa kumtandika na mjungu ndio watamdhoofishia nuru jk, sidhani majungu ndio njia sahihi ya kum address jk, all in all majungu humjenga anaepigwa jungu. Daima naamini ukweli hujitetea wenyewe hautaji defence.

majungu ni yepi hapo
 
sasa dhihaka iko wapi? leo hii hatuna umeme hatuna chakula cha kutosha wewe unalalamika wakenya wanamdhihaki rais wetu......acha mambo ya kis..ge
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Binafsi sidhani kama hizo ni dhihaka, kwani sifa alizosifiwa nazo zote ni za kweli, nadhani akijua hata waandishi wa kenya wanafahamu kuwa yeye ni mdhaifu kwa madhaifu hayo yaliyotajwa atajirekebisha kwa yale ambayo anauwezo wa kuyarekebisha.
MI SINA TATIZO WAACHENI WAKENYA WATUSAIDIE KUUWEKWA UKWELI HADHARANI, ILA RAI YANGU WAKIANDIKA MAMBO YASIYO NA UKWELI BASI TU-ACT UPON THEM.
 
Wenye akili fupi wanaotawaliwa na fikra na itikadi zisizo huru watashangilia kitendo hiki na hawa ni wale wenye fikra fupi wasiotaka kuona mbali, wenye uwezo wa kuona mbali wataishia kusikitika hata kama anayosemwa nayo kikwete ni ya kweli ila je yanasemwa kwa lengo gani? Baba yako hata kama kakunyima hela ya mtaji wa biashara haimvui thamani ya kuwa baba na hata kama ikitokea anasemwa kwa mabaya hata kama ni kweli inapaswa uzalendo ukuguse, na haya ndo mapenzi ya kweli kwa taifa lako. Kijana mwema ni yule ambaye hujenga nyumba kwa mikono na aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Nakuunga mkono Mkuu..............Ni wivu tu walionao Wakenya kwa TZ
 
Wenye akili fupi wanaotawaliwa na fikra na itikadi zisizo huru watashangilia kitendo hiki na hawa ni wale wenye fikra fupi wasiotaka kuona mbali, wenye uwezo wa kuona mbali wataishia kusikitika hata kama anayosemwa nayo kikwete ni ya kweli ila je yanasemwa kwa lengo gani?

Baba yako hata kama kakunyima hela ya mtaji wa biashara haimvui thamani ya kuwa baba na hata kama ikitokea anasemwa kwa mabaya hata kama ni kweli inapaswa uzalendo ukuguse, na haya ndo mapenzi ya kweli kwa taifa lako. Kijana mwema ni yule ambaye hujenga nyumba kwa mikono na aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.


BABA yupi huyo. Aliyebaka mama yako na kupatikana katika laana! Acha hizo. Hakusitahili kuwepo hapo bila kubaka demokrasia. NEC na wenzake!! KIlio Kilio x2 jamani! Kilio kilio xjamani.......
 
WanaJF nilikuwa napitia gazeti la The East African lililotoka Jumamosi tarehe 16.07.2011 nikakutana na kichwa cha habari kisemacho A record Four East African Presidents Set to Retire. Mwandishi amewaongelea Marais wa EA kwa upande wa Rais wetu nikaona sentensi zifuatazo;

"Tanzania's Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."

Haya maneno hayakunifurahisha kwa kuwa magazeti ya Kenya yamekuwa mstari wa mbele kudhihaki viongozi wetu wakati magazeti yetu hayajawahi kuwadhihaki viongozi wa Kenya. NAkumbuka kuna wakati Gazeti moja kama si hili la East African lilichora kikatuni kikionyesha kiongozi wetu akilamba viatu vya wazungu. Nadhani ni wakati muafaka dhihaka hizi zikomeshwe.

Source:The East African:  - News |A record four East African presidents set to retire

YES ..... ninalo hili gazeti nalisoma

duh .... hii ni kweli wakenya wanasema kwamba watanzania wanakili na ni watu wazuri sana lakini watanzania wamekosa bahati ya kuwa na aggressive leaders
 
Nakumbuka Prof Lipumba aliwahikusema kwenye kampeni kuwa JK hana sera ila wanadai( CCM) anapendeza jukwani. Ndicho walichomchagulia, naye alisema anataka kukumbukwa kwa kutoa toka sehemu moja hadi nyingine. Hakufafanua kumbe ni kutoka kwenye Umeme kwenda GIZANI.

Siamini, Utadhani nchi imetekwa Umeme masaa 20 hakuna!!!

kweli tumepatikana na hatuna jinsi wataendelea kuahidi mpaka watoke madarakani.

Waache Wakenya na wengine wandike watakavyo na labda ataacha kuzurura akijua hata nje ya mipaka wamemjua si lolote ni Mr. Promise tu.
 
Pongezi nyingi kwa huyo Mhariri ila kasahau kimoja alipata PhD kwa umahiri wa kucheza KIDUKU (Kiduku Phd Holder)
 
Hivi dhihaka ni nini?! Mkisifiwa na wageni mnajitapa, kumbe mnataka wakiona madudu yenu wasiyaseme?! Mimi wameniudhi kwa kuandika kwa ufupi mno, walitakiwa waingie deep!!
 
Back
Top Bottom