Magazeti ya Kenya na dhihaka kwa Rais wetu

WanaJF nilikuwa napitia gazeti la The East African lililotoka Jumamosi tarehe 16.07.2011 nikakutana na kichwa cha habari kisemacho A record Four East African Presidents Set to Retire. Mwandishi amewaongelea Marais wa EA kwa upande wa Rais wetu nikaona sentensi zifuatazo;

"Tanzania's Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."

Haya maneno hayakunifurahisha kwa kuwa magazeti ya Kenya yamekuwa mstari wa mbele kudhihaki viongozi wetu wakati magazeti yetu hayajawahi kuwadhihaki viongozi wa Kenya. NAkumbuka kuna wakati Gazeti moja kama si hili la East African lilichora kikatuni kikionyesha kiongozi wetu akilamba viatu vya wazungu. Nadhani ni wakati muafaka dhihaka hizi zikomeshwe.

Source:The East African:  - News |A record four East African presidents set to retire

Jiulize swali zuri tu, Yaliyosemwa ni kweli? This is an important question before you ground your complaint!!! If there is truth and truth only, then keep quiet. Tell your beloved president to make reformation/rectify the situation. Basi.
 
Kwani wamekosea nini? wameongopa au kukuza jambo hapo? Ktk profession ya uandishi na mambo ya habari mwandishi anatakiwa kuwa ukweli na facts za kutetea ukweli huo. Nashangaa, na sijui wamekudhihaki wapi.

Anyway pole sana kwa machungu yako!
 
Mkuu unatakiwa uelewe kwamba gazeti la East African pamoja na kuminilikiwa na nation media group ambayo makao makuu yake ni Nairobi si mali ya wakenya au serikali ya Kenya kama unavyotaka kupotosha, na upotoshaji huu unaufanya makusudi ili kuneutralize hoja. Gazeti hili ndiyo the only one linalocover habari za east Africa almost equally kiusawa wa no. of pages. Ni gazeti linalokubalika na kuaminika, it is "the economist" of East Africa.

Tukija kwenye hoja yako kwa kumbukumbu yangu maraisi wote wa East Africa wamekuwa wakichambuliwa vilivyo ndani ya gazeti hili, ishu kama ya mke wa Kibaki waliiandika ina way mama Salma angeandikwa vile na gazeti kama majira au "la kenya" (mwananchi) basi lingefungiwa. Na kama alivyosema Pasco hapo juu, these guys they just call a spade a spade. Ni kipi hapo unachokiona si kweli kuhusu JK?

Mkuu najua kwamba Nation Media Group haimilikiwi na Wakenya nadhani inamilikiwa na Aga Khan kama sikosei na sikuwa na nia ya kupotosha. Ila tu nikuambie kwamba Kenya hakuna uhuru wa Habari kama hapa kwetu. Soma tena hiyo makala uone, mbona hawajasema kuhusu Kibaki alivyong'ang'ania madaraka na kupora ushindi wa Odinga na kuapishwa wakati bendera imeshushwa!!

Kuhusu mke wa Kibaki siwezi nikasema mengi lakini nakumbuka kwamba alimchapa kibao mwandishi wa habari ya hayo magezeti ten news room na sijui nini kimetokea hadi leo!!
 
Mbona gazeti la Mwananchi ama the Citizen hawaandiki kuhusu viongozi wa Kenya na maluweluwe yao kwa njia ya dhihaka kama alivyoandika Obbo?
Kimbunga unaweza kuwa nazi mkubwa wa JK lakini ukweli uko pale pale hakuna nchi katika eac zaidi ya Kenya ambayo ina media critical kwa viongozi nchi...unakumbuka mke wa Kibaka alishampiga mhariri gazeti moja kwa kumuandika vibaya Kibaki. Kuna mtanzania anaitwa Gado ana vipindi vya vibonzo specifically vinawalenga kina Kibaki, Raila na viongozi wengine wa juu.
 
Mkuu unatakiwa uelewe kwamba gazeti la East African pamoja na kuminilikiwa na nation media group ambayo makao makuu yake ni Nairobi si mali ya wakenya au serikali ya Kenya kama unavyotaka kupotosha, na upotoshaji huu unaufanya makusudi ili kuneutralize hoja. Gazeti hili ndiyo the only one linalocover habari za east Africa almost equally kiusawa wa no. of pages. Ni gazeti linalokubalika na kuaminika, it is "the economist" of East Africa.

Tukija kwenye hoja yako kwa kumbukumbu yangu maraisi wote wa East Africa wamekuwa wakichambuliwa vilivyo ndani ya gazeti hili, ishu kama ya mke wa Kibaki waliiandika ina way mama Salma angeandikwa vile na gazeti kama majira au "la kenya" (mwananchi) basi lingefungiwa. Na kama alivyosema Pasco hapo juu, these guys they just call a spade a spade. Ni kipi hapo unachokiona si kweli kuhusu JK?
Mkuu Nyambala thanks a lot kwa hapo nilipobold, nilitaka nirudi baadaye kupaelezea hapo ili records zikae vizuri nashukuru umeliona hilo pia.

Pamoja na kwamba gazeti la EA linamilikiwa na National Media nadhani ni makosa kuliita ni la Kenya otherwise unaweza usiwe fair kulingana na namna walivyo objective kwenye kazi.Natamani tungekuwa na magazeti mengi kama haya huenda yangesaidia sana.

Kuna jamaa katoa mfano wa baba na mwana kumtetea Kikwete, huo mfano haufit kabisa hapa. Mfano huo unanikumbusha Madam speaker wetu aliposema PM hawezi kudanganyana natamani ningekuwa karibu nimuulize Pinda si mwanadamu?
 
Wanasema mjumbe hauwawi, wewe ndo mchawi wa Kikwete sasa wewe ndo umemdhihaki kwani watanzania wengi hawasomi magazeti hayo hapo kilichokuwa kifanyike ni funika kombe mwanaharamu apite sasa wewe ndo unamtukana rais wetu mpendwa ambaye watanzania wanamtukuza mh.dr wa ma.dr wote kiongozi wa kwanza msomi mtanzania nyerere aliishia MA, mkapa alikuwa mseja , mwinyi stashahada sasa tunaye dr. hollible,mpenda nini wamesema anapenda anasa , eti wamesema mwoga wa maamuzi,ni shujaa wa kubembea hali wananchi wanateseka, ni shujaa maana amemtajirisha kijana wake, ni mjasilia mali kule serengeti
 
Tumekubali wenyewe kuwa na uongozi unaofanya mambo yanayotoa nafasi kwa majirani kutukebehi. Hii ni aibu kubwa, tunapaswa kulikataa hili kwa kutorubuniwa kuweka madarakani viongozi bila kufikiri kwa kina.
 
"Tanzania's Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."
Hakuna jipya, magazeti ya TZ yameandika mambo hayo hayo kuhusu JK. In fact hizo sentensi zimebeba ukweli mtupu kama watanzania waelewa wanavyofahamu. Hebu nitajjie raisi mwingine ktk east na central Africa anayependa matanuzi na safari zisizokuwa na tija kama JK! kama wewe ni mfuatiliaji, unalinganishaje idadi ya safari za raisi wetu na za maraisi wenzake katika nchi zinzotuzunguka?

wauza unga anawafahamu, mafisadi anawafahamu, wala rushwa anawafahamu wazinzi anawafahamu (obviously waarabu wa pemba alama yao kilemba, lazima wajuane tu).

Yote yaliyozungumza ni ukweli. Waandishi wa TZ wataandika nini kuhusu siasa za kenya? Kama unafahamu kitu ambacho waandishi wetu wanaweza kuandika kuhusu siasa za kenya, chenye faida kwa wasomaji wa TZ na EA kwa ujumla, watonye waandike! Wataandika!

Ukweli huwa unauma! pole!
 
Absolutely correct walichokiandika ni ukweli, ukweli mtupu na hawa jamaa sio wakenya kama mtoa mada unavyotaka kupotosha. Gazeti limeajiri Waganda, Watanzania na Wakenya mle. Makao kuwa nairobi si hoja.... ndio maana hata jina lenyewe linajieleza wakuu.
 
Mkuu Nyambala thanks a lot kwa hapo nilipobold, nilitaka nirudi baadaye kupaelezea hapo ili records zikae vizuri nashukuru umeliona hilo pia.Pamoja na kwamba gazeti la EA linamilikiwa na National Media nadhani ni makosa kuliita ni la Kenya otherwise unaweza usiwe fair kulingana na namna walivyo objective kwenye kazi.Natamani tungekuwa na magazeti mengi kama haya huenda yangesaidia sana.

Mkuu hili ni gazeti la Kenya kwa kuwa limeandikishwa Kenya kama ilivyo kwa the Citizen na Mwananchi ni magazeti ya Tanzania na Monitor na Bhukede ni magazeti ya Uganda!!!
 
Absolutely correct walichokiandika ni ukweli, ukweli mtupu na hawa jamaa sio wakenya kama mtoa mada unavyotaka kupotosha. Gazeti limeajiri Waganda, Watanzania na Wakenya mle. Makao kuwa nairobi si hoja.... ndio maana hata jina lenyewe linajieleza wakuu.

Mkuu kwa kuajiri waganda, wakenya na watz kuna maana gazeti si la Kenya? Ukenya wake unatokana na lilikoandikishwa!! Kama jina ni hoja basi News of the World lingekuwa si la Uingereza bali la Dunia!!
 
Hakuna jipya, magazeti ya TZ yameandika mambo hayo hayo kuhusu JK. In fact hizo sentensi zimebeba ukweli mtupu kama watanzania waelewa wanavyofahamu. Hebu nitajjie raisi mwingine ktk east na central Africa anayependa matanuzi na safari zisizokuwa na tija kama JK! kama wewe ni mfuatiliaji, unalinganishaje idadi ya safari za raisi wetu na za maraisi wenzake katika nchi zinzotuzunguka?

wauza unga anawafahamu, mafisadi anawafahamu, wala rushwa anawafahamu wazinzi anawafahamu (obviously waarabu wa pemba alama yao kilemba, lazima wajuane tu).

Yote yaliyozungumza ni ukweli. Waandishi wa TZ wataandika nini kuhusu siasa za kenya? Kama unafahamu kitu ambacho waandishi wetu wanaweza kuandika kuhusu siasa za kenya, chenye faida kwa wasomaji wa TZ na EA kwa ujumla, watonye waandike! Wataandika!

Ukweli huwa unauma! pole!
 
Mkuu maneno haya yangesemwa nyumbani ingeonekana ni fitna. So good yamesemwa nje ya nchi, lakini nyumbani sio siri.
 
wauza unga anawafahamu, mafisadi anawafahamu, wala rushwa anawafahamu wazinzi anawafahamu (obviously waarabu wa pemba alama yao kilemba, lazima wajuane tu).

Mkuu hii dhihaka nyingine tena!!
 
Mwandishi ameandika habari sahihi na zenye uhakika! That is professionalizm! Very good.
 
Rais wa nchi hawezi kufananishwa na baba. Baba anaongoza familia kwa mapenzi lakini rais anaongoza kwa sheria. Rais anapaswa kusimamia rasilimali za taifa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na vijavyo. Rais anapokuwa mzembe mzembe lazima asemwe tu.
 
WanaJF nilikuwa napitia gazeti la The East African lililotoka Jumamosi tarehe 16.07.2011 nikakutana na kichwa cha habari kisemacho A record Four East African Presidents Set to Retire. Mwandishi amewaongelea Marais wa EA kwa upande wa Rais wetu nikaona sentensi zifuatazo;

"Tanzania’s Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."

Haya maneno hayakunifurahisha kwa kuwa magazeti ya Kenya yamekuwa mstari wa mbele kudhihaki viongozi wetu wakati magazeti yetu hayajawahi kuwadhihaki viongozi wa Kenya. NAkumbuka kuna wakati Gazeti moja kama si hili la East African lilichora kikatuni kikionyesha kiongozi wetu akilamba viatu vya wazungu. Nadhani ni wakati muafaka dhihaka hizi zikomeshwe.

Source:The East African:  - News |A record four East African presidents set to retire

ukweli unauma..lakini sisi wa-TZ tumejaa dhihaka.
so, tunaishia kuchagua viongozi kwa dhihaka.
viongozi wanaishia kuwa wenye dhihaka.

...so sishangai kama rational thinking people outside the borders wakiwadhihaki viongozi wetu. infact, by extension wanatudhihaki wewe na mimi pia!!

and you know what? we deserve it!!
 
Wako sawa kabisa , mimi nawaunga mkono.
MATENDO HAYO YOTE YALIYOORODHESHWA NI KWELI, HATUWEZI KUMTETEA KISA KAANDIKWA NA GAZETI LA EAST AFRICA.
Kama hataki aandikwe hivyo si abadilike aone kama watamchafua?

siwapendi wakenya lakini vilevile siwezi kumtetea huyu mtu,mwache aandikwe vibaya kwa ujinga wake
 
Back
Top Bottom