Magazeti ya Kenya na dhihaka kwa Rais wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti ya Kenya na dhihaka kwa Rais wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimbunga, Jul 18, 2011.

 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  WanaJF nilikuwa napitia gazeti la The East African lililotoka Jumamosi tarehe 16.07.2011 nikakutana na kichwa cha habari kisemacho A record Four East African Presidents Set to Retire. Mwandishi amewaongelea Marais wa EA kwa upande wa Rais wetu nikaona sentensi zifuatazo;

  "Tanzania's Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."

  Haya maneno hayakunifurahisha kwa kuwa magazeti ya Kenya yamekuwa mstari wa mbele kudhihaki viongozi wetu wakati magazeti yetu hayajawahi kuwadhihaki viongozi wa Kenya. NAkumbuka kuna wakati Gazeti moja kama si hili la East African lilichora kikatuni kikionyesha kiongozi wetu akilamba viatu vya wazungu. Nadhani ni wakati muafaka dhihaka hizi zikomeshwe.

  Source:http://www.theeastafrican.co.ke/news/A+record+four+East+African+presidents+set+to+retire/-/2558/1202538/-/ycjmm3/-/index.html
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wako sawa kabisa , mimi nawaunga mkono.
  MATENDO HAYO YOTE YALIYOORODHESHWA NI KWELI, HATUWEZI KUMTETEA KISA KAANDIKWA NA GAZETI LA EAST AFRICA.
  Kama hataki aandikwe hivyo si abadilike aone kama watamchafua?
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Mimi maneno hayo yamenifurahisha sana, kwani ni ukweli kabisa na hizo ndio sifa alizonazo Kikwete.
   
 4. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Hata mimi haya maneno yamenikera, ni sawa na kumsikia jirani anajadili mapungufu ya ndoa yako wakati hata ya kwake inaning'inia
   
 5. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ukweli unauma daima pole
   
 6. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hawakuchora wakilamba viatu vya wazungu....ila walichora kikatuni waandishi wa Habari wa Tz wakimlamba miguu ya aliyedhaniwa kuwa ni Kikwete...hawajatkana ndo sifa za Rais wetu..na n Uhuru wa kujieleza!n mtazamano wa Mtu!
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  mhariri wa hilo gazeti nampa big up sana. Wako sahii asilimia 1000%
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  acha uzindiki hapa. yamekukera wapi? wako sahihi kabisa raisi wetu amempiku hata mugabe wa zimbabwe kwa safari za nje aliye kaa madarani miaka takribani 30 sasa.
   
 9. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Sasa wasiseme ukweli? Tena hawajasema yote sijui wanamwonea aibu?
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,622
  Trophy Points: 280
  Wee PJ, unasema abadilike ili aone kama watamchafua?, kumbe ni wanamchafua tuu?, ukiimaanisha ni msafi ila anachafuliwa?!. The EA ni gazeti la 'A Spade is a Spade!'.
   
 11. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Udhalilishwaji?

  Kebehi?

  My skin!
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona gazeti la Mwananchi ama the Citizen hawaandiki kuhusu viongozi wa Kenya na maluweluwe yao kwa njia ya dhihaka kama alivyoandika Obbo?
   
 13. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siku zote ukweli unauma!!!!
   
 14. B

  Bobby JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi nahisi tatizo lako hapo ni kwa kuwa ni gazetil la Kenya ,magazeti ya ndani yamemwandika kuliko hivyo kwa kuwa hivyo ndivyo alivyo. Wewe unajuwa na I'm sure mtu yeyote mwenye akili ya wastani anajuwa kwamba rais wetu ni kituko kuliko hayo maneno ya The EA.
   
 15. A

  Akiri JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,453
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  sijaona hata moja ambalo wamemsingizia tena kuna mengine wamesahau kuyaandika naomba email ya huyo mhariri nimtumie mengine ambayo wamesahau kuyaweka ili next week waweke, ila huyo mwandishi kaniudhi kidogo kasahau kabisa kuandika hata hili kwamba ndiye rais pekee wa E.A anayelindwa na maruhani
   
 16. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wenye akili fupi wanaotawaliwa na fikra na itikadi zisizo huru watashangilia kitendo hiki na hawa ni wale wenye fikra fupi wasiotaka kuona mbali, wenye uwezo wa kuona mbali wataishia kusikitika hata kama anayosemwa nayo kikwete ni ya kweli ila je yanasemwa kwa lengo gani?

  Baba yako hata kama kakunyima hela ya mtaji wa biashara haimvui thamani ya kuwa baba na hata kama ikitokea anasemwa kwa mabaya hata kama ni kweli inapaswa uzalendo ukuguse, na haya ndo mapenzi ya kweli kwa taifa lako. Kijana mwema ni yule ambaye hujenga nyumba kwa mikono na aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
   
 17. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Mkuu unasema hayo magazeti hayakukufuraisha kwanini? Kama mtu ambaye umepitia shule unatakiwa kuwa objective ni kitu gani kimeandikwa hapo ulipo site ambacho ni dhihaka? Unajua tofauti ya ukweli na dhihaka?

  Niseme tu hilo gazeti lisingepata hayo yaliyoandikwa kama si raisi wako kuyatengeneza. Again ungekuwa mtu objective kwa kumuuliza raisi wako juu ya yaliondikwa. Vp kuhusu maraisi wengine wameandika nini juu yao? Kumbuka si magazeti yote yanaweza kuandika kama Uhuru au Daily News.
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu unatakiwa uelewe kwamba gazeti la East African pamoja na kuminilikiwa na nation media group ambayo makao makuu yake ni Nairobi si mali ya wakenya au serikali ya Kenya kama unavyotaka kupotosha, na upotoshaji huu unaufanya makusudi ili kuneutralize hoja. Gazeti hili ndiyo the only one linalocover habari za east Africa almost equally kiusawa wa no. of pages. Ni gazeti linalokubalika na kuaminika, it is "the economist" of East Africa.

  Tukija kwenye hoja yako kwa kumbukumbu yangu maraisi wote wa East Africa wamekuwa wakichambuliwa vilivyo ndani ya gazeti hili, ishu kama ya mke wa Kibaki waliiandika ina way mama Salma angeandikwa vile na gazeti kama majira au "la kenya" (mwananchi) basi lingefungiwa. Na kama alivyosema Pasco hapo juu, these guys they just call a spade a spade. Ni kipi hapo unachokiona si kweli kuhusu JK?
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haya maneno kwa kiasi kikubwa yamenifurahisha sana, maana yamemwelelezea Rais wetu "live bila chenga!" Ambacho hakijanifurahisha ni kwamba JK ataondoka madarakani baada ya miaka 4! Muda huo ni mrefu sana kwa maslahi ya nchi yetu, ingekuwa heri aondoke mwezi ujao!
   
 20. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ehehhee ukweli mchungu wauma sana
   
Loading...