Magazeti ya IPP hayawezi kumkosoa Rais Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti ya IPP hayawezi kumkosoa Rais Kikwete?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, Feb 16, 2013.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2013
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,448
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nasoma hukumu ya kesi ya Regnald Mengi dhidi ya Sarah Hermitage iliyosomwa mwishoni mwaka jana kwenye mahakama moja nchini Uingereza. Mengi alishindwa hii kesi na kutakiwa kulipa faini kubwa. Katika kesi hii kuna ushahidi ulitolewa mahakamani kuwa wahariri wa vyombo vya habari vya Regnald Mengi wamepigwa marufuku kuandika habari zinazomkosoa Rais Kikwete.

  Kuna memo moja ililetwa mahakamani kama ushahidi na pia ushahidi wa Erick Kabendera, mwandishi wa zamani wa IPP, kuwa ni marufuku kuandika habari zinazomkosoa Rais Kikwete. Indaiwa kuwa ushahidi wa Erick Kabendera alioutoa mahakamani tayari umehatarisha usalama wake na wa familia yake. Things fall apart in Tanzania: on media manipulation and hypocrisy

  Hii ni sehemu ya hukumu ya mahakama ambapo jaji alizungumzia ushahidi wa kutoandika habari za kumkosoa Rais Kikwete kwenye magazeti vyombo vya habari vya Mengi.

  87. The hollowness of the pretence that the editorial teams at Mr Mengi's newspapers exercise robust independence at all times is illustrated by a memorandum of 16th October 2008 from Mr Kiondo Mshana, Managing Director of the Guardian, to Sakina Datoo, then IPP Print Media Group's Editorial Director. Headed "Publication of stories on the President", and copied to Mr Nguma in his capacity as a director of The Guardian Ltd, the memo read:

  "You will recall my having officially notified you recently that it is absolutely necessary for my advice to be sought before any of The Guardian Limited publications runs controversial or any otherwise sensitive stories on President Jakaya Kikwete.

  I told you that I must actually see the copy in question before it goes to print or, in case circumstances make that impossible, that I be contacted by telephone so that I can advice as appropriate.

  I take this opportunity to state that this remains the Company's official stand and that all editors are obliged to observe it without fail. Doing so has many advantages. Please, ensure no-one defaults on this. Many thanks for your understanding and cooperation."

  88. The next day Mr Mshana was slapped down by Mr Nguma, who wrote:

  "In my view, this is direct interference with editorial independence and I hope that you will not do this again in the future in respect of this or any other case".

  89. Mr Nguma was right: the memo was indeed direct interference with editorial independence. But, Mr Price asked, how did it come about that Mr Mshana was under the impression that a policy of not criticising the President in the Guardian without asking the managing director's permission remained the Company's "official stand" which all editors were "obliged to observe….without fail"?

  Mr Mshana was identified by Mr Kabendera, a young Tanzanian journalist who worked for the Guardian in 2009-10 and gave evidence for the Defendant, as having been present in court during part of the evidence before me. Nevertheless no evidence from Mr Mshana, written or oral, was produced, with the result that he could not be asked for his explanation.

  90. The obvious inference to be drawn from Mr Mshana's memo is that it was a momentary glimpse of the truth. The memo is also consistent with evidence from Mr Kabendera that he and other reporters at the Guardian were told that they must never publish anything negative about President Kikwete."

  Unaweza kusoma hukumu nzima hapa: Mengi v Hermitage [2012] EWHC 3445 (QB) (30 November 2012)
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2013
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,476
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  Interesting. Come to think of it sijaona makala zozote katika magazeti ya IPP media yakihojia uamuzi mbalimbali wa Kikwete na utendaji wake.
   
 3. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2013
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mengi ni mfanya bisahara na ana Uhuru wa kuamua afanyeje biashara zake.

  IPP siyo kampuni ya Umma kama ambavyo mlikuwa mnadai eti ITV iwe Television ya Taifa. Inabidi muanzishe za kwenu siyo rahisi kutegemea chombo cha mtu binafsi au cha serikali kueneza propaganda za chama ambacho hakiko madarakani. Nadhani hii habari haikupaswa kuandikwa humu.

  Mbona kuna memo ya Tanzania Daima na Mwananchi kuhusu kubadilishana front titles za kuipaka serikali na CCM?? Hiyo inafahamika na serikali na CCM wamejipanga wanajua kinachofanyika na wanaokifanya
   
 4. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #4
  Feb 16, 2013
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,329
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu EMT
  Sioni kama hili jambo ni la ajabu kwa sababu hizo practice huwa zinafanyika siyo kwa third world media hata kwa Western world media. Cha ajabu tu Erich Kabendera ku-whistle halafu akaamua vile vile ku-blower his former boss.

  Media 'illicit activity' and bias zipo tu. Hata newspaper za Tanzania ukizisoma mara nyingi utagundua mlengo wa kila gazeti kisiasa na mara nyingi linakuwa soft au hard kwenye chama cha siasa kipi. This is the reality.

  In UK, kwa sasa kuna kesi na kulikuwa na Independent enquiry kuhusu kampuni ya Media Mogul, Rupert Murdoch inayoitwa News Corporation kutoa rushwa kwa polisi na kuingilia mawasiliano ya mtoto ambaye alikuwa abducted and murdered na kuwaacha wazazi wakifikiria kama yuko hai kila wakiacha voicemail ambazo gazeti lilikuwa linazisikiliza na kuandika kinachoendelea.

  Independent enquary waligundua kuwa mawaziri wakuu na wanasiasa nchini UK wanajipendekeza kwa Managing Editor ili wao na vyama vyao waandikwe vizuri kwa mtaji wa kujijenga kisiasa. Mpaka kesho, kuna watu wamefungwa na wengine wana kesi mahakamani.

  kama ulifuatilia wakati wa misuguano kabla ya vita vya Irak, kwenye Media za Western Countries especially, UK and USA. Kulikuwa na bias za waziwazi ambazo zilisababishwa na vi-memo kutoka government ili waandike kumponda Saddam Hussein, even ALjazeera TV was banned in USA during war kwa kigezo cha patriotism.
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,599
  Likes Received: 5,928
  Trophy Points: 280
  Vyombo vya habari vinatakiwa kuwa na some semblance of objectivity na principles fulani vinavyosimamia.

  Hukatazwi kutaka kutengeneza hela, hukatazwi hata kuwa pro-CCM, lakini hizi habari za vimemo vya rais asiandikwe vibaya ni scandal ambazo wenzetu wameziepuka tangu enzi za FDR huko.

  Na hata leo tunajua kwamba The Wall Street Journal is right leaning and conservative while The New York Times is generally left leaning and liberal, lakini siku ukisikia moja kati ya haya magazeti owner katoa kimemo rais asiandikwe vibaya itakuwa scandal.

  Itakuwa gazeti linabadili objective ya chombo cha habari kutoka ku ripoti habari na kuwa chombo cha propaganda zisizofuata maadili ya uandishi.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,125
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana kumbe magazeti haya hata siku moja hayaandiki uovu wa serikali. Ni magazeti ya matukio tu na si analysis. Haitashangaza pia kwamba na magazeti mengine mengi sana nchini yamezibwa mdomo; except Tanzania daima (kidogo), Raia mwema na Mwanahalisi wakati wake. Aliwahi kusema wakati fulani mhariri msaidizi wa gazeti la Tanzania daima (Ngurumo I guess) kwamba alilazimishwa apokee bahasha ya kaki ili aache kumwandika vibaya Kikwete.

  Siamini kwamba haya ni maamuzi ya mmiliki wa haya magazeti, binafsi naamini hata yeye amepokea order kutoka kwa wenye mamlaka ya juu, ndiyo akatoka kwenda kuimplement kwa watu wake. Kama hali ndiyo hii basi Kikwete ana wakati mgumu sana. Maana sasa anaongoza nchi kwa njia ya polisi plus kuyafunga midomo magazeti. Ndiyo maana mambo yanakwenda hovyo na waandishi wanashindwa kuyaweka wazi? Na wale wanaojaribu kuyaweka maovu ya seriakli bayana magazeti yao yanafungiwa kabisa (eg Mwanahalisi).

  Mikakati iandaliwe ili baada ya utawala wake kuisha tukutane mahakamani
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2013
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 64,019
  Likes Received: 61,690
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lukolo si unaona lilikoishia Mwanahalisi kwa kuandika habari ya ukweli kabisa kuhusu mauaji yaliyotaka kufanywa dhidi ya Dr Ulimboka. Halafu Kikwete anadanganya umma wa Watanzania kwamba limefungiwa kwa kuandika uchochezi. Naona kati ya sasa na 2015 zitafanyika juhudi kubwa sana za kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na vile ambayo havitaheshimu matakwa ya mafisadi basi vitaishia kufungiwa.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. makavulaivu

  makavulaivu JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2013
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KUHONGA WAHARIRI AU WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NI KUPOTEZA MUDA NA RESOURCE ZAO, HASA KTK HUU UWANJA MPANA WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI AMBAPO VIPO VINGI.

  Vyombo vingi vimejikuta vinapaswa kuchagua kati ya haya.
  1.Kuficha uovu wa watawala,kupokea rushwa,ahadi za vyeo na kuishia kupoteza hadhi na wasomaji
  mfano ni majira, Rai.
  2.Kufichua uovu,kupata wasomaji wengi na kukumbana na vikwazo vingi na adhabu kwa watawala
  Mfano Mwanahalisi etc
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2013
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 120,159
  Likes Received: 245,794
  Trophy Points: 280
  tunaona hata shughuliza Bunge sasa ni siri yao..................tutafika kweli?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2013
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  I think kumkosoa ni muhimu ila kumkashifu sio vizuri

  Tatizo letu tena hasa wanasiasa, hawawezi hata kuchanganua basic stuffs... ukimwambia ukweli au kumkosoa atakuja na catalogue ya takataka kulazimisha kuwa umemkashifu

  I failed to work with politicians
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2013
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,311
  Likes Received: 1,608
  Trophy Points: 280
  Hapa nilishapata kuandika kwamba, hili suala la Haki ya Vyombo Vya Habari Wahariri wawaachie wamiliki wa vyombo hivyo kupigania haki hiyo na badala yake wao(WAHARIRI) wapiganie haki yao ya kutominywa na wamiliki wa vyombo vya habari! Siamini hata kidogo kwamba Mhariri wa Tanzania Daima au Uhuru wanaweza kuandika habari iliyo kinyume vyama vya CHADEMA au CCM hata kama habari hiyo ipo! Matokeo yake kila siku Tanzania Daima wataishia kuimba mazuri yaliyopo na yasiyokuwepo na kuacha mabaya yote yaliyopo kwa CHADEMA...hali kadhalika, Uhuru nao hivyo hivyo!

  Nirudi upande wa IPP...nazani kule hakuna kabisa uhuru wa kuandika! Mie ni mnazi wa Yanga....wakati wa Uchaguzi mkuu uliopita nilisikia suala la Yusuf Manji kuchukua form za kugombea Uenyekiti wa Yanga! Hakika sikuamini coz' sikuona busara aliyotumia ya kujiingiza moja kwa moja kwenye soka la TZ! Ikawa kila siku na-tune Radio One nisikie habari za Manji.....hadi uchaguzi ule unaisha, Jina la Manji halikutajwa ingawaje kila siku majina ya wagombea wengine yalikuwa yanatajwa! hapo ndipo nikaja kukumbuka bifu la Mzee Mengi na Manji(Recall Mafisadi Papa scenes)! Nikafahamu kwamba lazima kwenye News Desks kuna Standing Orders za kutotangaza habari za Yusuf Manji! Maulid Kitenge, Mzee wa Kupepesa alipepesa kweli kweli!
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2013
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,230
  Likes Received: 4,595
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  Umeishaona makala yeyote kwenye Tanzania Daima ikiwakosoa Mbowe au Dr Slaa.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2013
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,476
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  Ritz,
  Unataka kuniambia magazeti ya IPP ni mali ya Kikwete? Au ni mali ya CCM?
   
 14. akenajo

  akenajo JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 1,564
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kumbe kuna mambo yapo under carpet yanaendelea thanks jf
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2013
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,230
  Likes Received: 4,595
  Trophy Points: 280
  Hapana siyo mali ya Kikwete wala CCM ni gazeti binafsi wala siyo la serikali kusema linaendeshwa na kodi zenu huwezi kulipangia.

  Hata CUF wanasema IPP Media hawaandiki habari tofauti na Chadema na CCM.

  Labda nikuulize Tanzania Daima ni gazeti la Chadema ndiyo maana huwezi kukuta makala ya kumkosoa Mbowe au Dr Slaa.
   
 16. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2013
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,311
  Likes Received: 1,608
  Trophy Points: 280
  Ritz,
  Mwache Jasusi apumzike....hawezi kuwa na jibu la swali lako!
  Hii nchi si kwamba hakuna uhuru wa vyombo vya habari bali hakuna uhuru wa kuandika habari!
   
 17. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2013
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,775
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Uhuru wa habari upo at stake!!
  Au ni ile kadi ya CCM alochukua mwaka juzi?
  Au ni utimilizi wa "unabii" wa Sumaye kuwa ukitaka biashara zako zikunyokee jiunge na CCM?
  Poor Mengi!!
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hata Mwanahalisi pia lilikuwa linasifu tu upande mmoja wa upinzani walikatazwa na chadema kuisifu serikali japo tu kwa machache mazuri?

  Mlengo wa Gazeti hilo haukuwa wa kusifu chochote kuhusu serikali.
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tuwe wakweli CHADEMA itakapoanzisha TV yake itakuwa inaruhusu kumsifu KIKWETE?

  Vyombo vya MENGI si vya UMMA ni vyake wala haviendeshwi kwa kodi yetu.
   
 20. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Inawezekana Serikali ilisaidia kulipa faini ya Mengi kwa huyu Mama wakapewa masharti ya kutomuandika vibaya Mh. JK
   
Loading...