Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,073
Magavana wa benki kuu za mataifa ya Afrika Mashariki wamekanusha madai kwamba wao ndiyo wanachelewesha mchakato wa kufanikisha hatua ya kuwa na shirikisho la kifedha chini ya utaratibu wa jumuiya hiyo ili iweze kutumia sarafu moja na hivyo kupunguza gharama za kuendesha biashara. Aidha wametoa hakikisho kwamba uchumi wa jumuiya hiyo hautaathirika mara moja kutokana na hatua ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.
Source: DW
Source: DW