Magari yote ya kubeba maiti yatakiwa kulipa Tsh milioni

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,740
21,181
Kila siku Serikali kupitia vitengo vyake mbalimbali wanabuni njia za kuongeza mapato.

Tozo mpya ya shilingi milioni moja kwa magari yanayokodishwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo ya kubeba miili ya marehemu inatazamiwa kupitishwa na kuanza kutumika, kumbuka tozo hiyo inayosimamiwa na (LATRA).

IMG_20210118_191710.jpg


Nini maoni yako mdau wa JF?


UPDATES:
Mjadala ukiwa unaendelea huku wadau hasa wa mitandaoni ndiyo wenye kujua kwa ukaribu kile kinachoendelea kwa haraka, sasa ipo hivi.

Tukiwa tunashangaa hili la gharama za kukodisha gari la kubeba maiti, hivi karibuni watu waliofariki wameonekana wakisafirishwa kutoka vijijini hadi hospitali kwa ajili ya kuhifadhia maiti wao.

Hali hiyo inatokea nchini huko DRC Kwa kuwa hawana uwezo wa kukodisha gari ya kusafirisha na kuhifadhia maiti.

Watu wanaamua kuifunga kwa vitambaa kisha wanapakia nyuma ya bodaboda kisha jamaa wa bodaboda anaelekezwa aipeleke pale inapotakiwa, safari hii inaweza kuchukua masaa hadi 10 wakati mwingine zaidi kulingana na eneo analotakiwa kufikisha maiti.

👇🏿Hizi hapa chini ni baadhi ya picha zikionyesha maiti zilizo tayari kwa safari kwenye pikipiki.

Screenshot_20210124_102217.jpg
Screenshot_20210124_102121.jpg
 
ngoja ufe wewe mkeo/mtot wako/wazazi wako au yeyote atakayekuwa anahusika nammaiti yako abandikwe milioni hiyo
Akitozwa mmachinga 20,000/- ya kitambulisho safi kabisa, akidaiwa retention fees ya mkopo wa elimu safi kabisa. Akitozwa mfanyabiashara wa kusafirisha maiti ni dhambi kisa anafanya biashara?

Acheni unafiki kodi /tozo hazitungwi bila kuangalia biashara inatengeneza faida kiasi gani na tozo liwe kiasi gani. Hiyo ni biashara kama biashara nyingine za usafirishaji zinazolipa hizo tozo (LATRA) au kisa wamegusa maiti?
 
Akitozwa mmachinga 20,000/- ya kitambulisho safi kabisa, akidaiwa retention fees ya mkopo wa elimu safi kabisa. Akitozwa mfanyabiashara wa kusafirisha maiti ni dhambi kisa anafanya biashara? Acheni unafiki kodi /tozo hazitungwi bila kuangalia biashara inatengeneza faida kiasi gani na tozo liwe kiasi gani. Hiyo ni biashara kama biashara nyingine za usafirishaji zinazolipa hizo tozo (LATRA) au kisa wamegusa maiti?
vyote hivyo vimelalamikiwa
 
Lakini kama wanakomoa hiyo ni shauri Yao kwani zinatubeba Sisi na ndugu zetu uchwala?? Hizo si huwaga wanakodi wenyewe ma don king. kwani ziko ngapi hapa mjini mpaka tumalize bando kuziongelea....??.........lakini sawa Tu kwani si zinafanya biashara ya pesa ....na Sheria ya pesa ni kuweka pesa upate pesa.
 
Sasa kuna maendeleo nchi hii? Kwanini baada ya miaka 60 ya uhuru shule zetu nchi nzima ni hohe hahe kwenye kila dept? Kwanini 2.7 trillions inakwapuliwa hazina na huyo anayejiita mwendawazimu kisha anagomea uchunguzi?

Kwanini wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara wanadhulumiwa? Kwanini Watanzania wasio an hatia wanabambikiwa kesi fake kisha kuporwa pesa zao eti ni faini? Kwanini trillions za walipa kodi zinatumika bila idhini ya Bunge?
 
Akitozwa mmachinga 20,000/- ya kitambulisho safi kabisa, akidaiwa retention fees ya mkopo wa elimu safi kabisa. Akitozwa mfanyabiashara wa kusafirisha maiti ni dhambi kisa anafanya biashara? Acheni unafiki kodi /tozo hazitungwi bila kuangalia biashara inatengeneza faida kiasi gani na tozo liwe kiasi gani. Hiyo ni biashara kama biashara nyingine za usafirishaji zinazolipa hizo tozo (LATRA) au kisa wamegusa maiti?
Kumbuka gari hizi zinalipa kodi ya biashara kama ilivyo gari zote za biashara ya kukodishwa.
Njia rahisi ni kubeba kwenye guta au pawatila.
 
Back
Top Bottom