Yajue Magari yanayoongoza kwa ubovu duniani

freelander ni gari nzuri na economy,mhm ongeza ukubwa wa mashimo ya kwenye gasketi hutopata tatizo tena la kuchemsha. Nadhan mtengenezaji alijisahau juu ya khali ya joto kwa huku kwetu hivyo hilo tatizo hutokea. Discovery itabaki n gari niipendayo,niitumiayo na nitakayotumia wakati wote wa uwepo wangu hapa dunia. Ni gari inayofanya kile nikitakacho gari inifanyie na kwa wakati huku ikiwa n economy kwa mafuta.
 
Mwenye uwelewa na Nissan Dualis, vipi gari hii ni nzuri kwa matumizi ya kawaida....kuhusu mafuta, vipuri, nk.
 
Kwenye Toyota Prius sio kweli. Mimi naendesha Prius Hybrid ya mwaka 2011, mpaka leo ishatembea miles zaidi ya 200,000. Miles 10 ni km 16. Haina tatizo tazizo lolote, nakwenda nninapotaka. Full tank lita 40 ambazo zinanipa wastani miles 420.

Sasa sijui Prius ipi inayoisema wewe.

Big up Mkuu mimi ninayo Toyota auris hybrid ya 2011 niliagiza uk huwa nasafiri nayo sana tu full tank nafika mwanza bila kuongeza mafuta, naenda moshi na kurudi dar kwa full tank, mwaka wa pili haijawahi kunisumbua kitu chochote
 
Hakuna gari bovu mitandaoni issue ni mafundi wetu ohh D4 eti ni pasua kichwa,wanaozijua D4 hawasemi.ufundi wetu ni shida sana na matumizi ya gari hiyo ndio shida nyingine we unaambiwa mafuta tumia unleaded tuu wewe unaweka ya matopeni kisungwa na kidumu chako unadhani rvr yako itadumu?? We nunua gari tumia muda wake ukipita ikisumbua tafuta nyingine..
 
mpita-njia,
Baada ya hizo kuisha kinatokea niniii mzeee maana naona kachajii kapo mwishooii...au ikiisha ndio unapaki gariii
 
Freelander ina tatizo gani coz kuna mtu nimeshamlipa nusu bado nusu ili nichukue kitu.

Anaiuza 12M mi nilimwambia achukue 10 akakubali ila anasema engine ndo inashida but kanambia kuwa inaweza patikana for less than 2M.
Asee,mwambie akurudishie hela yako haraka,unanunua umaskini,tafuta rav 4 mkuu,au suzuki escudo
 
Back
Top Bottom