Yajue Magari yanayoongoza kwa ubovu duniani

Freelander ina tatizo gani coz kuna mtu nimeshamlipa nusu bado nusu ili nichukue kitu.

Anaiuza 12M mi nilimwambia achukue 10 akakubali ila anasema engine ndo inashida but kanambia kuwa inaweza patikana for less than 2M.
Katika list yote hapo gari ambalo lina tatizo kubwa ni Freelander na tatizo lake ni Gasket na kuchemsha hasa kwa nchi zetu za joto kali
 
Labda kuna ukweli ama la, but mafundi wetu wengi wenye ufundi wa kurithi toka kwa mjomba, sijui after std7 basi anashinda gereji after few years ni fundi, basi kitu ikimshinda anaanza gari mbovu, haifai, rumors zinatapakaa, jamani mafundi wetu muende shule, gari nyingi sasa hivi ni so electric mda sio mrefu wachina ndo watakua mafundi wetu
Aliekwambieni kama ubovu wa gari unapimwa kwafundi kushindwa kutengeza nani?

Ubovu wa gari unajulikana kwa common problems, na matatizo yenye kujirejea au yalokosa suluhisho la permanent.

Mfano BMW 7 series za mwaka 2002-2004, zinasifa ya kubuma gearbox, gear haijibadilishi na inakulazimu uendeshe spidi ndogo ili engine isihitaji gear kubadilika, inasababisha ulaji wa mafuta mwingi. Pia zina matatizo ya idrive system ambayo mara ina freeze na kukataa kufanya kazi.

Fundi akishindwa kulitengeza sio kwamba gari bovu, ila matatizo ya hio gari sokoni ambayo ni common yapi? Hayo matatizo common basi ndio yatasababisha gari kuitwa mbovu. Ikiwa xtrail nyingi zinatatizo la kuganda piston bila sababu na kufanya isizi basi hilo bovu
 
Kama ndio HV Tanzania hatuwezi kupata mtumba wa Gari. MTU anakaa na Gari miaka 20!!! Hongera kwa kutunza chombo
Izo gari zilikuja mpya wanajeshi walikopeshwa miaka ya nyuma ivi,so haikuja mtumba so kukaa miaka 20 ni kawaida sana kwa gari iliyonunuliwa 0 km
 
Gari za ccm

kweli aisee hizi gari CCM waikuwa nazo kibao saivi sijui ziko wapi. naona sasa hivi wanatumia viberiti {land cruiser}..
ila kwa mtazamo wangu kila gari ni mbaya kama hakuna matunzo ila kama unaitunza vizuri unaweza ukasahau gereji ulienda lini. Gari matunzo
 
Back
Top Bottom