Yajue Magari yanayoongoza kwa ubovu duniani

Hakuna gari isiyopata ubovu kama inatumika usipotoshe watu,labda ongelea upatikanaji wa spea kuwa mgumu nitakuelewa...ukiwasikiliza hao jamaa zako wa YouTube wanaotafuta viewers hutakaa ununue gari lolote kwani hakuna waliloliacha...gari yoyote inayotumika huharibika na spea zipo genuine na feki...ukimiliki gari angali huna uwezo wa kulihudumia utaishia kuponda kila gari hasa yasiyokuwa common Tanzania....wazambia na wengine huko landlocked countries wananunua magari bila kujali brands...ila Tanzania most of us lazima gari liwe Toyota tatizo mafundi wetu wengi sio professionals wanatumia uzoefu hivyo wengi kuwadanganya watu eti "ooh gari hili na lile huwa halitengenezeki"not true.

Hata spea sio tatizo zama hizi spea unaagiza from overseas inafika Tanzania within 10 days...mfano hawa jamaa MegaZip - Genuine OEM Parts From Japan, USA, UAE | Online Store wana supply hata nuts au logo ya gari tena genuine...spea zao hakuna hakuna mfano search gari lolote unapata spea yake kisha unatoa oda inaletwa kwa FedEx au DHL etc..

UKILIPENDA GARI LOLOTE NUNUA...muhimu uwe na Pesa za kulihudumia tu mafundi professional wapo.

Ni bahati mbaya hata humu JF kuna jamaa anajifanya fundi kumbe muongo anaigiza kama vehicles analyst ilhali anagugo tu...acheni kupotosha watu gari unainunua used na utaitumia hata maisha yako yote muhimu maintenance tu.
 
N'yadikwa, Umenena vyema sana...
Mafundi wa Tanzania ndiyo wanaopotosha watu kuwa gari ni toyota pekee...lakini kuna brands nyingine zinafanya vizuri sana.
 
Yaani wewe unamsikiliza huyu tapeli anayekwenda kula pizza halafu unatuletea humu
 
Unachosema kweli coz niya yangu ni kuambia watu wasinunue magari hayo yajiwa used lamda kama ni mpya lakin kama used usisubutu kununua izo gari hapo
Iyo mazda mr8 kuna kaka yangu moja alipata ela za puh akanunua iyo gari mateso aliyopata namuonea huru sana mpaka leo hii lipo juu ya jiwe coz katengeneza sana bila mafanikio
Wewe gari mpya unaweza kununua bojo jaribu hata vitz mpya 0km uone moto wake
 
N'yadikwa, Mkuu, unaweza nisaidia namna ya kuagiza. Mfano nataka side mirror ya Toyota raum old model ya 2001.

Nafanyaje, na wanalipa kwa njia ipi PayPal au credit card?

Vipi wasipotuma, refund hawasumbui wala kuchelewesha?
Asante
 
Mkuu, unaweza nisaidia namna ya kuagiza. Mfano nataka side mirror ya Toyota raum old model ya 2001.

Nafanyaje, na wanalipa kwa njia ipi PayPal au credit card?

Vipi wasipotuma, refund hawasumbui wala kuchelewesha?
Asante
Hawasumbui nimeshaagiza mara nyingi,ingia hapo kwenye link press order then unalipa kwa PayPal ukishindwa nenda kwa banker wako atakusaidia kupress order au fika pale Puma petrol station Oysterbay kuna agent wa online trade atakusaidia kuagiza...alternatively side mirror ya Raum hata Befoward wanazo kwenye duka lao la spea,hawa hawana magumashi wacheki
 
Niko Dom, befoward hao wanawza nitumia huku.

Pia nimejaribu kuingia hapo naona kama wanataka niingize namba ya parts kitu ambacho sijui zinasomwa wapi kwenye gari hiyo

Usichoke, huenda kupitia mie wakaelimika mamia mkuu
Hawasumbui nimeshaagiza mara nyingi,ingia hapo kwenye link press order then unalipa kwa PayPal ukishindwa nenda kwa banker wako atakusaidia kupress order au fika pale Puma petrol station Oysterbay kuna agent wa online trade atakusaidia kuagiza...alternatively side mirror ya Raum hata Befoward wanazo kwenye duka lao la spea,hawa hawana magumashi wacheki
 
Umenena vyema sana...
Mafundi wa Tanzania ndiyo wanaopotosha watu kuwa gari ni toyota pekee...lakini kuna brands nyingine zinafanya vizuri sana.
Kweli ndugu jamaa zangu wa vijiwe bubu wanawadanganya sana raia, matokeo yake wanaogopa kununua gari aina tofauti na Toyota wakati kila gari inatengenezeka...labda mtu aje na factor ya uchumi mbovu wa watu binafsi kushindwa kuhudumia magari ya brands nyingine ambayo spea zake ni aghali kiasi k.v Suzuki,Mitsubishi,Audi,VW na nyingine.
 
Back
Top Bottom