Magari ya Zimamoto fedha za BoT?!!! EL!!!??

Mjukuu

New Member
Dec 10, 2007
4
0
Jamani haya magari ya zimamoto ndiyo yale yaliingizwa na dogo, Lukaza wa Kernel? yule anayehusishwa na BoT, EPA? Je, si ndiye aliyekwenda Monduli kuchoma nyama siku mbili kabla ya Chrrimas, Desemba 23? NAULIZA TU MAANA NASIKIA HARUFU MBAYA. SIPENDI KUSEMA HADI YANIUME


Waliokwamisha usajili wa magari ya zimamoto kukiona

2008-01-22 10:11:27
Na Restuta James


Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, imeitaka serikali kuhakikisha kuwa, utafiti wa kina unafanyika kuhusu suala lililochelewesha usajili wa magari ya zimamoto kwa miaka miwili.

Aidha, kamati hiyo imeitaka serikali kuweka taarifa ya utafiti huo hadharani na kuwachukulia hatua zinazostahili wahusika waliochelewesha usajili huo.

Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. William Kusila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za bunge.

Alisema magari hayo yalikuwa yameagizwa kwa ajili ya Manispaa ya Dodoma, Kigoma, Temeke, Moshi, Kibaha, Songea, Ilala, Morogoro na Mtwara.

``Oktoba 19 mwaka jana kamati ikiwa katika shughuli zake za kawaida ilitembelea kikosi cha zimamoto ambapo tulibaini kuwa magari tisa ya zimamoto yaliyoingizwa hapa nchini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita yalikuwa hayafanyi kazi kutokana na kutosajiliwa. Jambo hili liliishtua kamati,`` alisema.

Alisema kamati yake inahitaji kufahamu jambo lililokwamisha usajili kwa magari hayo na kueleza kuwa hapa nchini kuna upungufu mkubwa wa magari hayo.

``Serikali isilichukulie suala hili kwa wepesi...ni jambo zito kwa sababu hatuoni kwa nini tatizo liwe kwenye usajili, lazima kuna tatizo hata katika manunuzi`` alisema.

Aliongeza kuwa mara baada ya kamati yake kugundua ucheleweshwaji wa usajili, magari hayo yalisajiliwa na kuanza kazi.

Kwa mujibu wa Bw. Kusila, tayari Ofisi ya Waziri Mkuu imekwishaunda tume kwa ajili ya kuchunguza suala hilo.

``Kwa kweli sifahamu muda ambao tume hii itamaliza kazi lakini tunaomba kupata maelezo ya kina maana tuna upungufu mkubwa sana wa magari haya na hatuoni sababu ya kukwamisha usajili tena kwa kipindi cha miaka miwili,`` alisema.


ANGALIZO: WAHARIRI WOTE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UAMUZI Serikali kuunda Tume ya Wataalamu kuchunguza magari ya zimamoto yaliyoingizwa nchini lakini hayakufanyakazi kwa kutosajiliwa ni kupata ufumbuzi wa kudumua wa suala hilo.
Maelezo hayo yalitolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Celina Kombani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana (Jumatano Jan. 23, 2008) kufafanua suala la magari hayo.
Naibu Waziri alisema magari hayo yalinunuliwa kwa utaratibu uliowekwa na kwamba wakati wa usajili yalibainika mapungufu ambayo yalihitaji ufafanuzi kutoka Halmashauri husika na watengenezaji.
Mapungufu hayo ni pamoja na kukosekana kwa dhamana (warranty) na hivyo kujenga hisia kuwa magari yaliyonunuliwa yalikuwa makuukuu, alisema.
Kombani alisema kuwa kutokana na magari hayo kutosajiliwa mapema, Waziri Mkuu aliitisha kikao Desemba 3, mwaka 2007 cha viongozi wa Wizara pamoja na Wakurugenzi wa Haamshauri husika ili kupata maelezo kuhusu ucheleweshaji wa kusajiliwa magari hayo.
“Kutokana na maelezo ya pande zote kutomridhisha Waziri Mkuu ililazimu kuunda Tume ya Wataalamu ili wachambue kama taratibu zilifuatwa kujiridhisha kama magari hayo ni mapya au makuukuu na kisha kutoa ushauri ili mapungufu ya namna hiyo yasijitokeze tena,” alisema.
Aliongeza: “Ikumbukwe kwamba madhumuni ya Serikali ya kuunda Tume hiyo ni kuhakikisha kuwa suala hili linapata ufumbuzi wa kudumu katika muda mfupi ili wananchi wapate huduma za uhakika na bora.”
Kuanzia mwaka 2004/2005 na 2006/2007 Halmashauri za Manispaa za Kigoma/Ujiji; Moshi, Songea, Ilala, Dodom a, Morogoro, Mtwara, Temeke na Halmashauri ya Mji wa Kibaha, zilitengewa fedha za kununua magari ya zimamoto.
Magari hayo yalikuwa yamesimama bila ya kufanyakazi kutokana na kutosajiliwa kwa karibu miaka miwili.
(mwisho)
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Alhamisi Jan. 24, 2008

http://majira.co.tz/mobile/page.php?soma=sayansi&habariNamba=3686

06.09.2007 0143 EAT
Karnel yaeleza umuhimu wa vifaa vya kuzimia moto

*Yasikitishwa Watanzania kukosa elimu ya kukabiliana na moto
*Wamiliki majumba na magari wengi hawana vifaa vya zimamoto
*Yabainika tatizo si uwezo wa kiuchumi bali elimu kwa wananchi

===========================================================
TANZANIA imekuwa ikikabiliwa na matukio mengi ya ajali za moto lakini tahadhari inayochukuliwa kukabiliana nayo hailingani na madhara yake. Katika makala haya, Mwandishi Wetu REUBEN KAGARUKI, anaeleza jinsi ukosefu wa elimu unavyochangia tatizo hilo, wajibu wa Serikali na ushauri wa wataalamu wa kampuni ya Kernel inayouza vifaa vya kuzimia moto.
==========================================================
KWA Jiji la Dar es Salaam ni jambo la kawaida kusikia au kuona magari la vikosi vya Zimamoto yakipiga ving'ora yakielekea maeneo yenye ajali za moto.

Ajali nyingine za moto zinasababisha hasara na watu kupoteza maisha. Inawezekana ajali nyingi zinazuilika ikiwa Watanzania watachukua tahadhari mapema.

Tahadhari hizo ni pamoja na kuhakikisha watu wanaweka vifaa vya kukabiliana na moto pindi unapotokea ndani ya nyumba na kwenye magari. Hata hivyo bado hilo halifanyiki kama inavyotakiwa matokeo yake, watu wanazidi kupoteza maisha na mali zao kwa ajali ya moto.

Matukio ya ajali za moto yanayotokea mara kwa mara yananikumbusha tukio nililoshuhudia jijini Dar es Salaam miaka miwili iliyopita, ambapo watoto watatu wa familia moja na mama yao walipoteza maisha baada ya nyumba walimokuwa wakiishi kuungua.

Nyumba walimokuwa wakiishi ilikuwa na thamani ya zaidi ya sh. milioni 40, lakini ilionekana wazi kuwa imejengwa bila kufuata taratibu za mipango miji, hivyo kuwa vigumu hata magari ya vikosi vya zimamoto kufika eneo la tukio kirahisi.

Watu walijitahidi kuzima moto kwa maji bila mafanikio, ndipo alipotokea mzee akiwa na mitungi miwili yenye gesi ya kuzimia moto. Mzee huyo alisaidia kwa kiwango kikubwa hadi ukapatikana upenyo wa watu kuingia ndani na kufanikiwa kuokoa watoto wawili.

Kama mzee huyo asingefika na mitungi hiyo, watoto hao wasingepona. Mzee huyo aliyekuwa akiishi nyumba jirani amepanga na hakuwa na uwezo mkubwa kiuchumi, lakini kwa kutambua athari za moto, aliweza kununua mitungi hiyo na kukaa nayo nyumbani mwake.

Kilichonishangaza zaidi ni mmiliki wa nyumba iliyoungua ambaye ni msomi na aliweza kujenga nyumba yenye thamani ya sh. milioni 40, lakini akashindwa kununua mitungi ya kuzimia moto kwa ajili ya tahadhari inayoanzia viwango vya sh. 9,000.

Ajali hiyo ilinifumbua macho na kuanza kutathmini majumba na magari ya kifahari yaliyopo Dar es Salaam siku yakishika moto, wamiliki wake watafanya nini kuokoa mali hizo ambazo wametumia gharama kubwa kuzipata.

Kimsingi hakuna sababu ya msingi ya watu kushindwa kununua vifaa vya kukabiliana na ajali ya moto bali hali hiyo inasababishwa dharau na ukosefu wa elimu.

Leo hii ni jambo la kawaida kumkuta mtu akiendesha gari ya kifahari lenye thamani ya sh. milioni 40 lakini akashindwa kununua kifaa cha kuzimia moto na kukiweka kwenye gari lake kwa ajili ya tahadhari.

Mfano, siku moja niliwahi kumsikia aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Bw. John Chiligati, akisisitiza umuhimu wa watu kuweka vifaa vya kuzimia moto kwenye nyumba na magari kwa ajili ya tahadhari.

Baada ya kumaliza kuzungumza na makamishna wa Zimamoto, Bw. Chiligati alianza kutembelea vikosi vya zimamoto, lakini baada ya kuchunguza kwenye gari lake, hakukuwa na kifaa cha kuzimia moto kama alivyokuwa akihimiza.

Hali hiyo ni kielelezo kuwa si kweli kwamba watu wanashindwa kununua vifaa hivyo kwa sababu za kiuchumi, bali ni kutojali na ukosefu wa elimu kuhusiana na umuhimu wa vifaa hivyo.

Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Bw. Rashid Salum (47), anasema inashangaza watu kushindwa kununua vifaa vya kuzimia moto vinavyouzwa bei ndogo wakati huo huo wanamudu kununua magari na kujenga nyumba za kifahari.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Kernel inayosambaza vifaa vya kuzimia moto, Bw. Fred Musika, anasema ingawa madhara ya moto ni makubwa kwa maisha ya binadamu na mali zao, lakini hatua za kukabiliana na athari zake bado ni ndogo.

Anakiri kuwa Watanzania wengi hawajaona umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto kwenye nyumba na magari yao.

Kinachoshangaza zaidi tabia ya wenye magari na majumba ya kifahari kuona ni gharama kununua vifaa vya kuzimia moto wakati uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Bw. Musika anasema tatizo hilo pia linawakabili hata wamiliki wa kampuni ya mabasi ya kusafirisha abiria. Anasema basi moja linauzwa kwa sh. milioni 100 lakini hawanunui vifaa hivyo.
"Wanasahau kuwa ukitokea moto wanaweza kupoteza basi zima pamoja na maisha ya watu na mali zao," anasema Bw. Musika.

Anasema kampuni yake ya Kernel ipo tayari kusambaza vifaa hivyo kwa wenye mabasi na kutoa elimu kuhusiana na jinsi ya kuvitumia.

Bw. Musika anasema wenye magari ya kusafirisha mizigo nje wameanza kuona umuhimu wa kuwa na vifaa hivyo ndani ya magari yao. Anasema si busara mtu apewe kusafirisha mzigo wa sh. milioni 200 kwenda Burundi, lakini ashindwe kununua kizimia moto.

Bw. Musika anasema wanavinunua ili kuepuka hasara kubwa wanayoweza kupata endapo moto ukitokea kwenye magari yao na matokeo yake kujikuta wakilazimika kulipa fidia ya mamilioni ya fedha.

Anataja wadau wengine wanaotambua umuhimu wa kampuni yake na kwenda kununua vifaa vya kuzimia moto na kupata mafunzo kuwa ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Akieleza shughuli za kampuni yake, Bw. Musika anasema ni pamoja na kusambaza vifaa vya kuzimia moto, kutoa elimu na ushauri wa kitaalamu kujisiana na jinsi ya kuepukana na ajali hizo na jinsi ya kukabiliana nazo.

Anasema wao kama wasambazaji wa vifaa zaidi ya aina 120 ya kuzimia moto wanahamasisha wananchi wafika kwenye ofisi zao kujionea vifaa mbalimbali ambavyo wavinasambazwa na Kernel.

Bw. Musika anasema hawaishii hapo, bali pia mteja hupewa muda wa miezi sita ya kutumia kifaa kilichonunuliwa kwenye kampuni zao na pindi ikitokea ajali ya moto kikashindwa kufanyakazi wao wanawajibika kumlipa fidia iliyotokana na hasara aliyopata.

"Tuna uhakika na kazi tunayofanya ndiyo maana tumejiwekea utaratibu huu," anasema Bw. Musika na kuongeza kusema kuwa baada ya miezi sita kupita wanavifanyia ukarabati tena na mteja akikataa, basi yanayomkuta wao kama kampuni wanakuwa hawahusiki.

Tangu kampuni hiyo ianze kutoa huduma hiyo nchini, mwaka 1998 hakuna ilipotokea ajali ya moto na vifaa vyao vikashindwa kufanya kazi. Baadhi ya vifaa vinavyosambazwa na kampuni yake kuwa ni pamoja na mitungi yenye ukubwa tofauti yenye gesi ya kuzimia moto, makoti na buti zisizopenya moto na bomba za kumwaga maji hadi ghorofa ya sita.

Vifaa vingine ni vile vya kutumika kuzima moto kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi. Anasema vifaa hivyo vinakuwa kama mpira na vikirushwa eneo lenye moto kinapasuka kuuzima mara moja.

Mbali na hiyo anasema wanatoa elimu kwa watu wanaotumia na majiko ya gesi majumbani mwao kuwa makini na kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kuzimia moto.

"Vifaa vya gesi ni hatari, hivyo ni lazima watu wawe makini vinginevyo wanaweza kupata madhara makubwa," anasema Bw. Musika. Eneo jingine ambalo wamekuwa wakitoa ushauri ni kuhusiana na taratibu za ujenzi.

Anatoa mwito kwa Serikali kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto ndani ya nyumba zao.

"Serikali ichukue jukumu la kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto, sisi tutakuwa wasambazaji," anasisitiza Bw. Musika.

Anasema tatizo hili linaweza kupatiwa ufumbuzi ikiwa Serikali itaanzisha programu maalumu ya kuelimisha jamii na kuchukua hatua kuhakikisha wananchi wanakuwa na vifaa hivyo ndani ya nyumba na magari yao.

Kwa upande wa matatizo wanayokabiliana nayo, Bw. Musika anasema ni kuwepo kwa watu wanaosambaza vifaa vibovu. "Watu wanaosambaza vifaa vya kuzimia moto visivyofaa ni hatari na inabidi wachukuliwe hatua," anasema Bw. Musika.

Mbali na hiyo, anasema tabia hiyo inaharibu sifa ya kampuni ya ndani na inaonekana kuwa Waafrika wao kazi yao ni kuuza vifaa vibovu.


©2008Business Times Limited .
 
Hivi karnel haina uhusiano na Liyumba?mtu anayeweza kupata AOA au MOA atueleze kwa uwazi.
 
kuna moto ulitokea ikulu wakati wa Che Nkapa tuliambiwa ni moto uliosababishwa na pasi je ilikuwa pasi ya mkaa au ipi? naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom