Magari ya kifahari ikulu, na serikali..kenya na rwanda waachana nayo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari ya kifahari ikulu, na serikali..kenya na rwanda waachana nayo!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Jul 8, 2009.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Wakati mawaziri wetu wakingangania kutembelea magari ya kifahari yanayotumia mafuta mengi na gharama inayofikia milioni 100 kwa kila gari...na wakati IKULU wakitumia magari ya kifahari kwa misafara ya rais na viongozi wengine[mfano rais wetu siku hizi akitoka na nissan patrol...basi msafara wote ni nissan patrol,siku akitoka na vx nyeusi basi msafara wote ni vx,pia siku anatoka na mercedes s class basi ni zote..,na mara nyingine hutoka na set ya BMW X5...Ni zote...]..hapo bado waziri mkuu na makamu....majirani zetu wao wameamua kuchukua affirmative action...kwa kuongoza kwa mifano...  [​IMG] President Kibaki's motorcade. The President on Tuesday rejected eight new limousines. Photo/CHRIS OJOW
  By BERNARD NAMUNANEPosted Tuesday, July 7 2009 at 22:30

  In Summary
  • President and First Lady say they are backing Treasury's austerity measures


  State House on Tuesday rejected eight new luxury cars, signalling the government's determination to observe austerity measures.

  A statement from State House quoted President Kibaki and First Lady Lucy Kibaki saying they did not order and were not aware of the purchase of the cars that had just been delivered.

  The Nation learnt that the cars - four luxury Mercedes Benz limousines, three 4-wheel-drive Toyota Land Cruiser Prados and one Nissan Hardbody - were bought last month.

  The purchase of the vehicles appears to have been part of last month's last-minute spending by ministries and government departments to avoid returning unused funds to the Treasury.

  The Presidential Press Services (PPS) said that the decision was meant to give support to measures announced by Finance minister Uhuru Kenyatta to cut down government expenditure.

  The minister, in his Budget speech last month, announced that Cabinet ministers will be limited to cars of not more than 1800cc. The number of cars allocated to each minister was also reduced, but some ministers have openly ridiculed the measure and announced that they would not surrender their limousines and fuel-guzzling 4x4s.

  "State House will support austerity measures announced by the Minister for Finance on a freeze in the purchase of new vehicles. As an immediate measure, we are ordering the return of the eight vehicles that were purchased without our knowledge. We also appeal to all ministries to support the efforts by the Finance minister to cut down on government costs," said the President and the First Lady.

  The four Mercedes Benz limousines and a Nissan Hardbody were bought from DT Dobie, while the three Prados were acquired from Toyota Kenya

  "Following the instructions, the eight vehicles were this morning delivered to the dealers," PPS said.

  Accounting officer

  The vehicles, the Nation learnt, were delivered to State House last week.

  They cost about Sh50 million, with the Mercedes S Class vehicles fetching about Sh8 million each, the Toyota Prados Sh4 million each and the Nissan Hardbody going for about Sh2 million.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  At least Ikulu yetu hawajanunua magari ya wizi from UK ...unless unataka kutuambia kitu kuhusu viongozi wa upinzani wetu wanaotembea na ma Vogue ya wizi from UK
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  Kaka Game ..nilijuwa tu kuwa kama mtu ana akili ya kuku anaweza kufikiri nimeanzisha hii thread kwa ajili ya siasa...but for sure hapa inahusu taifa ,kama taifa viongozi wetu lazima waoneshe mfano ..kama kweli wanataka kuokoa pesa zetu za kodi....

  kwa namna ulivyo jibu inaashiria kuwa hoja yeyote hata ikiwa na uzito namna gani huwa unapinga au kukubali ...kutokana na hisia za imani ya mrengo wa kisiasa.....acha!! huko ni KUFIKIRIKA!!!

  SUALA la matumizi ya magari nimeliona linaongelewa sana bungeni...,na hata rais amelitolea kauli akiwataka viongozi waache kutumia magari ya kifahari...waziri mkuu ameshapiga marufuku halmashauri kununua magari haya...lakini pamoja na rai zote za viongozi wakuu bado yananunuliwa.....kama mwananchi unapoona viongozi wa jirani wanachukua hatua za ziada kuzuia ufujaji huu...sina budi kuleta habari hiii hapa...huenda ikawa chachu kwa viongozi wetu....

  ....BADO UNAFIKIRI NI SIASA???...UCHAGUZI BADO!!!...
   
 4. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Viongozi wangapi wa upinzani wanaotumia magari hayo ya wizi kutoka UK? Someone needs to do his job here. Kama GT anaelewa wazi kuwa viongozi wa upinzani wanatumia magari ya wizi halafu hamna mtu aliyefunguliwa mashitaka, then kuna ubovu hapa.
  Itakuwa vyema Bw. GT utoe evidence usaidie serikali kupitia vyombo vya sheria ili sheria ichukuwe mkondo wake. Kama huna evidence nafikiri itakuwa jambo la busara kuomba APOLOGY.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hawahitaji kununua magari ya wizi. Tayari wizi ulishafanyika treasury.
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  GT this is too low for you. Wizi wa magari toka Uk ?
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ..bora useme na wewe kaka!!!
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kutaja ma Vogue ya wizi from UK naona nimetouch some nerves

  mhhh haya
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Thats too low of you kaka. Umechemsha.
  Viongozi wa upinzani wanatumia hela zao za mifukoni serikali inatumia hela yangu na yako na ya wengine, au huoni uchungu kwasababu upo UK?!
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  are you okay....gari la mtu binafsi we yeyote linahusu nini,..hapa tunajadili public funds ...nashangaa sana siku hizi sijui ukoje!!...yaani wewe unataka kufananisha ...gari za wananchi wa kawaida na state cars!!!..

  houni alichofanya kibaki na kabla kagame kukataa kutumia magari ya kifahari kabla ya kushurutisha wasaidizi wao watumie magari ya bei nafuu ni kuongoza kwa mfano...au unataka kubisha tu....

  just take one example ...nikiongelea mfano watanzania..

  1.msafara day one [5 pcs S class Mercedes benz SPECIAL@ 160,000usd = 800,000usd[ 1.1billion tsh]

  2.msafara day 2[5 pcs BMW 5 SPECIAL @ 200,000 = 1,000,000USD[1.3BILLION TZS]

  3.MSAFARA DAY 3[5 PCS NISSAN PATROL FULL LOADED SPECIAL] @85,000USD = 425,000[550MILLION TZS]

  4.MSAFARA DAY 4 [5 PCS PRADOS .SPECIAL.HIZI ZIMENUNULIWA JUZI TU ]@90,000 = 450,000USD [620MILLION TSH]

  MAGARI YA MOJA KWA MOJA YA IKULU YA MSAFARA WA RAIS [YALIYO IKULU YA DAR ES SALAAM PEKEE] YANAKADIRIWA KUFIKIA DHAMANI YA 4BILLIONS T SHILLINGS...

  HIYO NI MBALI YA MAGARI YANAYOSHIRIKI MAALUM KWENYE MSAFARA WAKE YALIYO ATTACHED POLICE NA KWENYE VYOMBO VINGINE......

  HIYO NI MBALI YA MAGARI YA RAIS YALIYO MOJA KWA MOJA ...KWENYE IKULU NDOGO...ZA MIKOA MIKUBWA KAMA ARUSHA ,DODOMA NA MWANZA...IKULU ZA MIKOA HIYO ZINA MAGARI YAKE NA HAIHITAJI KUSAFIRI NA MAGARI AKIENDA MAENEO KAMA HAYO...

  ZOTE HIZO NI PESA ZA WALIPA KODI!!! ZETU!!...SASA KAMA TUNATAKA KUBANA MATUMIZI SI TUANZIE JUU...ILI WA CHINI WAOGOPE WAFUATE!!!

  NJIA MOJA MUHIMU KWA RAIS KUBANA MATUMIZI YA MAGARI NA KUOKOA MUDA NI KWA KUTUMIA HEALCOPTER ZAIDI...KUPAMBANA NA FOLENI ZA BARABARANI.....NA KUPUNGUZA FLEET YA MAGARI YAKE...HII INAWEZA KUFANYIKA KWA KUACHA KABISA KUNUNUA MAGARI MAPYA KWA AJILI YAKE KWA MIAKA YOTE ILIYOBAKI....AKIBADILISHA MAGARI MIAKA 5 MARA MOJA SI MBAYA...LAKINI SISI HADI MIAKA 5 HAIJAISHA TUMESHANUNUA JOZI 3 ZA MAGARI MABYA KWA RAIS....alipoapishwa alipewa mercedes benz s class mpya kabisa...lakini yeye ameshaongeza BMW,NISSAN PATROL, na sasa PRADOS!!!

  hapo hujaongelea makamu wa rais,waziri mkuu ,mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa mikoa,wilaya ...na maafisa wengine waandamizi wa srikali[nadhani mnajuwa kuwa mwaka huu pekee wamenunua ....LANDCRUIZER GX NEW MODEL 100 UNITS]@90,000USD.....
   
 11. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  .....kaka angalia.....'Vdole' na 'Mdomo' ni sehemu ndogo tu za Mwili,ila hukiponza 'Kichwa' kizima!!..hope you know whatImean.
   
 12. H

  Huduma Member

  #12
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAPA Tanzania kazi. Maana viongozi wetu wachovu sana wanaamini kwamba heshima na utukufu wao unatokana na kuwa na magari ya kifahari na ofisi zenye eyakondishenaa eti na vimbwanga bwanga vingine nyumbani, nyumba ndogo na maofisini. Wengine ninasikia eti wana 'lifti' zao wenyewe na chakula chao mchana kinatoka Steers au Subway au Kempinsky!

  Eti wakienda Ulaya ingawa mshahara wao haufiki milioni 3.5 wanakaa kwenye hoteli ambazo tozo lake kwa siku ni dola 2,000-3,000. Ni nani anawalipia hawa au ndio nani za EPA na Benki Kuu zilikoishilia ???

  Kuachana na magari ya kifahari na mambo mengine ya anasa kwa viongozi wa nchi masikini kama Tanzania sio tu kitu kinachowezekana bali kitu cha lazima. Lakini inategemea aina ya uongozi na dhamira ya chama kilicho madarakani kama ni kutumikia wananchi au ni kubebwa na kulishwa kwa njaa, kiu, umasikini na matatizo ya wananchi.

  Na ishuu kubwa waliyoiona wenzetu wa Kenya na Rwanda sio magari yenyewe. Maana kuyanunua hata kama ni milioni 80 mpaka 100 kwa gari sio ghali sana. Ughali baba unakuja wakati wa kujaza petroli au dizeli. Na safari zao unajua haziishi hao. Kama mkuu anakwenda majuu kwanini wao wasiende mikoa yote ndani ya nchi ? Kazi. Ukichanganya na vipuri na 'hereni ' au speapati za magari hayo sasa inakuwa mzigo usiobebeka. Wao hawaoni. Kama wewe umepanda punda kwani uzito wausikia weye ? Punda mwenyewe halii, hakatai kwenda wategemeaje. Semeni mtakavyosema lakini hakuna kitakachofanyika. Kinachotakiwa ni kwa Watanzania wenyewe kuandamana, ikishindikana kuyakamata magari yote ya anasa na kumuona Jaji Mkuu kama yule wa Honduras kutangaza kwamba magari hayo ni persona or automobile non grata hapa nchini!!!!
   
 13. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu asante sana, hapa ni kuchagua upande wa kuwa na kili za binadamu ama za kuku!
   
 14. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  .....i can hardly see any major constuctive measures put into place with such an atmosphere btw. the leaders.just listen to this:
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=n13FAzuY_fA"]YouTube - Raila steps up attack on Kibaki[/ame]
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Bipolar disorder?.........wengine inabidi wasimamiwe ili wanywe dawa zao.........
   
 16. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ...it takes one to know the other,and i'nt the one mate!
   
 17. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  HUJAMUELEWA Ogah!

  Alikuwa na ku support wewe umeelewa vingine. LOL
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ........yaani nimecheka kweli kweli..........asante Mkuu
   
 19. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Na bado kuna watoto wanakalia mifuko ya rambo kwa vile hakuna pesa ya kununulia madawati.
   
 20. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #20
  Jul 9, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya baadhi ya watu wenye "makengeza ". wa..le ambao bwana mkubwa akija hapo kwa bibi au kwa mayankee wanapata kuokota makombo mezani kwake kwa kuambulia visenti vya ukuwadi hawaoni haya.....wananchi wanapata taabu sana..

  Mnajuwa gari moja la kawaida la serikali [90,000$]..linaweza kuanzisha shule mbili za msingi au sekondari ukichanganya na nguvu za wananchi?

  mnajuwa LIMOUSINE moja tu la rais ...gharama yake inatosha kujenga majengo ya hospitali yenye hadhi ya wilaya ...maeneo ya vijijini????

  sasa nado tunataka ikulu ambayo kila mwaka wako busy kuangalia kuna gari gani latest imetoka wanunue???....na kama rais anakubali kupanda ina maana amebariki...na viongozi wengine kuanzia makamu hadi maafisa wa serikali wanaiga......wote wanataka magari mapya...

  kuna magari ya dola $25,000[landrover ,ford] hawataki wanataka GX V8 ya dola 90,000 bila kodi.....na ajabu wanagawa magari bila protocal ...waziri anapanda GX V 8 na maafisa pia wapande hilohilo???
   
Loading...