Magari ya abiria: Aliyewadanganya abiria wote tunapenda kelele alikosea sana

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,962
6,087
Wakuu,

Gari za abiria zimekuwa na kawaida ya kuweka mziki sauti ya juu mno mpaka unajiuliza nini hiki.

Mtu unatoka katika mihangaiko yako iwe kazi ama kibarua unafika katika gari unataka nafsi itulie na kutafakari yanayoendelea katika dunia yetu lakini unashangaa mara mamuu aah mamuu, mara sijui otimbi.

Kiukweli mimi binafsi sipendezwi na kelele na huwa nachukia sana vile sina namna nyingine, inashangaza katika movie mtu anapanda gari na kupata usingizi kabisa lakini hapa kwetu utulivu hakuna.

Ukibahatika kupata gari halina mziki utashangaa hali ya barabara na yale mashimo usingizi haupatikani kabisa.

Tena siku hizi hata mwendokasi nao wanapiga muziki tena sauti ya juu kiasi kwamba huwezi kutafakari.

Wengine hatuna uwezo wa kununua magari yetu lakini isiwe ndio sababu ya kututesa na hayo makelele.
 
Wakuu,
Gari za abiria zimekua na kawaida ya kuweka mziki sauti ya juu mno mpaka unajiuliza nini hiki!

Mtu unatoka katika mihangaiko yako iwe kazi ama kibarua unafika katika gari unataka nafsi itulie na kutafakari yanayoendelea katika dunia yetu lakini unashangaa mara mamuu aah mamuu, Mara sijui otimbiii
Kiukweli mimi binafsi sipendezwi na kelele na hua nachukia sana vile sina namna nyingine, inashangaza katika movie mtu anapanda gari na kupata usingizi kabisa lakini hapa kwetu utulivu hakuna, ukibahatika kupata gari halina mziki utashangaa hali ya barabara na yale mashimo usingizi haupatikani kabisa...

Tena siku hizi hata mwendokasi nao wanapiga mziki tena sauti ya juu kiasi kwamba huwezi kutafakari,
Wengine hatuna uwezo wa kununua magari yetu lakini isiwe ndo sababu ya kututesa na hayo makelele
Mwendokasi unayotaka upate utulivu wa kutafakari ni hizi hizi za Dar es Salaam Tanzania?
 
Singeri imepamba moto daladala za DSM,pia gari likiwa kimya kuna baadhi ya abiria wanakuwa na wireless visimu vya tochi anakiwasha nakukiweka sikioni,sasa kinakuwa hakidaki mawimbi vizuri na kupelekea noise pollution
 
Haaaaaahaaaaa umenikumbusha mjomba wangu juzi kati hapa alikata nyaya za spika katoka zake huko wanampigia kelele akamwambia dereva "punguza sauti" dereva hasikii basi alikaa siti ya nyuma kule wakashangaa tu kimyaaa!

Unatumia akili ya ziada kuondoa ugomvi
 
Acha uzuzu wewe, mnakaa kwenye foleni masaa mawili unatoka au kwenda kazini si bora muziki uwe tiba ya foleni kwa muda huo. Ukiona kero, nunua gari lako.
 
Kapande matatu nairobi ndio utajua magari ya abiria yanapiga mziki. Ukiingia tuu hata simu hauwezi pokea
 
Wakuu,

Gari za abiria zimekuwa na kawaida ya kuweka mziki sauti ya juu mno mpaka unajiuliza nini hiki.

Mtu unatoka katika mihangaiko yako iwe kazi ama kibarua unafika katika gari unataka nafsi itulie na kutafakari yanayoendelea katika dunia yetu lakini unashangaa mara mamuu aah mamuu, mara sijui otimbi.

Kiukweli mimi binafsi sipendezwi na kelele na huwa nachukia sana vile sina namna nyingine, inashangaza katika movie mtu anapanda gari na kupata usingizi kabisa lakini hapa kwetu utulivu hakuna.

Ukibahatika kupata gari halina mziki utashangaa hali ya barabara na yale mashimo usingizi haupatikani kabisa.

Tena siku hizi hata mwendokasi nao wanapiga muziki tena sauti ya juu kiasi kwamba huwezi kutafakari.

Wengine hatuna uwezo wa kununua magari yetu lakini isiwe ndio sababu ya kututesa na hayo makelele.
MNAOTAKA UTULIVU nunueni magari yenu,
 
Mimi ni mpenzi wa daladala zenye mziki inafkia hatua kama daladala halina mziki nashukaa na folleni za dar kama tunaenda msibani
 
Me huwa nakata waya za spika
Dah! Nishawahi kufanya hivyo. Unakuta kwenye daladala wameweka spika siti ya nyuma kabisa, halafu yule mpumbavu anayewasha huo mziki yeye yuko mbele kazi yake kuhatarisha maisha yenu kwa kujitia ubize na redio.

Mbaya zaidi, mnapigiwa SINGELI au TAARAB, mpaka unashuka kichwa kinauma. Mi siku hiyo nikajionea ujinga, nikakata waya wa spika na nail cutter, kelele kwisha
 
Hakuna miziki ya kipumbavu na isiyoakisi hata nusu ya maadili bora kwa watoto kama taarabu na singeli.

Ningekuwa na mamlaka ningeifungia kabisa isisikike.

Back
Top Bottom