Magari kazi kama haya yangetolewa kodi kurahisisha biashara na kilimo.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Moja la tatizo kubwa kwenye biashara na kilimo Tanzania ni usafiri ingekuwa vema serikali ingetoa kodi zote kwenye magari kazi kama malori na pickups. Hili litarahisisha watu kupeleka mbolea shambani na hoho, vitunguu na nyanya sokoni gharama iwe ni kununua na kusafirisha tu. mnaonaje?
03.jpg
fuso_header6.jpg
 
Iyo ishu inawezekana tatizo wa bongo ni mabingwa wa modification anaweza agiza hilo la maziwa asilipe kodi na akalitumia kubebea mafuta,hayo mengine akatumia kubebea vitu kama mkaa na baadae serikali kukosa kodi

Mi kwa maoni yangu naona vitu kama martekta yangetolewa kodi iwe free ili tuepukane na jembe la mkono

Na mashine zote za kilimo na wangetoa kodi ili ziingie nyingi tupate viwanda vingi kwa wazawa wazitumie zifanye uzalishaji tulipe kodi kupitia faida hapo tutakua tumeifikia nchi ya viwanda mapema tena kwa kuwa na viwanda vingi vya wazawa
 
nafikiri mashine za shambani tayari zina msamaha wa kodi. Wachache wanaweza fanya ujanjaujanja. pia naona hata wakimodify na gari akabaki ya kazi siyo mbaya. gari ya kazi ni mtaji ni kama mashine za viwandani. faida ya gari ya kazi inapita mbali faida ya kodi. huku kwetu kuna 110 za 80's bado zinabeba karoti.
 
Sasa tatizo siyo ubingwa wa modification, rule of law, good governance, etc! E.g. mbona Dubai hawana hawachakachui, mbona Ulaya hawachakachui?
 
nafikiri mashine za shambani tayari zina msamaha wa kodi. Wachache wanaweza fanya ujanjaujanja. pia naona hata wakimodify na gari akabaki ya kazi siyo mbaya. gari ya kazi ni mtaji ni kama mashine za viwandani. faida ya gari ya kazi inapita mbali faida ya kodi. huku kwetu kuna 110 za 80's bado zinabeba karoti.
Tatizo bandari itapoteza mapato kwani asilimia zaidi ya 80 ya watanzania ni wakulima hivo wanaweza kua na shughuli mbadala (non agricultural activities) na wakatumia kibali cha kilimo kupitisha mizigo bandarini na baadae faida ikabaki kwa wananchi tuu pasipo serikali nayo kufaidika
 
  • Thanks
Reactions: MC7

siyo kwamba kuwe na vibali maalumu kwa wakulima. iwe kila atakaye agiza gari la kazi apewe msamaha wa kodi. so haiwezi kuwa kama uhuni wa taasisi za dini. kwa maoni yangu gari kazi zinafaida kwa uchumi kuliko kodi wanazokata ziingiapo. wanauchumi wanaita capital goods.
 
Mugabe aliweza sema sasa hivi kachemka tani 10 kuendelea ilikua hakuna VAT, Bus lilikua halina VAT na Pick up kuanzia tani moja na nusu ndio unalipa VAT ndio kupindi hicho Zimbabwe kilimo na usafirishaji na uuzaji chakula Nje ya Nchi ulikua juu sana..sasa kama Bongo tuu gari zote kodu..
 
moja la tatizo kubwa kwenye biashara na kilimo Tanzania ni usafiri. ingekuwa vema serikali ingetoa kodi zote kwenye magari kazi kama malori na pickups. hili litarahisisha watu kupeleka mbolea shambani na hoho, vitunguu na nyanya sokoni. gharama iwe ni kununua na kusafirisha tu. mnaonaje?
03.jpg
fuso_header6.jpg
Mkuu zitajaa Pick Up mjini mpaka utashangaa!
 
wakazi wengi wa mjini hata kama ni mfanyakazi utakuta ana duka, bar, mgahawa, kuku, kanga, nguruwe, kwale, ng'ombe, analima nje ya mji bamia, tikiti, nanasi, embe, etc. bado majiji yetu hayana uchumi wakujiendesha kama ya ulaya ambako kipato kutokana na professional kinatimiza mahitaji yote. haata watu wa mjini wanahitaji hizi gari.
 
Kama mh,raisi akiliona hili akalifanyia kazi nchi yetu itasonga kwan hayo magari yatakuwa cheap,
 
Mugabe aliweza sema sasa hivi kachemka tani 10 kuendelea ilikua hakuna VAT, Bus lilikua halina VAT na Pick up kuanzia tani moja na nusu ndio unalipa VAT ndio kupindi hicho Zimbabwe kilimo na usafirishaji na uuzaji chakula Nje ya Nchi ulikua juu sana..sasa kama Bongo tuu gari zote kodu..
naona uchumi unamlazimisha akusanye kila senti, ila ni jambo zuri sana kwenye kuboost kilimo na biashara.
 
siyo kwamba kuwe na vibali maalumu kwa wakulima. iwe kila atakaye agiza gari la kazi apewe msamaha wa kodi. so haiwezi kuwa kama uhuni wa taasisi za dini. kwa maoni yangu gari kazi zinafaida kwa uchumi kuliko kodi wanazokata ziingiapo. wanauchumi wanaita capital goods.
Lakini ikumbukwe kuwa mbinu mojawapo ya kupunguza msongamano na idadi ya vyombo vya moto ni kuweka kodi kubwa katika bandari mana taifa litakuwa na magari mengi kupelekea uchafuzi wa mazingira na msongamano kama vile ilivo India
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom