Magari chakavu kuchafua mazingira ni hoja mfu, Twende kwa fact

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,809
2,000
Kumekua na hoja kua magari chakavu hasa yaliyotengenezwa miaka 2000 kurudi nyuma ni chakavu na yanachafua mazingira hivyo kupigwa kodi ya kufa mtu ili yasingie nchini,hoja hii ni mfu kwa kua kuna mambo amabayo hayajakaa sawa. Twende,

umaskini-kuna barabara mbovu ambazo kiukweli zinahitaji magari kuanzia miaka 2000 kurudi nyuma, nenda makete,Chunya,Ludewa,Babati na maeneo ya Morogoro kuna barabara mbovu kiasi cha kuhitaji gari imara sio mayai za 2010+.

Huduma za kijamii vijijini hasa Ambulance zianaweza kupatikana kwa uwepo wa magari hasa vijijini. Kodi kubwa kwenye magari kumepelekea hata ukosefu wa magari vijijini. Uwepo wa magari ungepunguza hata demand ya ambulance maana usafiri ungekuwepo hata gari binafsi.

USA ambaye ndiye mchafuzi mkuu wa mazingira anasema suala la globla warming na uchafuzi wa mazingira ni porojo tuu hivyo ataendelea kujenga viwanda kadri awezavyo, je magari chakavu ni hatari kuliko viwanda???

Matumizi ya makaa ya mawe, bado tunaona makaa ya mawe hasa viwandani ni sawa ila magari ndo yanachafua mazingira Si sawa..tuache double standard

Matatizo ++++, Magari mengi yalitlyotengenezwa 2010+ yanakufa kuliko magari ya 1990's. Ni rahisi sana kudumu na gari ya miaka ya 90 kuliko ya miaka ya 2000 hivyo dumping rate ya magari ya miaka 2000 ni kubwa kuliko ya miaka 90 na garama kuyatunza ni kubwa sana.

Sekta ya usafiri na usafirishaji imedorora sana vijijini hivyo kuimarisha usafiri na usafirishaji kodi inabidi ipungue. Miaka hii ya 2019 kuna baadhi ya maeneo wanasafiri na malori, pikup, na fuso, hii inatokana na either barabara na ukosefu wa magari.

Tukubali: kama tunajenga viwanda ambavyo ni mchafuzi mkuu wa mazingira basi tupunguze kodi ya magari ili kuendana na kasi ya viwanda hasa kwenye usafirishaji wa mazao ya kilimo na bidhaa.

NB: Tuangazie hii mada kwa muktadha wa wilayani na vijijini... Sio mjini....... ambapo usafiri na usafirishaji ni duni. Kuna vijiji vingi mazao yanaharibika kisa hakuna usafiri wa uhakika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom