Magari aina ya BMW na Mercedez Benz huwa na matatizo gani?

Wakuu Ni kwa nini watu wengi hawapendelei gari hizi? Tatizo ni bei na gharama za maintainance ama ni nini shida kubwa ya haya magari..?)
Bmw na Merc sio gari za kawaida. Ni gari luxury kwahio hata maintanance yake ipo juu, sio sawa na carina,corolla etc. Ila ukiangalia bei ya used from Japan haina tofauti sana na toyota kwasababu ya demand. Ila gharama ya maintanance iko juu vile vile kwahio ukiwa nalo jipange usije kuambiwa shock absorber moja tzs 350,000 ukapata ugonjwa wa moyo.

Ila ni gari za starehe kweli na mbio mbio kweli.
 
tmp-cam--995243486.jpg
 
Ila benz series C nayapenda sana. CIF cost kati ya Dolla 2750-3500, tena ya mwaka 2002-2005! Haya mazuri ni yale ya cc 1790
Pia napenda Volkswagen Touran ya mwaka 2004-2007! Zipo za cc 1380,1590 na 1980.CIF ni dollar 2500-3500!Nyingi zenye cc 1380 ndo zina bei ya Dollar 3000-3500
 
Je spea na mafundi wa Magari haya ambayo ni stable barabarani vipo kwa Dar? Mafundi wanapatikana wapi? Spea zinapatikana wapi? Na kwa nini ziwe adimu?
Kabla sijanunua naomba wajuzi watuambie
 
Bmw na Merc sio gari za kawaida. Ni gari luxury kwahio hata maintanance yake ipo juu, sio sawa na carina,corolla etc. Ila ukiangalia bei ya used from Japan haina tofauti sana na toyota kwasababu ya demand. Ila gharama ya maintanance iko juu vile vile kwahio ukiwa nalo jipange usije kuambiwa shock absorber moja tzs 350,000 ukapata ugonjwa wa moyo.

Ila ni gari za starehe kweli na mbio mbio kweli.
Vipi kuhusu Volkswagen kiongozi, hizi ndogo kama Polo na Golf. Naona bei zake ni za kawaida kw mtumba wa japani, hata CC zake ni kawaida tu, mbona hazitumiki sana huku kwetu? Au nao maintenance zake ni shida??
 
Labda hujaangalia vizuri tu. Sasa hivi VW ni nyingi sana, moja ya sababu spares zake zipo nyingi na bei sio juu sana kulinganisha na bmw/merc.

Ukiniuliza ununue gari gani ya Euro nitakwambia VW yoyote ile. Popular model bongo ni Touareg,touran,golf,polo.
 
mafundi wapo dar na Arusha pia spea zipo kwa dar cheki na makampuni yanayouza used spare wanazo kila kitu kuanzia milango injini,arusha utapata kila kitu Nairobi wapo agents wakubwa wa hizi models BMW,MERCEDES BENZ ,AUDI PIA UKIFANYA CHOICE ni vyema ukachagua AUDI ni muungano wa kampuni nne ikiwemo Mercedes benz ,bmw faida yake ni upatikanaji wa spea ni rahisi,
 
Labda hujaangalia vizuri tu. Sasa hivi VW ni nyingi sana, moja ya sababu spares zake zipo nyingi na bei sio juu sana kulinganisha na bmw/merc.

Ukiniuliza ununue gari gani ya Euro nitakwambia VW yoyote ile. Popular model bongo ni Touareg,touran,golf,polo.
Kweli, hizo models ulizotaja zote ni nzuri. Hii tendency ya kununua Toyota tu inabidi watu wabadilike. European products ni bomba sana.
 
Vipi kuhusu BMW 318i na 320i ni gari ambazo nazipenda sana na kila mara nazipigia mahesabu sana,uimara wake ukoje na mapungufu yake? Kuhusu spare na mafundi nahisi wapo maana siku hizi ni nyingi sana hasa DSM
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom