Magamba ya ccm kutangaza nia,kumesababisha njaa kwa wauza magazeti.

Mwaipaja ima

JF-Expert Member
Oct 30, 2014
404
76
Kuanzia magamba yaanze kutangaza nia ya kugombea Urais ununuaji wa magazeti umekuwa mgumu sana,wauzaji wanalia njaa stori za magamba hazivutii watu kununua magazeti.
 
Inasemekana kuwa Shetani ni muongo na baba wa huo uongo. Asemapo uongo ndo kweli yake. Kamwe usitafute kweli kwenye uongo. CCM ni hewa na baba wa hao hewa, wakikuahidi kitu jua umeahidiwa ahadi hewa na kamwe kwenye hizo ahadi hewa zao hutakaa upate kitu bali hewa tu.
Kumbuka, maneno yao yoote ni maneno ya watu ambao hawako kwenye system. UKAWA ndo walitakiwa wayaseme hayo maneno kwani wao wapo nje ya system, iweje leo Mwingulu utangaze utakalofanya kama ukiwa kiongozi wakati weye ni kiongozi tayari??? Iweje Wasira useme utaleta mapinduzi ya Kilimo wakati weye ni waziri wa Kilimo hicho hicho? Iweje Mbunge wa miaka 30 useme utabadilisha umasikini wetu nawe hujawahi toa mchango wako ukakataliwa?
Wangesimama na kutueleza kwamba kumbukeni mwaka uleee nilitoa mchango wangu wa mawazo haya yafuatayo wakayakataa naomba nipeni ruksa niliweke hili kwa vitendo sasa. HAKUNA ila ahadi hewa za kutudanganya tukupe ofisi.
Hatutaki kukusikia na ofisi hatukupi, hivyo gazeti hatununui kwani hatuweki rekodi hewa
 
Back
Top Bottom