Magamba Wamtosa Vengu wa Orijino Komedi!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Kwa muda sasa nimesikia huyu kijana amekuwa kitandani kutokana na malazi. Hivi karibuni nilisikia kuwa jamaa anaumwa 'seriously' kwa nyeti za juu juu ni kwamba anaugua saratani ndani ya kichwa. Binafsi ikaja taswira jinsi huyu dogo na wenzake kina Msanja, Seki na wengineo jinsi walivyotumika na CCM katika kampeni zao za uchaguzi. Kama sijakosea, hawa jamaa walipita kila mahali nchini kote ambako magamba walijua kuna mtaji wa kura za wananchi. Hakuna ubishi kwamba kwa sehemu kubwa ushindi wa magamba mwaka 2005 ulichangiwa pia na hili kundi ambalo nadhani sikosei nikiliita TOT namba 2. Binafsi nilidhani kwamba walau CCM wangemkumbuka huyu dogo hata kwa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi maana namuona ni kama familia ya magamba kwa jinsi alivyokuwa akipigania kura zao kuliko walivyomtosa sasa ambapo nna uhakika kwa muda aliokaa hospitalini, ni wazi uwezo wa matibabu ya juu na yenye ubora kwa sasa hana. Wakati dogo anaendelea kuugua pale muhimbili, tafadhalini kwa wale ambao ni wafuasi wa magamba humu jamvini, wafikishieni kina Miraji taarifa hizi wazifikishe kule kwa watoto wa magamba-UVCCM-walau waonyeshe ubinadamu kwa kumsaidia huyu kijana kwani mchango wake kwa magamba ulikuwa si haba. Nawasalimu wote, Asanteni!
 
mkuu inawezekana una hoja nzito ila ulivyoandika hata haieleweki kwani imejaa ushabiki na ni kama vile ulikua unawahi kwa kuhisi mwingine atapost kabla yako
 
huwa sijui kupanga hoja naomba nisaidie ku editi then uipost wewe! unajua hapa nilipo nasinzia
 
We ni mtanzania na yule ni mtanzania mwenzako, unaweza kumsaidia au ukawaomba watu tofauti tofauti wakamsaidia na sio kina magamba tu mkuu! Kuna wagonjwa wengi tu wakiwemo akina mama wajawazito mpaka leo wanaangamia na watoto/kuacha watoto kwa kukosa huduma ya matibabu stahiki, na ni haohao walipiga debe na kutoa kura kwa magamba na bado hawawajali, wana tofauti gani na huyu kijana au kwa sababu ye ni maarufu??? Kuna watoto wengi wanaokufa na magonjwa yanayoweza kutibika lakini viongozi wetu ndo kwanza wanazidi kuchakachua!! Sitaki kuliangalia hili suala kwa ushabiki, ila tujue kuwa naye alikuwa na haki ya kukishabikia chama alichokipenda so tusimhukumu kwa hilo wala kuwalaumu magamba kwa ugonjwa wake au unataka kutuambia kuwa kila chama kinatakiwa/nilazima kuwatibu walokipigia debe?? Kama alilipwa is up to yeye na hapo ndo achanganye malipo yake yamuume ili siku ingine asipokee na afanye kwa hiari!!!
 
Kuna kitu hapa watu wanakose origina komedi wakiwa wanawafagilia magamba wapo kazini hiyo ndo ajira yao, ujasirimali na niugumu kwenye hiyo fani yao kama mnavyoona alasivyo mwenzetu angeweza kujikimu kwenda india huku kutibiwa. au hata kagrupu kama kangekuwa na uwezo wangemchangishia. Lakini ndo hivyo wao wapo na kinasiye chini ya piramidi waliopo juu tu ndo wanafaidi na kupelekana india siye twabanaa muhimbili.
 
nampatia pole kijana ila kama yeye ni mtanzania mwenzetu mimi na wewe inatuhusu kumsaidia.anza wewe kwanza kama mfano nasi sisi tutafuatia.
 
Maskini kumbe bado yuko hospitali? Ni kweli ana kansa ya kichwa? Ooh my God plz help Vengu....
 
toeni ushabiki kwenye hii ishu,
hapa huyubwana angekuwa libya enzi za gadafi, angepelekwa india kutibiwa na serikali, lakini hapa kwetu,ni watu fulani tuu wanathaminiwa. i hate this elite.
 
Sasa km watu wanaenda kutibiwa malaria india kweli wanashindwa kmpeleka kijana huyu huko india ili akatibiwe?......................
 
Na mimi nadhani kwamba watanzania tuwe na moyo wa kusaidia wenye matatizo kama tunavyochangia harusi. Kijana huyu sijamuona siku nyingi kwenye luninga.
 
Duuuuhh, Mungu ampe afya njema tena,
Niliwahi kusikia huyu dogo alifukuzwa kwenye kundi lao la Komedi kabla ya hajaanza kuumwa, sijui kama ni kweli.
 
Back
Top Bottom