Magamba walipotufikisha. Soma picha hii na utafsiri sahihi

Kwa namna hii ndio JF itakavyorudisha heshima na hadhi yake, badala ya kuanza kushambuliana ni vyema tukawa tunauliza maswali, ili kujibishana na kulumbana kwa HOJA.

Majukumu ya msingi ya serikali ni kutunga na kusimamia sera. Kusimamia sheria za nchi na kutoa huduma kwa raia wake.

Sasa tukianza kuongelea sera, mfano katika elimu, serikali ilisema itajenga shule za sekondali katika kila kata. Imefanya hivyo, lakini swala hili linachangamoto zake na bado serikaji inafanya jitihada kukabiliana nazo. Kuna haja ya kuwa na vifaa vya kufundishia, kama madawati, chaki, vitabu na mahitaji mengine ya msingi ya shule. Nyumba za walimu nazo pia ni kipaumbele cha serikali katika utekelezaji wa sera hii.

Kuna huduma kama ujenzi wa miundombinu ya maji, barabara+madaraja na ya umeme. Haya ni majukumu ya msingi ya serikali. Na tumeshuhudia barabara nyingi za mikoa zikijengwa kwa kiwango cha lami. Huduma ya umeme pia bila kusahau ujenzi wa madaraja kadha wa kadha.

Vituo vingi vya afya vimejengwa na kuongezeka kwa madaktari na wahudumu katika vituo husika. Muhimbili wameweka kitengo maalumu cha magonjwa ya moyo ili kupunguza ulazima wa watanzania kwenda nje ya nchi sanasana India ili kupata matibabu ya magonjwa ya moyo.

Upatikanaji na ugawaji wa huduma ya maji safi na salama, hapa sina haja ya kuongelea maana tumeshuhudia ujenzi wa miundombinu kadha ya maji na wananchi wengi wamepunguziwa mzigo wa kutembea masafa marefu kupata huduma hii ya msingi.

Katika swala la kusimamia kilimo kupitia dhana ya "kilimo kwanza", tumeona jinsi ilivyowasaidia wakulima katika kupandisha thamani mazao yao na kuuza nje kwa wingi na kujipatia kipato. Lakini kutokana na majanga kadha ya njaa yaliyoikumba nchi yetu, serikali iliwazui wakulima kuuza nje mazao ili kulikombomboa taifa na janga la njaa.

Kukabiliana na mfumuko wa bei, hapa kupitia kazi nzuri inayofanywa na gavana wa benki kuu, tunaweza kununua bidhaa mbalimbali kwa fedha kiduchu, mfano kutumia sh. 1000/= kupata sahani ya wali, hii ni kutokana na kazi ya gavana kulinda thamani ya pesa. Sio kazi ndogo ndugu yangu.

Ulinzi na usalama, kusimamia na kulinda mipaka ya nchi na ile ya ukanda wa bahari.

Majukumu yako mengi na wamefanya mengi sana, lakini hawajaweza kufanya yote na bado awamu ya nne haijaisha. Sio vyema kuanza kudhihaki serikali kuwa IMESHINDWA.

Huu upuuzi wako umechelewa kuuandika, ulipaswa kuuandika at least in the 1990s ambapo watu walikuwa wanategemea gazeti la uhuru kupata habari! We can see and think, and you are f.o.o.l if you think otherwise. The matter of fact is: kikwete na ccm yake wameshindwa kuongoza, period! It is only a f.o.o.l who can't honestly see that.
 
wengi wetu humu JF ni imani yangu kuwa tumepita shule, idadi ya waliokuwa wanasoma miaka ya 1960-2000 ni ndogo ukilinganisha na alivyoingia JK.

Serikali kipindi hicho iliweza kutoa huduma mbalimbali kwa wanafunzi wa ngazi zote.

Leo hii idadi kubwa inataka huduma zilezile walizokuwa wakipata wanafunzi wa enzi hizo, unatarajia kwa hali hii ubora unaousema wewe utapatikana?

Kama hukuwai kufika katika nchi yeyote iliyoendelea, basi usome hata majarida mbalimbali ya nchi hizo. Mfano, Marekani mpaka leo bado haijaweza kutoa huduma kwa shule za umma na vyuo vyake, kama zinazotolewa na watu binafsi.

Ila mbona atujiulizi hawa wanafunzi wa shule hizo mnazosema sio bora, mbona kuna wanafunzi wanaofanya vizuri? na hata wakifika juu wanaendelea kufanya vizuri?

Binafsi sijawai kupata fursa ya kufaidika kwa kufundishwa na mwalimu darasani kwenye masomo yangu yote. Lakini jitihada binafsi za mwanafunzi zinahitajika katika kufanikisha na kufikia malengo yake.

Hii ndio silaha pekee ya kula keki ya taifa, kupata taaluma na kutumia taaluma kubadilisha hali yako na ya jamii inayokuzunguka.

Badala ya kuilaumu serikali, ambayo kimsingi ni kama muwezeshaji tu, lakini nafasi kubwa ni sisi wazazi na walezi kuwaimiza vijana wetu wazingatie masomo yao.

BADILIKA UBADILI TAIFA.
Umejaribu kujenga hoja lakini kuna mambo huyajui na nadhani ni wajibu wangu kukusaidia ujue ni kwanini watu wanailaumu serikali kwa hali tuliyo nayo.

Moja ni kwamba serikali ndio wenye jukumu la kukusanya kodi kutoka vyanzo mbalimbali,kupanga mipango kwa kadri ya vipaumbele na mahitaji ya jamii,kubana matumizi ikiwa ni pamoja na kutopanua ukubwa wa taasisi zake unnecessarily.

KUPANGA NI KUCHAGUA,Hivi unaweza kusema ni bora kutibu watu wengi kwa kuwapa robo dozi huku ukijua kuwa kufanya hivyo ni kuengeza tatizo?? Kujenga shule 3000 huku unajua hakuna walimu na hata wanafunzi wa kusoma shule hizo ni vigumu kuwapata wenye sifa, je si kupanga mipango vibaya?pili, serikali ndio wakusanyaji kodi za mali zinazobinafsishwa lakini nyingi wanajiuzia wao kwa kulipa fedha kidogo sana,je huko siyo kulihujumu taifa?

Siku hizi ni vigumu sana kupata vjana wenye uwezo wa kuandika kiswahili kwa ufasaha,sababu ni kwamba wamefundishwa chini ya kiwango!! Tutapata wapi akina SHABANI ROBERT WENGINE? Serikali haiwezi kukwepa lawama hata kidogo.
 
Vyovyote utakavyosema ukweli utabakia kuwa ukweli,viongozi wamejijengea utawala usio na tija nakujirundikia mali na fedha isivyo halali. Watanzania walishtakia kwa Mungu na sasa majibu yanaanza kuonekana "Mungu atakaposema NO hakuna wa kusema YES"

Haya ni matamshi ta mtu aliekata tamaa!! Nchi itakombolewa na wale wasiokata tamaa kwani hata maneno katika vitabu vya dini yako wazi kuwa "MUNGU HUWASAIDIA WALE WANAOJISAIDIA". Tafakari na uchukue hatua!!
 
Mkuu unaakili sana na nimependa jinsi ulivyojenga hoja yako hapa.

Tatizo tulilonalo watanzania wengi ni kutojua majukumu ya kila kada. Utawasikia wanalalamika kuwa "serikali imetufikisha hapa kwenye huu umaskini" as if ni jukumu la serikali pekee kupambana na umaskini.

Jiulize wewe hapo ulipo kwa nafasi yako, umepambana vya kutosha kustahili kuilaumu serikali? au na wewe unastahili kulaumiwa na watoto wako?

Jukumu la kulisha, kusomesha na kuangalia kwa kusimamia na kuchunga maadili ya watoto wetu ni ya mzazi au mlezi.

Kama haupo tayari kutoa huduma hizo nilizo orodhesha hapo juu, kaa na ugumu wako utulie, sio kufyatua watoto utarajie waje wapate elimu bure na bora kwa mgongo wa serikali, ambayo kimsingi inapata mapato yake kutoka kwa wafanyakazi, wafanyabiashara, wajasiriamali, wawekezaji na wakulima. Sio wavivu na wazembe kama wewe ambae unatarajia kila kitu ufanyiwe na CCM.

Serikali imefanya mambo mengi makubwa na kwa yeyote mungwana basi hana budi kuipongeza kwa kazi nzuri. Ila kama ilivyo ada, hakuna kilichokamilika chini ya jua, kama kuna mapungufu yamefanywa na serikali, basi kuna namna ya kufanya tathmini na kuiwajibisha kama ipasavyo.Sio huu utaratibu wa kuja kutukana, kukebei, kukashfu na kuelemea upande wa makosa tuuu kwa serikali yetu.

Mimi naona mleta mada kama angekua ni mtu mwenye akili timamu, angeorodhesha ahadi za kikwete, aorodheshe yaliyofanikiwa na ambayo yanaendelea kushughulikiwa, halafu aeleze yaliyoshindikana kabisa.

Hapo ningemwona mungwana, sio huo upuuzi wa kuweka wabunge 3 wa CCM kati ya wabunge zaidi ya 230 wa CCM hapo bungeni, heti tukubaliane nae kuwa HAWAFAI?

Mbona hujakiweka UDOM? chuo cha mandela pale Arusha? takwimu ya kuongezeka kwa vyuo vikuu? idadi ya kuandikishwa wanafunzi shule za msingi? unajua hamasa wamepata wapi? idadi ya wanaoingia sekondari? idadi ya wanaoingia vyuo vikuu? idadi ya wanaopata ajira na wanaojiajiri?

Idadi ya vituo vya afya? utoaji wa huduma ya maji safi na salama? ulinzi na usalama? ongezeko la madaktari? ongezeko la walimu? uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya maji, umeme na barabara+ madaraja? Kutetea na kuzitambua haki ya mwanamkee na watoto? kukomesha mauaji ya vikongwe na albino?, kufuta kabisa ujambazi? Haya yote ni katika kudumisha ulinzi na usalama.

Siku nyingine huyu mleta mada alete na mazuri basi sio kusema tu mheshimiwa rais AMESHINDWA, great thinkers hawawezi kufanya tathmini kirahisi rahisi hivyo, labda uwapelekee hizi picha zako wajinga wenzio.


Mkuu nathamini mchango wako, lakini kidogo niogezee au nikuulize.

Umesema kila kada ina majukumu yake ni kweli, lakini umesahau kitu kimoja mahitaji ya lazima ya mwanadamu (basic humani needs). Mishahara lazima ilenge kukidhi mahitaji hayo ya msingi kinyume chake ni kumuibia mtanzania na dhana unayoiimba ya kujikwamua inabaki kuwa historia kwasababu wafanyakazi wanaibiwa haki yao na hakuna uwezekano wakajiendeleza.

Kwanza unakubaliana na malipo ya 10,000 kwa siku yaani 300,000 kwa mwezi? kama ndivyo kidogo tuutafakali huu mshahara.

-Kodi ya nyumba, vyumba viwili tu 80,000/mwezi
-Umeme 10,000/mwezi
-Maji 5000/mwezi
-Matibabu 20,000/mwezi
-Usafili kwenda kazin na kurudi 600/siku 3000/week, 12000/mwezi
-Mavazi 10,000/mwezi
-Nauli ya watoto 2 shuleni 600/siku 12000/mwezi
-Chakula watu 4 kwa siku 15,000, 450,000/mwezi

Mpaka hapo nikama 500,000/mwezi. (makato ya kodi na michango mbalimbali hatujaijuisha, je? wafanye ujasiliamali kwa mtaji upi nao wanafanya kazi bure wakiibiwa haki yao?)

Maswali yangu kwako mkuu

a) Ili huyu mtu ajikombowe kwa jitihada zake kama ulivyo dai waache kufundisha na kuhudumu (manesi) waende wapi? na kwanini wasilipwe haki stahiki au 300,000/mwezi ndiyo stahiki ya kada zao?

b) Watoto ili wapate elimu bora anatakiwa kuwapeleka shule zenye ada walau 600,000 kwa mwaka afanyaje?

b) umesema mwanafunzi afanye jitihada kujisomea sio lazima walimu katika moja ya post zako, hivi mambo ya differential equations, na vitheory vya Archimedes principles and law of flotation bila mwalimu vitakwenda eti? Ni elimu ipi unayoizungumzia ya bila mwalimu bora na aliyehamasika?


c) Umeorodhesha vituo vya afya, hivi umeishi vijijini ukaona watanzania wanavotaabika na wanavokufa kwenye hivo vituo na dhahanati kwa kukosa tiba? hakuna chochote huko! tuliokulia vijijini tunafahamu.

d) Jaribu kuwa muungwana unaposema idadi ya wanafunzi wanaojiunga vyuo na kada mbalimbali hususani za serikali hebu tuambie ni kwa ubora upi wa wahitimu serikali ijivunie tuipongeze? Taaluma inashuka kila mwaka na huu ni ukweli angalia ubora wa mitihani unaporomoka kila mwaka. Shule hazina maabala wala walimu wakutosha sasa tuipongeze kwa lipi?

e) Je kwa mshahara huo wa laki tatu kwa mwezi unazani afya na elimu vitatupatia ubora tunaoustahili watanzania hasa wa vijijini kwawatoto wetu? Maana Mwalimu na wauuguzi wote wanakwenda na njaa kazini, familia zao hazipati mlo stahiki, elimu duni, mavaz nk


Nina mengi lakini tuanzie hapo, halafu tutaendelea.

Hatusemi hakuna maendeleo, lakini uwiano wa maendeleo ukilinganisha na miaka ya kuwa madarakani ccm, pia raslimali nyingi za nchi yetu ni aibu tena aibu kubwa serikali kutufikisha hapa tulipo.
 
KAMA MNGEKUWA MNAELEWA NCHI INATOKEA WAPI KWENDA WAPI NA STATISTICS WALA USINGELETA MADA HIYO,lete takwmu za idadi ya shule za msingi,sekondari,clinik,vyuo vikuu,pato la taifa,DO YOUR HOMEWORK THEN COME BACK USEME KKWETE HAFAI.kwa hiyo mambo unayoyasoma kwenye magazeti wenzako hao ndio kazi zao hata angie nani lazima aandikwe vibaya, hope wewe s muandishi wa habari?:A S 39:

lete takwimu za idad ya wanafunz wa shule za msingi wanaomaliza shule pasina kujua kusoma,kuandika wala kuhesabu na wanaenda sekondari,,,,,,pia idad ya shule za msingi na sekondari ambazo hazina walimu,madawati ,vitabu na maabara,pia vituo vya afya vina wauguzi???na hospitali zina vifaa tiba??na je rasilimali tulizonazo zinaendana na upuuzi huu???hadi sasa naandika comment hii wagonjwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili wanalala chini,case study ni SEWAHAJI,MWAISELA NA KIBALISA KATIKA WODI NAMBA 17 NA 18,KUHUSU PATO LA TAIFA UNAJIVUNIA NINI IKIWA WATU WANAIBA HELA NA KUFICHA NJE KULIKO ZA BAJETI YA TAIFA LAKO????hapo mtanzania anapaswa vip ku-play his/her part?
And then ukiongelea idad ya vyuo inaendana na ubora wa elim unaopaswa hasa kwenye soko la ajira la sasa????utaratbu gani umeandaliwa wa kutoa fursa za ajira kwa wahitimu???wameweza kupewa nyenzo au mikopo????au tuendelee kujisifia kuwa na vyuo vikuu viiiingi na wahitimu weeengi pasipo ajira????
 
KAMA MNGEKUWA MNAELEWA NCHI INATOKEA WAPI KWENDA WAPI NA STATISTICS WALA USINGELETA MADA HIYO,lete takwmu za idadi ya shule za msingi,sekondari,clinik,vyuo vikuu,pato la taifa,DO YOUR HOMEWORK THEN COME BACK USEME KKWETE HAFAI.kwa hiyo mambo unayoyasoma kwenye magazeti wenzako hao ndio kazi zao hata angie nani lazima aandikwe vibaya, hope wewe s muandishi wa habari?:A S 39:

kinachoulizwa hapa si idadi ys shule au vyuo vingapi, ni ubora wa elimu na maamzi ya kisiasa yasiyoonesha tija. wizi unaofanyika katika shughuli hizo ni mkubwa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya ya viongonzi hawa hazitii matumaini.
 
Haya ni matamshi ta mtu aliekata tamaa!! Nchi itakombolewa na wale wasiokata tamaa kwani hata maneno katika vitabu vya dini yako wazi kuwa "MUNGU HUWASAIDIA WALE WANAOJISAIDIA". Tafakari na uchukue hatua!!

Maendeleo ya nchi hayaletwi na mtu mmoja mmoja na ndio maana uaminifu au ufisadi wa mtu au watu fulani unaathari kwa wengine. Wewe mpaka sasa umechukua hatua gani ambayo imeleta mabadiliko kwenye jamii?
 
KAMA MNGEKUWA MNAELEWA NCHI INATOKEA WAPI KWENDA WAPI NA STATISTICS WALA USINGELETA MADA HIYO,lete takwmu za idadi ya shule za msingi,sekondari,clinik,vyuo vikuu,pato la taifa,DO YOUR HOMEWORK THEN COME BACK USEME KKWETE HAFAI.kwa hiyo mambo unayoyasoma kwenye magazeti wenzako hao ndio kazi zao hata angie nani lazima aandikwe vibaya, hope wewe s muandishi wa habari?:A S 39:

kinachoulizwa hapa si idadi ys shule au vyuo vingapi, ni ubora wa elimu na maamzi ya kisiasa yasiyoonesha tija. wizi unaofanyika katika shughuli hizo ni mkubwa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya ya viongonzi hawa hazitii matumaini.
 
shukrani ya punda.......shule za kata,unajua kubofya cm,unangia mliman city na foleni barabarani kuonyesha maisha bora kwa kila mtz,mpewe nini jmn mpewe nini?awamu ya mwinyi mmelalamika,ya mkapa mkalalamika kwa sana kaja kikwete ndo usiseme,na atakayekuja baada ya kikwete mtamkumbuka kikwete.STOP COMPLAINING ABOUT UR COUNTRY YOU FO********........... JUST DO YOUR PART WELL:tape2:
. Naogopa kusema!! Ila mh ngoja nipite.
 
Hi, jamii forums!
Kwa hili naogopa kusema au labda macho yangu hayaniambii ukweli kuhusu yule jamaa alielala pale!! Namwona vizuri kweli??
 
Hi, jamii forums!
Kwa hili naogopa kusema au labda macho yangu hayaniambii ukweli kuhusu yule jamaa alielala pale!! Namwona vizuri kweli??

yupi mkuu? Wahasira, mkombamboga au msitisha ukweli wa poormond?
 
hakuna mtoto anayezaliwa akijua kutembea bwana mkubwa.mvumbuzi wa jenereta alpata upinzani mkubwa wakati anazindua jenereta kutoka kwa watu wenye mawazo kama ninyi,kama unabisha nikuletee toleo la kwanza la kompyuta za ibm,THINK BIG
 
Ndugu wananchi kama mnakumbuka wakati tunakabidhiwa nchi hali ilivyokuwa,mwaka 2008 had 2010 kukatokea tetemeko la uchumi,lakn tuliweza kuhimili misukosuko,na takwimu za mwezi wa nane mwaka huu tumeweza wote kuckia ktk ripoti ya bot kuwa kwa mara ya kwanza tembelea link hyo http://www.mwananchi.co.tz/news/51-...ikali-yakusanya-mapato-zaidi-ya-matumizi.html kwa hyo ndugu wananchi naomba tumpe moyo na nafasi kiongozi wetu na rais mteule mh. j k aliendelezze gurudumu la taifa. MUNGU IBARIKI AFRICA,MUNGU IBARIKI TANZANIA,
 
Back
Top Bottom