Magamba - Mbozi utafiti wa makaa unapopitilza na kuwa uchimbaji wa makaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magamba - Mbozi utafiti wa makaa unapopitilza na kuwa uchimbaji wa makaa!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Aug 31, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Madiwani walia na kampuni ya Jenerali Robert Mboma
  Na Thobias Mwanakatwe
  31st August 2011

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile
  Mzimu wa kuiandama Wizara ya Nishati na Madini umeendeleabaada ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeyakumbana Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, wakimtaka atoe maelezo nikwanini kampuni ya Troll Mining inafanya kazi ya kuchimba makaa ya mawe katikakijiji cha Magamba wilayani hapa bila ya kuwa na leseni wakati wanafahamuilipewa leseni ya kufanya utafiti na siyo ya uchimbaji.
  Kampuni hiyo inamilikiwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali Robert Mboma, pamoja na wabia wengine wawili kutoka Norway naUjerumani ambao ni Erling Johan na Rolf Giesing.
  Madiwani hao walimbana Mwakipesile wakati wa kikao maalumcha baraza hilocha kupitia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serika (CAG)kilichofanyika jana mjini hapa.
  Walisema wanafahamu kuwa kampuni hiyo ilipewa kazi yakufanya utafiti wa makaa ya mawe katika kijiji hicho tangu mwaka 2005, lakinikatika hali ya kushangaza inafanya kazi ya kuchimba na kusafirisha makaa hayoya mawe.
  Mboma, akizungumza na NIPASHE kwa simu, alisema madiwaniwanachokisema ni majungu kwa sababu hawajui sheria ya madini na kwambawanachotakiwa kukifanya ni kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.
  “Madiwani wafikirie udiwani wa wananchi na sio kujadilimambo ya madini kazi ambayo inafanywa na wizara. Kimsingi hakuna sheriailiyovunjwa na kampuni ya Troll Mining,” alisema Mboma.

  Diwani wa Kata ya Halungu (CCM), Samson Simkoko, alihoji kama Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi inahitaji kuongezamakusanyo ya ndani ni lazima sheria ya madini iangaliwe upya kwani kuna kampuniambazo zimekuwa zikifanya uchimbaji bila kulipa chochote kwa halmashauri.
  “Mheshimiwa Mwenyekiti (Mkuu wa Mkoa wa Mbeya) kampuni yaTroll Mining ilikuja kufanya utafiti wa makaa ya mawe au kuchimba? Maana kwamuda mrefu tumeshuhudia shughuli zikiendelea bila kupata maelezo yeyote kutokaserikalini na halmashauri yetu haipati kitu,”alisema Simkoko ambaye alikuwaakichangia hoja ya makusanyo ya mapato ya madini.

  Kufuatia maelezo ya diwani huyo, Mwakipesile alijibu kwa kifupi kuwaanachofahamu ni kwamba kampuni hiyo ilipewa leseni kwa ajili ya kufanya utafitina kwamba tayari kuna mazungumzo ya kampuni moja inayotaka kuwekeza kutoka India ambayohata hivyo, hakuitaja.

  Majibu hayo ya Mwakipesile yalimfanya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya yaMbozi, Erick Ambakisye, kutoa ufafanuzi kwamba madiwani wanahoji suala hilo kwa sababu kunautata juu ya utafiti wa makaa ya mawe unaofanywa na kampuni hiyo kwa kuwaumechukua muda mrefu huku ikionekana shehena kubwa ikichukuliwa na kupelekwakusikojulikana.

  Mwakipesile alimjibu Ambakisye kuwa tatizo lililopo ni kwamba sheria ya madiniimekuwa na matatizo na ndiyo maana serikali imeamua kuzipitia upya sheria zoteza madini na baadaye zitakuwa na majibu mazuri ambayo yataziwezesha halmashaurikunufaika kwa kupata kodi kupitia sekta ya madini tofauti na ilivyo sasa.
  Mapema Septemba 2008, Kamshina wa Madini nchini, Dk. PeterKafumu, aliagiza kampuni ya Troll Mining inayochimba mkaa wa mawe katika kijijicha Magamba wilayani Mbozi, mkoani Mbeya kusimamisha uchimbaji huo hadiitakapokata leseni ya uchimbaji.
  Dk. Kafumu ambaye alizungumza na waandishi wa habari jijiniDar es Salaam, alisema kuwa kampuni ya Troll Mining ilipewa leseni ya utafitimwaka 2005 yenye namba PL 3423/2005 ambayo iliisha muda wake na ilihuishwaJulai 24, mwaka 2008.
  Naye Ofisa wa Madini wa Kanda kipindi hicho, MhandisiBenjamin Mchwampaka, alieleza kuwa kampuni ya Troll Mining iliomba kuchimbamakaa ya mawe tani 16,600 za majaribio ili kupeleka kwa kampuni za MbeyaCement, Mbeya Textiles, SPM Mgololo, Tanga Cement, Bamburi Cement (Kenya) naFGX Septech (China).
  Pia Julai mwaka 2008, Mwakipesile alipotembelea mgodi huo wamakaa alipewa taarifa ya kazi zinazofanyika mgodini hapo na kuelezwa kuwa makaahayo yanachibwa kwa sururu na chepe kwa ajili ya vitofali vya kutumika kwamajiko ya mkaa na “kidogo” kwa ajili ya majaribio katika kiwanda cha sarujiMbeya.
  Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa katika mgodi huo ilibainikakuwepo chombo kimoja kinachoitwa “Excavator” kinachotumika kuchimba na siyosururu; mashine za JCB backhole loader (2) na JCB Wheel Loader na si chepe kama alivyoambiwa Mwakipesile.
  Ubora wa makaa ya mawe unaopatikana katika machimbo hayoulishathibitishwa kuwa unafaa kuwa chanzo cha nishati ya uzalishaji sarujitangu mwaka 1934.
  Machimbo haya yenye hazina ipatayo tani 52 milioni za mkaawa mawe, yanapakana na katika kijiji cha Galula, Wilaya ya Chunya.

  Source:NIPASHE 31 AUG
  Naona kuna haja ya kuwapa kibari ili waanze rasmi uchimbaji ili ivyo viwanda tajwa apo juu wapunguze gharama za uzalishaji na hatimae kupunguza bei ya bizaa
   
 2. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  ha ha ha mbomaaa
   
Loading...