Magafuli mbumbumbu? Foleni ya leo Morogoro Road | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magafuli mbumbumbu? Foleni ya leo Morogoro Road

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Mar 3, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Leo kuna lori moja liliharibika opposite na kituo cha daladala Mbezi mwisho kutokea usiku. Lori hilo limesababsiha foleni kubwa sana, kutokea Kibamba foleni iifika Makondekona kutokea mjini foleni ilifika Stop Over wakati napita na pikipiki.

  Ibara ya 9 (1-10) za Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 zilizopitishwa kwa Tangazo la Serikali Namba 21 la Tar 23 Januari 2009 zinazip mamalak TANROAD ya kuondoa magaro yoyote yaliyoharibika na kakaa barabara kwa zaidi ya masaa 6 mijini na masaa 24 vijijini.

  Wakati magari yanayoharibika na kutelekezwa barabarani yakiendelea kusababisha ajali, vifo, majeruhi na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara kama ilivyotokea leo asubuhi Morogoro road, Mhe John Magufuli anaendelea kudai kuwa mabango ya biashara yaliyowekwa katika hifadhi za barabara ndio kero namba moja katika barabara zetu na kwa kutumia ibara ya 32 ya Kanuni zilizotajwa hapo juu kuiagiza na kuisimamia TANROAD kuyawekea alama ya X na kuyaondoa mara moja.

  Hii kati ya mabango ya matangazo yaliyoko katika Road Reserve na magari yanayoharibika na kutelekezwa barabara ni kwa masaa na hata siku kadhaa ni kipi ni kero zaidi kwa watumiaji wa barabara? Mbona hatumuoni Mhe Joihn Magufuli kuisimamia TANROAD kutumia fedha za mfuko wa barabara kununua breakdowns za kuweza kuondoa magaro ya aina hii?

  Au kwa Magufuli sheria zinapaswa kutumika pale ubomoaji wa aina fulani unapohusika k.m kuondoa mabango ya matangazo, kubomoa jengo la TANRSCO n.k, na kwingineko sheria kuwekwa kapuni hata kama suala hilo li kero kubwa na husababisha ajali, vifo, majeruhi na usumbfu kwa watumiaji wa barabara. Toka lini sheria zikageuka kuwa kama "MENU" katika migahawa ambapo mlaji huchagua chakula akipendacho na kuacha asichopendea?
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Nimtendaji wa Media anapenda coverage!!Hivyo tutaendelea kuumizwa na foleni!!
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Je ulitoa taarifa yoyote kwa vyombo husika ili gari hilo litolewe au ndio ulipita na kuja hapa kulisemea na unasubiri Magufuli aende akalitoe?

  Bila kushirikiana kazi wala maendeleo tuyatakayo hayawezi kuja,kutegemea mtu mmoja kufanya yote wakati wote tunawajibika katika kufanikisha mambo mbalimbali yanayohusu nchi yetu ni jambo linalozidi kuturudisha nyuma.
   
 4. H

  Hume JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Kweli watanzania ni kiboko, yaani umetumia akili zako zoooooote ukaona kazi ya kuondoa magari yaliyoharibikia barabarani ni ya waziri?
   
 5. d

  deecharity JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 831
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  hapana nat m2 wa media, jiulizeni hyo gari imetolewa taarifa? Ishu ya mabango jaman kubalini hakuna nch inayotaka maendleo bila baadh ya hasara kwa wananch kuwakuta mtake mstake.
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Wanaopaswa kulaumiwa ni jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani ambao kwa mujibu wa sheria uliyotoa ndiyo wasimamizi wa sheria hiyo na ndiyo wanaopaswa kuchukua hatua. Hivyo sioni hapa kama magufuli anahusika aidha ni vizuri hao wasimamizi wa hizi sheria kuchukuwa hatua mapema kuliko kungoja viongozi wakisiasa watoe matamko.
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Bwana Jatropha,
  Naona tangu jana (nikiwa visitor) unamshambulia sana Dr Magufuli,una suala binafsi naye au ni itikadi? Ingekuwa vema kama ungeishauiri au kuishambulia serikali kuliko yeye kama mtu binafsi kwa kuwa naamini hayuko peke yake katika maamuzi yake...na kwa hili la foleni ya leo katu si wajibu wake pamoja na mapungufu yake.
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kuharibika kwa gari barabarani na kuondoa mabango kwenye road reserve vina uhusiano gani?
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kama walio yaweka mabango hawakufuata taratibu si vibaya kuyaondoa...ile Coco Beach imeharibiwa sana na mabango haya
   
 10. K

  Kijunjwe Senior Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh! Kuna kitu hapa Jatropha,
  Sasa huyu Magufuli atakuwa sehemu ngapi za barabara za nchi hii? natumai jibu lako ni hawezi kuwa kila sehemu? Sasa kwa kuwa hawezi kuwa kila sehemu umesaidiaje basi kwa wale wasaidizi wake kujua kuwa huko kwenu kuna tatizo? Kama hujafanya jitihada zozote na umekimbilia hapa kuja kutoa lawama lazima utakuwa na matatizo ya kufikiri na hasa katika utambuzi wa vina vya matatizo yanayokuzunguka? Kama ndivyo, basi jifunze kuwa focused hasa unajaribu kutatua mambo yanayokukwaza.
   
 11. H

  Haika JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Namuunga sana mkono Magufuli kwa kufanya MAAMUZI magumu. Wote/wengi wanakereka sana kwa mtikisiko wa kuingia kwake wizara hii ngumu, lakini hebu rudi nyuma kidogo tu, je anavunja sheria ipi??
  Halafu jiulize, je hao waliokubali kuweka hayo mabango hapo walijua kuna hio sheria? waliikubali? walishatoa malalamiko ibadilishwe???
  Je MAgufuli angekaa tu ofisini asifanye kazi zake zilizo kwenye mpango kazi kwa kuogopa hayo???

  Jamani tujipe moyo, tujifunze kufanya kazi tuliopewa sio kutafuta shorcuts, kama hizi za vipato vya mabango kwy road reserve (kama si sheria)

  Binafsi hahisi baada ya foleni kupungua tutamshukuru huyu baba, lakini sasa, mmmmhhh!!!
   
 12. M

  Mwana Apollo New Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ulifanya jitihada gani kuwajulisha wahusika ili waweze kushughulikia hilo tatizo?. Na kama ulifanya hivyo, ulihakikisha ni masaa sita yamepita toka ulitoa taarifa hizo?.Acha kukurupuka na kutumia akili yako yote kuandika kitu usichokua na uhakika nacho, Magufuri anapiga kazi mwache aendelee na ujue kwamba wizara yake ina watumishi zaidi ya 200 au una sababu zako?????
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  1 - Magufuli ndiye TANROADS?
  2- Anaishi mbezi luis kiasi kwamba ikitokea lori nimezuia barabara aende kuliondoa au afahamu automatically kimiujiza bila kujulishwa?
  3-kazi ya waziri wa ujenzi ni kufuatilia hata malori yaliyoharibika barabarani?
   
 14. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Me naona mtoa mada wa thread hii ndio mbumbumbu asiyejielewa kuwa ni mbumbumbu. Kashindwa kutofautisha kazi za tanroads na waziri. Na hajui magufuri ni waziri anayefanya kazi nchi nzima sio dar tu na si kila barabara zipo chini yake. Km unakumbuka tatizo la mabango kuna barabara hayajatolewa sababu hazipo chini yake. Hivi kila mkoa, kila barabara likitokea hilo tatizo inabid magufuri aende? Acha pumba zako we jotropha.
   
 15. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ....i think otherwise!!!!
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Soma thread yangi vizuri, "Mbona hatumuoni Mhe Joihn Magufuli kuisimamia TANROAD kutumia fedha za mfuko wa barabara kununua breakdowns za kuweza kuondoa magari ya aina hii" Au utendaji wake na kufuata sheria ni pale katika kuboma kile kilichokwisha jengwa?
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  nafahamu sana kazi za waziri ndio maana nimetaja ni vifungu vya sheria alivyodai kutumia kuondoa mabango ya matangazo na poia vifungu vya sheria anavyopasa kutumia kuisimamia tanroad itumie fedha za mfuko wa barabara kununua breakdowns za kuondoa magari yaliyoteleekzwa barabarani. Ndio maana nauliza sheria kwa magufuli ni zeli zinzzohusu kubomoa tano, mabango ya matangazo n.k
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kwakuwa magari yanayoharibika na kutekezwa barabara ni mengi na husababisha ajali, vifo na majeruhi karibu kila siku ndio maana nataka waziri magaufuli kama anavyochachamaa wakati wa kubomoa mali za wananchi awachachamalie tanroad watekeleze kanuni za sheria walizojitungi wenyewe wanunue breakdowns za kuondoa magaro hayo ili kunusuru maisha na mali za wananchi
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Anold Sheria ni ya Barabara namba 13 ya 2007 na Knuni zimetungwa na Waziri wa Ujenzi Jeshi la Polisi linaingia vii wakati katika Kanuni wamesema "The Road Authority shall after cause to be towed" hapo road authority ni nani kama sio TANROAD?
   
 20. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Haya bana amesikia maoni yako,atashughulikia ila kwa sasa ana-deal na ubomoaji wa mabango na jengo la tanesko.
   
Loading...