Magadi tuyachimbe?

Kidzogolae

Senior Member
Apr 20, 2008
133
2
kama hicho kiwanda kitasaidia wananchi, wanaohangaika wanatamani tu hata hao flamingo wangekuwa karibu wawakamate wawachinje walau wale nyama tu manake maisha magumu, sioni kama kuna umuhimu wowote wa kutuzuia tusijenge icho kiwanda kama kitaleta walau contribution fulani kwa nchi yetu. najua ni muhimu kuweka maliasili ili zije zisaidie vizazi vya baadae, lakini,simba akizidiwa hula hadi majani. na mtu akizidiwa,huwa yuko tayari hata kama atapata hasara kubwa,alimradi amefanikisha alichokuwa anakitaka. watu wengi wanaolalama kwenye suala hili ni wakenya, watu ambao huwa wanaona wivu mno,wanatuoneaga wivu watz. siku zote kenya ilishajihesabia kuwa wao wako juu kuliko tz. wakiona watz wanakuja juu huwa hawalali kabisa. wao wamefanya mradi kama huu wa magadi, wamafaidika sana na wanatuuzia sisi wenyewe magadi tena kwa garama. wanafaidika. kwanini sisi tusifanye hivyo? kwanini wanalalama sana. kuna siku nilikuwa Nairobi,nilifungulia moja ya tv zao,nusu nipasue kwa ngumi. Mimi nafikiri, kama kuna madhara machache tu,tuusapoti tu huo mradi.

kama tulifanya vibaya tukamaliza vizazi vya vifaru wanaoshika mimba kwa muda wa miaka mitano...kuna hasara gani bwana, kwani hao vifaru tunawala nyama? utalii wenyewe unatuingizia hela kidogo tu,na vijisenti vyenyewe vinaliwa na wachache. kama kuna madini hata kama leo tukiyaona katikati ya serengeti,kama yataleta ugali kwa wananchi wetu, tufanyage tu. mtindo wa kusema sisi tujitese kwasasaivi ili vizazi vya baadae vije viburidike, hio haipo. wao watakuja kutafutaga altenatives zao wenyewe kulingana na muda wao. NAOMBA HUO MRADI WA MAGADI UENDELEE. kama tunamaliza flamingo, basi,tutakula magadi....
NB:naomba msinirushie makombora makubwa mno. najua how u r going to react.hahaha
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom