William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Mkuu,
"Tumelilia Demokrasia tukapewa....." Hivi Demokrasia ni nini katika kufahamu kwako? Au kukubaliwa kwa mfumo wa vyama vingi kwa mbinu za kuuridhisha ulimwengu kwa kiini macho, kwako wewe ndio Demokrasia?
Hatamu za nchi, kwa maneno ya Mzee Julius Nyerere na kwa vitendo zilishikwa na bado zinaendelea kushikwa na CCM. Rais ndio Mwenyekiti wa CCM. Kukaa kwake kitini ni kwa ridhaa ya CCM. Naye ataendelea kwa hali na mali kuipendele
a CCM kwa kuwa ndio nguzo yake.
Unavyofikiri wewe huyo akiwa ndiye mwenye kuichagua tume ya uchaguzi, tunaweza kweli kuwa na tume huru? Uchaguzi ulio huru unajikita katika tume huru. Kimsingi Demokrasia ya kweli inategemea sana kiwanja sawa cha ushindani wa vyama vya kisiasa, ambao kwa hivi sasa hatuna.
Katika nchi yoyote iliyohuru, hatamu za nchi hushikwa na wananchi wenyewe na sio kushikiwa na chama chochote cha siasa. Na hatamu hizo zimo katika kuwawezesha wananchi kuwaweka viongozi madarakani na kuwaondoa hali kadhalika. Mtindo tulionao hauwawezeshi wananchi kuwaweka wala kuwaondoa. Uwezo huo ni wa CCM peke yake.
Je, hiyo ndio Demokrasi tuliyolilia na tuliyopewa?
Kama tuna Demokrasi kweli iweje leo hii tuna Katiba ile ile ya Chama kimoja iliyojaa viraka? Iweje mwananchi asiyekuwa mwanachama wa chama chochote
anyimwe haki yake ya msingi ya kugombea uongozi katika nchi yake mwenyewe? Iweje wakati wa kampeni na uchaguzi washindani watembezewe mkong'oto wao peke yao?
Che Nkapa akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM aisema hadharani kuwa atahakikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu hata kwa kutumia vyombo vya dola. Naam, sote tuliushuhudia "ushindi wa tsunami na ushindi wa kishindo."
Je, hiyo ndio Demokrasi tuliyolilia na tuliyopewa?
Unalalamika kutembezewa chuki, nasi tunadai tutandaziwe haki na ukweli. Mizengwe ikizidi, wenyewe mnaita "wembe ule ule" na chuki haitakosekana.
Huwezi kucheza mpira na wakati huo huo kuwa mwamuzi ukategemea timu unayocheza nayo kushinda. Halafu unatuhimiza tujiunge na vyama vingine. Tukafanye nini kama si kuwa wasindikizaji tu? Au unatusanifu?
Ukumbuke tu kuwa hata Himaya ya Roma ilitoweka.
- Kwanza punguza jazba kwa sababu mimi sio rais wa jamhuri wala kiongozi wa jamhuri licha ya chama chochote cha siasa, ila ninasaidia kuongoza NGO ya kuwasaidia watoto wasiojiweza kwenda kupata elimu, that is all.
- Kwamba ninalilia anything hapana, ila ninatoa mawazo yangu, ambayo ni clear kuwa yako tofauti na yako, naona una vitisho vingi sana lakini mimi I have nothing to with anything, kwa hiyo jaribu kuheshimu haki yangu ya kuchangia mada hapa JF na sio lazima niwe na mawazo kama yako.
- Simjui mwananchi yoyote wa Tanzania aliyelazimishwa kwa bunduki kukubali demokraisa uchwara tuliyonayo sasa, kulifanyika makubaliano kati ya the then watawala na wawakilishi wetu wananchi kutoka upinzani, makubaliano yalifanyika yakatiwa saini na wahusika wote pale Ikulu na picha ninazo, mmoja wa waliosaini ni baba mkwe wangu kwa hiyo ninaelewa vizuri sana what happened na what did not, hakuwahi kuniambia kwamba waliwekewa bunduki kukubali, ila alikubali makosa katika haraka zao za kukubali yale makubaliano, ambayo sasa hivi wengi hapa JF hatuyapendi, lakini sio taifa zima la Tanzania.
- Unaonekana una some complex maana unajaribu kunitisha na maneno mengi hewa why? Kwa sababu mawazo yangu yako kushoto na yako au una mengine mkuu? I mean umesema maneno mengi sana ambayo mimi nikiwa mwananchi kama wewe hayanihusu kabisa, vipi mkuu are you okay maana ya Roma yanatoka wapi? Samahani mimi sio mkazi wa huko Roma ila ninatoka Dodoma?
Ahsante
william.