Mag3 nasubiri kuona nchi inayumba kama itayumbishwa !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mag3 nasubiri kuona nchi inayumba kama itayumbishwa !!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Apr 1, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Mwanzoni kabisa tulionywa kuwa mafisadi wana nguvu kubwa na wakikamatwa tu, nchi itayumba. Akakamatwa Jeetu Patel na washiriki wenzake, nchi haikuyumba. Kafuatia Maranda na washiriki wenzake, nchi haikuyumba. Mramba na Yona wakapelekwa Keko, serikali hata haikutikisika. Kafuatia Liyumba na msaidizi wake, hata kutetereka serikali haikutetereka.

  Mag3 bado ninasubiri kumwona hili lisilokamatika/hao wasiokamatika ambao wakiguswa tu serikali na nchi nzima ya TZ itawaka moto. Kama hii itatokea kesho, wiki ijayo, mwezi ujao au hata mwaka ujao, kama kawaida yao watanzania wengi naungana nao kuisubiri hii siku - siku ambayo tutatakiwa kujikunyata kwa hofu ya balaa itakayoishukia nchi yangu Tanzania.

  Ni siku ambayo tutamfahamu mbaya wetu, tutamwona kwa sura yake halisi, tutamsikia anavyotema cheche kinywani na tutashuhudia atakavyowashukia wale wote waliothubutu kumnyooshea kidole. Siku hiyo zimwi letu linalotutafuna taratibu litajitokeza wazi wazi na masikini Mag3 na wenye mawazo kama yake watatakiwa kutafuta pa kujificha wasipaone.

  Siku hiyo tutawatambua bila shaka wale wote waliojificha kivulini mwake na ambao wamemwezesha kulala mlango wazi bila wasiwasi wakimlinda 24/7. Wengine tunao humu humu na hawatakuwa na haja tena ya kuficha majina yao tena - watatembela vifua mbele wakitudhihaki kwa vijembe, tuliwaonya na hamkusikia, sasa mtaonja machungu ya jeuri yenu.

  Pamoja na hayo yote naisubiri kwa hamu siku hiyo - kwa sababu licha ya nguvu za adui, ni siku wanyonge watajikomboa. Ni siku ghadhabu na hasira ambazo zimewajaa wazalendo hazitaweza kuzimwa hata kwa vifaru na tutasimama imara kutetea kilicho chetu. Silaha yetu kubwa itakuwa ni kiu ya haki na usawa, kiu ya maendeleo na kiu ya maisha bora - ole wao!!
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu mi nafikiri hapa unafanyika mchezo wa kuigiza. Inawezekana wakulu wanaka mezani na kukubaliana kuwa mkuu kesho tutakukamata na kukufikisha mahakamani ili jamii ione tunashughurika na ufisadi then tutayamaliza. Nafikilia hivi nikiangalia mchakato mzima wakuwakamata, dhamana walizotoa, na kinachoendelea sasa.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,451
  Likes Received: 81,691
  Trophy Points: 280
  Naam bm21, hicho ndicho kinachofanyika. Zile kesi za mafisadi wa EPA na fisadi Mramba na Yona zitapigwa kalenda mpaka baada ya uchaguzi wa 2010 baada ya hapo tutaambiwa kwamba hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwatia watuhumiwa hatiani hivyo wote wataachiwa huru na mafisadi watakuwa wanakenua mpaka gego la mwisho. Kama Kikwete angekuwa na nia ya kweli ya kupambanan na mafisadi basi angeamuru kesi hizo ziendeshwe kwa siku 5 au 6 kwa siku ili zimalizike haraka, lakini ni usanii mtupu wa kuwakingia vifua mafisadi.
   
 4. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Punguzeni majungu na uzushi, toeni solutions sio kutuchonganisha wananchi na serikali yetu, kuna wananchi mnaonekana mngependa kuwona taifa letu linakuwa kama Rwanda, kila kukicha ni ku-preach chuki tu hapa solutions hakuna, hili ni taifa la ki-demokrasia sasa, jiungeni na vyama vya siasa mtusaidie taifa uchaguzi umekaribia, hizi tabiri kama za Sheikh Yahya hazina nafais tena kwenye demokrasia kama tuliyonayo.

  - Tulilia demokrasia tukapewa sasa tuitumie kushiriki siasa ya taifa letu, sio ku-preach chuki kila kukicha wengine mnaonekana mnatoka Rwanda sijui, I mean hamuwezi mkaongea conctructive ila kupandikiza chuki tu katika jamii.

  - Rais amewateuwa watendaji wa sheria, sheria tunazo sasa kama huridhiki na mamuzi ya serikali on sheria basi nenda ufungue kesi against serikali, mbona kina familia za kina Kombe waliishitaki serikali na kuishinda? Mara ngapi Mtikila ameishinda serikali mahakamani? Wakuu punguzeni kuhubiri chuki katika jamii tumieni demokrasia tuliyonayo kwa sababu mifano ipo kwamba it works!


  William.
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Babu kwa busara zako na trend ya chama chako walai wakitangaza mabadiliko ya wakuu wa wilaya 2011 haukosi. This time ilibaki kidogo sana na wakina mwanakijiji na halisi wamekuharibia

  Babu hebu nieleze hivi wewe na huyu jamaa anijiita humu FS ES ni ndugu? samahani kwa kukuuliza hili swali kwani ninataka nijue kama na mi mi nina kipaji cha utambuzi kwani mawazo yenu yamefanana sana
   
 6. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Du, kurudi kundini kunataka moyo....

  Hata hivyo napenda kukusahihisha katika madai yako kuwa tulilia Demokrasia tukapewa. Ukweli ni kuwa hadi sasa bado hatujapewa Demokrasia. Tulichopewa hadi sasa ni mfumo wa ushindani wa vyama vingi na hiyo ni moja ya hatua alfu za kupata demokrasia.

  Pia wanaoleta chuki ni wale wanaotumia hali ya amani na umoja wetu kuwadhulumu ama kuwalinda wanaowadhulumu watanzania maisha bora kama yale wanayoishi wao (wanaudhulumu na walindao dhuluma) pamoja na vizazi vyao. Kitendo cha wenye nguvu kisiasa kwa kushirikiana na wenye nguvu kiuchumi kuwanyonya, kuwalaghai na hata kuwadhihaki wasio na nguvu kisiasa na kiuchumi ndio haswa kinachogombanisha wananchi na serikali yao

  omarilyas
   
  Last edited: Apr 1, 2009
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhh yaani wana create Soaps with several season na episode nyingiiiii, hii nchi wameigeuza michezo ya kuigiza, walichosahau ni kwamba huko vijijini w2 washaanza kuona ulimwengu thanx 2 generators na dishes, kule Bwasi Musoma vijijini wanaona Manu wakicheza live, sasa tutawadanganya nini? wakierevuka patachimbika, kama watawala wetu hawabadiliki na kuacha kutufanya majuha bin maamuma we r going to be worse than Rwandase. Mungu atuhurumie.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Lowasa siku alipotangaza kujiuzulu kule Bungeni, nchi ilitikisika kidogo. Bunge liliyumba kabisa. Serikali iliduwaa kwa muda.
   
 9. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  nilikua siamini kama nchi itayumba lakini sasa hivi niamini nchi itayumba, kwa ajili hamna fisadi aliyokamatwa mpaka sasa hivi, watu humu ndani mnaona michezo ya kuigiza halafu mnasema mafisadi wamekamatwa.
  watanzania mnaambiwa HR MANAGER (LIYUMBA), project manager (KWEKA), NA marehemu(BALALI), Wanaweza kuchukua $200m bila idhini ya board of directors mnaamini (HAMNA KITU KAMA HICHO DUNIANI ACHENI UPUMBAVU).

  "MAFISADI WAKIKAMATWA NCHI ITAYUMBA = KWELI"
  HICHI NI KITENDAWILI NA JIBU LAKE HILO HAPO CHINI, UMIZENI VICHWA KIDOGO WACHENI UVIVU WA KUFIKIRI.
  JIBU = ITABIDI UMKAMATE JK NA BWM, ALAFU UITISHE UCHAGUZI MKUU GHAFLA, HELA ZA MATAYARISHO YA UCHAGUZI NA MAKOROKORO KIBAO  KITENDAWILI KINGINE

  KAGODA IMESHINDIKANA
  JIBU = .......
   
 10. s

  skelleton Member

  #10
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thieti wanathema bwana mkubwa ana kithathi na liyumba kwa thababu ya d.....,
   
 11. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Ni afadhali ya RWANDA ya sasa kuliko Tanzania iliyojaa mafisadi umeona hao Rwanda wanavyosonga mbele
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Kama kweli una nia njema na taifa lako, anza kwa kuyataja hayo unayoyaita majungu na uzushi. Kumbuka kwamba solution haiwezi kupatikana mpaka kwanza uyaone, uyatambue na uyakubali matatizo yanayolikabili taifa. As long as wapo watu aina yako, ambao hawako tayari kuita koleo kwa jina lake halisi, safari yetu kuelekea maisha bora ni ngumu. Ili uweze kutibu ugonjwa ni lazima kwanza baada ya kujua kiini chake ukubali matibabu.

  Kama kuna wanaolipeleka taifa letu pabaya kwa kulea na kujenga chuki ni hao tuliowaweka madarakani. Chuki itakosekana vipi kama mkuu wa polisi anaogopa kukamata wezi na wahalifu kwa kuogopa nguvu yao. Chuki itakosaje kama Waziri Mkuu anataka mhalifu aachiwe asishtakiwe kwa kuwa ni diwani wa CCM. Chuki itakosekana vipi kama pesa hazipo za kukopesha vijana wapate elimu kwa sababu wezi wanaokomba mali zetu, wanaonekana wako juu ya sheria.

  Kama hili taifa ni la kidemokrasia basi Tanzania tunayo demokrasia ya kwetu peke yetu ambayo haina mfano duniani. Demokrasia haiwezi kustawi kwenye utawala usiojali haki na usawa mbele ya sheria. Demokrasia haiwezi kusitawi ndani ya katiba inayotoa mwanya kwa kikundi kwenye jamii kupata upendeleo mbele ya haki na sheria. Demokrasia haiwezi kuwepo kama viongozi wanapatikana baada ya chaguzi zenye sheria zisizotoa uwanja sawa kwa wagombea na zilizogubikwa na rushwa, wizi na upendeleo.

  Ni nani huyo aliyeihodhi demokrasia mpaka ikabidi muililie nyie na akina nani. Kwa miaka nenda rudi tumetoa mawazo very constructive - hasa namna ya kuboresha mfumo wa demokrasia ya kweli. Wasioitakia mema nchi hii kila mara wamebeza juhudi zetu kwa kutuita waroho wa madaraka - eti mroho ni yule ambaye hana na si yule ambaye anacho na ameatamia hataki mwingine apate. Kama hujui anayejenga chuki hapa, jiulize mapinduzi duniani siku zote yanasababishwa na nini ?

  Unasema mwenyewe Raisi kateua watendaji wa sheria halafu hapo hapo unashauri raia afungue kesi dhidi ya serikali. Leo unataka kutushawishi kuwa tukifungua kesi dhidi ya Raisi na mafisadi aliowateua ambao ndio hao hao watendaji wa sheria, haki itapatikana - na mfano unaoutoa ni kesi ya Marehemu Kombe ! Nakuomba upitie posts za nyuma humu ndani JF kuhusu kesi ya Kombe, utaweza kuelimika kuhusu kwa vipi iliendeshwa.

  Mara ngapi Mtikila ameshinda ndio lakini mara ngapi serikali imetumia jeuri yake kudharau maamuzi ya mahakama. Rejea hukumu iliyowahi kutolewa na Marehemu Jaji Lugakingira au hata mapendekezo yaliyotolewa na tume ya Marehemu Jaji Nyalali. Ukitaka kujua jeuri ya serikali ya Tanzania, jaribu kushitaki CCM iliyopora mali za Watanzania na kuziita zake mchana kweupee!

  Kaazi kweli kweli !!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mag3 maneno mazito, mwenye masikio na asikie!
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ukija kivingine unaongea hili ukija na hivi unalonga lile.....wewe jiandae tu na 2010
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Ni kwa sababu sikuwekeza kwa kwenye kampuni ya Mwakyembe, labda ndio maana nimekosa u-DC, maana nasikia waliowekza wote huko wanasubiri u-DC, akipata urais.

  William.
   
 16. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #16
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Demokrasia sio ruzuku au kulilia ruzuku tu kutoka serikali kuu ya CCM, kama tulivyofikiri mwanzoni, sasa tuwaombe watawala wakubali tukae chini tuanze upya na tukubali kwamba tuliporukia Demokrasia siku ile pale Ikulu, na kina Mtei kukubali kusaini makaratasi ya kuanzishwa kwa vyama vingi, tulikurupuka sasa we have come to our senses, na kuelewa kwamba demokrasia sio ruzuku peke yake kama tulivyodhani.

  William.
   
 17. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #17
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Wanasonga mbele kwa kulipia kodi mfukoni mwa Kagame, kwa kulipia hata hata kuku wa kufuga nyumbani, are you ready for that?

  William.
   
  Last edited: Apr 2, 2009
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  1.
  - Nasubiri Kuona nchi inayumba kama itatumbishwa.

  2.
  - Ni pamoja na sisi wananchi wote wa Tanzania kukubali kwamba we are all responsible for where we are now as a nation, badala ya kushmabulia wengine kila kukicha wakati matatizo mengi ni sisi wenyewe wananchi tunayachangia.

  3.
  - Ni maneno yanayokupatia temporary fame hapa JF, lakini hayana msaada wowote kwa taifa na wananci wake, kwa sababu sio lazima wote hapa tuimbe wimbo wako hili ni taifa tuko huru hatutishani wala hatulazimishani, ila tunajadili kwa mawazo tofauti na ndio demokrasia yenyewe, na hatuitachoka kusimama kwenye msimamo tofauti.

  4.
  - Haya matatizo yapo, lakini ni nani anayehusika nayo? Ndio walaumiwe indivually kwamba wewe mkuu wa polisi umeshindwa kazi kwa sababu one, two, and three kwa hiyo hufai, wewe waziri mkuu umeharibu one, two, and three hufai, that is the way to go, lakini sio kulaumu kila mtu wa chama fulani au kinachotawala wakati wewe unaoneakana unayajua makosa ni yapi na yamefanywa na nani na sio kuombea taifa zima liyumbe, kwa sababu mkuu wa polisi ameshindwa kuwajibika hizo sio siasa za kisasa za kulisaidia taifa.

  5.
  - Hapa uko swa kwa 100%, Tanzania tuna tatizo la kuheshimu sheria, eihter zipo hatuziheshimu ah hazipo kabisaa mpaka leo sijajua exactly lipi ni kweli, haya matztio uliyoyasema yapo, lakini siamini kwamba rais anawazuia watendaji kwenye mkono wa sheria kutowajibika, lakini you have a point tena a ver strong one.

  6.
  - Hayasababishwi na watendaji wa chini kutowajibika katika nafasi zao, hayasababishwi na wananchi kutoelewa haki zao kisiasa na ksiheria, mimi sio mtawala lakini ninajaribu kuelewa maneno kama ya Zitto kwamba Dowans haina tatizo, maneno ya Mbatia kwamba kumfikisha rais wa zamani kwenye sheria kutayumbisha taifa, hizi sio constuctive ideas kwa watawala, sasa kama wapinzani wanajikanyaga kanyaga watawala watafanya nini sio kuwasikiliza? Lakini bado una point kwamba watawala wetu hawasikilizi kama inavyotakiwa, lakini pia tuliowapa dhamana ya kutufikishia mawazo yetu kwa watawala na wao pia sio makini sana.

  7.
  - Nimesema kwamba ifike mahali iwapo wananchi tuna tatizo na serikali na tuna ushahidi wa kutosha, basi tuipeleke mahakamani kama vile familia ya Kombe ilivyofanya na kuishinda serikali, na kama Mtikila alivyofanya na kuishinda serikali, that is all hayo mengine sikuyasema hapana!

  8.
  - Mtikila aliishinda serikali kwenye kesi ya wagombea huru, lakini serikali ikaa-appeal mpaka leo kesi haijasemwa tena, lakini Mtikila aliiepeleka serikali kwenye sheria na kuishinda, that is a history ambayo watoto wetu wanahitaji one day kuja kuisoma.

  - CCM kama chama haijawahi kupora mali za wananchi, lakini inao viongozi wachache waliofanya hivyo, na hata sisi wananchi wa kawaida pia tumehirikia sana kwenye kulipora taifa letu wenyewe, Mama Mary Kejo sio mwenyekiti wa CCM wa tawi lolote nchini.

  Ahsante kwa post hii inayoweza kuelimisha wengine na hasa taifa at large.

  William.
   
 19. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #19
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - JF inatakiwa kuwa a home of great thinkers.

  William.
   
 20. K

  Kwaminchi Senior Member

  #20
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Mkuu,

  "Tumelilia Demokrasia tukapewa....." Hivi Demokrasia ni nini katika kufahamu kwako? Au kukubaliwa kwa mfumo wa vyama vingi kwa mbinu za kuuridhisha ulimwengu kwa kiini macho, kwako wewe ndio Demokrasia?

  Hatamu za nchi, kwa maneno ya Mzee Julius Nyerere na kwa vitendo zilishikwa na bado zinaendelea kushikwa na CCM. Rais ndio Mwenyekiti wa CCM. Kukaa kwake kitini ni kwa ridhaa ya CCM. Naye ataendelea kwa hali na mali kuipendele
  a CCM kwa kuwa ndio nguzo yake.

  Unavyofikiri wewe huyo akiwa ndiye mwenye kuichagua tume ya uchaguzi, tunaweza kweli kuwa na tume huru? Uchaguzi ulio huru unajikita katika tume huru. Kimsingi Demokrasia ya kweli inategemea sana kiwanja sawa cha ushindani wa vyama vya kisiasa, ambao kwa hivi sasa hatuna.

  Katika nchi yoyote iliyohuru, hatamu za nchi hushikwa na wananchi wenyewe na sio kushikiwa na chama chochote cha siasa. Na hatamu hizo zimo katika kuwawezesha wananchi kuwaweka viongozi madarakani na kuwaondoa hali kadhalika. Mtindo tulionao hauwawezeshi wananchi kuwaweka wala kuwaondoa. Uwezo huo ni wa CCM peke yake.

  Je, hiyo ndio Demokrasi tuliyolilia na tuliyopewa?

  Kama tuna Demokrasi kweli iweje leo hii tuna Katiba ile ile ya Chama kimoja iliyojaa viraka? Iweje mwananchi asiyekuwa mwanachama wa chama chochote
  anyimwe haki yake ya msingi ya kugombea uongozi katika nchi yake mwenyewe? Iweje wakati wa kampeni na uchaguzi washindani watembezewe mkong'oto wao peke yao?

  Che Nkapa akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM aisema hadharani kuwa atahakikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu hata kwa kutumia vyombo vya dola. Naam, sote tuliushuhudia "ushindi wa tsunami na ushindi wa kishindo."

  Je, hiyo ndio Demokrasi tuliyolilia na tuliyopewa?

  Unalalamika kutembezewa chuki, nasi tunadai tutandaziwe haki na ukweli. Mizengwe ikizidi, wenyewe mnaita "wembe ule ule" na chuki haitakosekana.
  Huwezi kucheza mpira na wakati huo huo kuwa mwamuzi ukategemea timu unayocheza nayo kushinda. Halafu unatuhimiza tujiunge na vyama vingine. Tukafanye nini kama si kuwa wasindikizaji tu? Au unatusanifu?

  Ukumbuke tu kuwa hata Himaya ya Roma ilitoweka.
   
Loading...