Marekani siyo mbinguni. Mafwele endelea kupiga kazi.Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imemtaja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania (TPF), Faustine Jackson Mafwele, chini ya Kifungu cha 7031(c), ikisema kuna taarifa za kuaminika zinazomhusisha na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Uamuzi huo unamzuia Mafwele kuingia nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka mmoja uliopita baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania waliwakamata, kuwatesa na kuwafanyia ukatili wa kingono mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi, waliokuwa jijini Dar es Salaam kufuatilia kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.
Tangazo hilo la umma limetolewa chini ya Kifungu cha 7031(c) cha Sheria ya Bajeti ya Usalama wa Taifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Programu Zinazohusiana ya mwaka 2026 (Div. F, P.L. 119-75).
Taarifa hiyo imetolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tommy Pigott.
Pia soma:
1. THRDC: Mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Mwanasheria Agather Atuhaire wa Uganda wanashikiliwa na Jeshi La Polisi
2. Mwanaharakati wa haki za Binadamu Agather Atuhaire, apatikana baada ya kutupwa mpaka wa Tanzania-Uganda, Mtukula
3. Agather Atuhaire asimulia alivyoteswa na kufanyiwa ukatili na polisi wa Tanzania, hili ni doa kubwa kwetu
4. Boniface Mwangi amepigwa na kuteswa na mamlaka za Tanzania na kutelekezwa Ukunda, familia yake yathibitisha
5. Tanzania yakanusha kuwanyanyasa Kingono Wanaharakati Boniface Mwangi na Agather Atuhaire
6. Agather Atuhaire na Boniface Mwangi Waishtaki Tanzania kwa Unyanyasaji wa Haki za Binadamu, Mahakama ya Afrika Mashariki
7. MAREKANI YADAI kuchunguza ripoti za mateso za mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi na Agather Atuhaire wa Uganda nchini Tanzania; inataka uchunguzi