Mafuta ya ubuyu

elimumali

Senior Member
Jan 13, 2010
149
8
Nimepata habari kuwa mafuta ya ubuyu ni dawa ya kumfanya mtu aache ulevi. Aliyenipa habari hii pia hana maelezo kamili. Members, nawaomba mwenye kufahamu atujulishe yafuatayo:
1. Inapatikana wapi
2. Matumizi yake (dose) na side effects zake
3. Bei yake
4. Maelezo mengine ya ziada

Natanguliza Shukrani.
 
Kule Ilala kuna msikiti wanauza maziwa ya Nyati.
Huwa najiuliza maswali mengi, je huyo ni nyati wa plastiki au wa kweli.
Tunajua makasheshe ya nyati halafu we ndo ukajidai unamkamu, utakufa kibudu.
Kuhusu mafuta ya ubuyu ndiyo kwanza nayasikia kwako, ngoja tu digg information, tutaibuka na majibu sahihi na tutakujulisha
 
Bujibuji Ubuyu una mbegu, hivyo inawezekana mafuta yanapatikana hapo - ila yanavyotengenezwa ndio sijui. Kuna mtu hapa ofisini kaniambia kuwa inawaponyesha pia vijana walioathirika na madawa ya kulevya, wanapoitumia inawafanya wasiwe na hamu kabisa ya kuyarudia. Tusaidiane kufanya utafiti namna ya kuipata tuwaokoe ndugu zetu.
 
Kule Ilala kuna msikiti wanauza maziwa ya Nyati.
Huwa najiuliza maswali mengi, je huyo ni nyati wa plastiki au wa kweli.
Tunajua makasheshe ya nyati halafu we ndo ukajidai unamkamu, utakufa kibudu.
Kuhusu mafuta ya ubuyu ndiyo kwanza nayasikia kwako, ngoja tu digg information, tutaibuka na majibu sahihi na tutakujulisha

Hayo maziwa ya nyati yawezekana kuwa kweli kwa sababu, kule Morogoro (Mvomero) wapo nyati wa kufugwa wanaitwa 'nyati maji'. Wanafugwa kama ng'ombe na wanatoa maziwa mengi sana. Pia nasikia maziwa hayo ni tiba kwa baadhi ya maradhi.

Nashawishika kukubali kuwa hayo maziwa ni ya nyati.
 
Kijana kuna nyati wanafungwa tena wapo wa maziwa na wengine ni maksai.
Kuhusu mafuta ya ubuyu icho kipindi kililushwa na ITV last week kwa kukusaidia check na ITV watakupa namba ya msambazaji wa hayo mafuta
 
Wapo Nyati wa kufugwa kwa ajili ya kutoa maziwa. Waliletwa hapa nchini na Hayati Baba wa Taifa kutoka Argentina enzi hizo. Wanapatikana pia huko Muheza,Tanga.
 
Mafuta ya ubuyu ni sawa na kusema mafuta ya pamba, inakuja kuja kwa mbali. Mkuu labda useme mafuta ya mbegu za ubuyu itakuwa na maana zaidi na yanaweza kupatikana. Fuata utaratibu wa kawaida wa kupata mafuta kutokana na mbegu kama wafanyavyo watu wa alizeti.
 
nimeona kwa mara ya kwanza dodoma kwenye maonesho ya 88 ni kweli hayo mafuta yana msaada mwingi kwa binadamu hasa kiafya kuondoa mapunye na kufanya ngozi iwe soft na yanayofanana na hayo; lakini hiyo ya kutibu mwenendo/tabia ya mtu kuacha pombe sina uhakika nayo.

miongoni mwa kina mama wanaohusika na uuzaji wa mafuta ya ubuyu ni jirani yangu namfahamu.
 
tupe contact zake pls

miongoni mwa kina mama wanaohusika na uuzaji wa mafuta ya ubuyu ni jirani yangu namfahamu.

tupe no zake pls
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom