Fahamu kuhusu mafuta ya habat soda pamoja na miujiza yake

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
453
376
Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo

Inapotokea wafalme wa Misri, Malkia wa Ulaya, Mitume na wanasayansi wa kisasa wanakuja na kukubaliana katika jambo moja, ni mhimu kudadisi juu ya jambo hilo.

Ingawa nyakati za sasa tunazungukwa na taarifa na elimu nyingi kuliko katika wakati mwingine wowote, bado tunahitaji kujifunza vitu kutokana na historia na maisha ya kale.

Kutoka kwa baba wa sayansi ya matibabu katika nchi za magharibi Hippocrates kwenda mpaka kwa kiongozi wa mfumo wa mwisho wa kifarao Cleopatra hadi kwa mfalme Tut na jamii iliyofuata, kitu cha pekee ambacho walikuwa wakifanana viongozi hawa kwa pamoja ilikuwa ni thamani waliyoiona katika mtishamba fulani.

Mtishamba au mmea huo ambao viongozi hao walikutana pamoja si mwingine bali ni habbat soda. Habbat soda ndilo jina linalotumika zaidi mashariki ya kati na huko ulaya hujulikana zaidi kama ‘black seeds’.

Kwahiyo niliamua kuchukua muda kusoma na kupeleleza zaidi kuhusu habbat soda kwa ajili yangu mwenyewe na ya wasomaji wangu ili hatimaye niweze kukuletea mwanga kamili juu ya mengi yanayosemwa kuhusu mafuta ya habbat soda.

Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na sehemu gani ya dunia ulipo.

Haya ni moja ya majina yake:
  • Kalonji Oil
  • Black Cumin Seed Oil
  • Nigella Seeds
  • Graine De Nigelle
  • Black Onion Seeds
  • Schwarzkummel
Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa kiingereza wanaita ‘black seed’. Kuna mashine nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kutengeneza mafuta yako mwenyewe kutoka katika mbegu za habbat soda ingawa bado nakushauri ununuwe yale ambayo yameandaliwa tayari.

Habbat soda ina sifa hizi:
  • Huondoa bakteria mwilini
  • Huondoa uvimbe
  • Huondoa sumu mwilini
  • Inaondoa fangasi
  • Inatibu kansa
  • Inatibu pumu
  • Inadhibiti kazi za histamini
  • Inaua virusi
  • Inazuia damu kuganda
Vitu viwili mhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya mafuta haya kuwa ni dawa kwa kila ugonjwa. Vinaimarisha moja kwa moja kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika na mwili.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo inaaminika ndiyo sababu mfalme Tut alipatikana na chupa ya mafuta ya habbat soda kwenye kaburi lake akitumaini kuyachukua na kuyatumia atakapofufuka!

Mtume Muhammad (S.A.W) amewahi kunukuliwa akisema ‘Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo’

Mbegu za habbat soda zinatoka katika majani ya mmea ujulikanao kama ‘Nigella Sativa’ na unalimwa karibu katika kila pembe ya dunia kwa sasa. Asili yake ni Afrika kaskazini, mediterania/ulaya na Asia na kutoka hapo umesambaa kila sehemu ya dunia.

Habbat soda inachukuliwa kama moja ya dawa za asili bora zaidi kuwahi kutokea.

Nini yanachoweza kufanya mwilini haya mafuta ya habbat soda? kuna matumizi mengi ya habbat soda katika kutibu na kukinga magonjwa mbalimbali.

Hapa nimejaribu kukusanya baadhi ya magonjwa 89 ambayo unaweza kujitibu kwa kutumia habbat soda.

Kama kawaida unapewa angalizo kutotumia dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari

1. Yanaimarisha afya ya moyo
Afya mbovu ya moyo inaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi lakini sababu zote chanzo chake kikuu ni matokeo ya kutokuupa moyo virutubishi unavyovihitaji.

Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta safi na yenye Omega 6 na 9, pia yana kirutubishi kingine mhimu zaidi kijulikanacho kama “phytosterols” ambacho husaidia kulazimisha kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu na hivyo kusaidia kuzuia damu kuganda na kujikaza katika ateri.

Viinilishe hivi pia husaidia kushusha lehemu kwenye damu na kiasi cha damu sukari.

Kwa karne nyingi mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo mengi yanayohusiana na moyo.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili

2.Hupigana na maambukizi ya fangasi
Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na ukurutu.

Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa kila mtu kuwa nayo nyumbani.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja. Mengine pakaa kama mafuta yako ya kupakaa sehemu yenye muwasho kutwa mara 2 hadi 3.

3. Hudhibiti Aleji (mzio)
Wengi wetu tunapatwa na aleji na kutokewa na chafya au mafua yasiyoisha na kupelekea kushuka kwa kinga yetu ya mwili. Kutumia mafuta asili ya habbat soda kwa ajili ya kutibu aleji kunaweza kuleta matokeo mazuri bila gharama kubwa.

Na siyo kwamba mafuta haya yatakupa nafuu kwa haraka sana dhidi ya aleji tu, bali pia yatakufanya kujisikia nafuu haraka zaidi kuliko dawa nyingine nyingi za kutibu aleji za viwandani zilizopo sokoni leo.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

4. Ni mafuta mazuri kwa ajili ya ngozi yako
Iwe ni muonekano au afya ya ngozi kwa ujumla, ipo sababu kwanini watu wanapenda kuwa na ngozi ya kupendeza na yenye afya.

Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta mhimu zaidi, yana vitamini nyingi, yana viondoa sumu vya kutosha na asidi amino mhimu ambazo miili yetu huzihitaji.

Mafuta ya habbat soda ni mafuta safi ya ngozi kwa nyakati zote za siku na kwa siku zote. Mafuta haya pia yanasaidia ngozi kutokuungua moja kwa moja na miale ya jua huku yakizuia usizeeke haraka kwa kuondoa mikunjo yoyote kwenye ngozi yako.

Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku

5. Hutibu kansa ya ngozi (Melanoma)
Kansa ni matokeo ya kinasaba cha damu (DNA) kujizidisha au kujizalisha mara nyingi na kwa haraka zaidi dhidi ya uwezo wa kinga ya mwili. Mara nyingi kansa hutokeza vivimbe sehemu mbalimbali mwilini.

Mafuta ya habbat soda yana virutubishi vingine viwili ambavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’ ambavyo utafiti unaonyesha huwa vina uwezo wa kudhibiti kansa kwenye ngozi na kansa nyingine mbalimbali mwilini.

Hii ni kutokana na sifa yake ya haya mafuta katika kuzuia uvimbe na bakteria, sifa kuu mbili za habbat soda.

Habbat soda hufanya hivyo kwa kuzilenga seli zako nyeupe za damu kwa kuziongezea kinga ya mwili na hivyo kuua seli za kansa.

Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku.

6. Hutibu chunusi
Chunusi ni matokeo ya moja kwa moja ya vivimbe kwenye ngozi hasa ya paji la uso na usoni kwa ujumla.

Mafuta haya yanaondoa uvimbe wa aina yoyote kwenye ngozi na kuitengeneza upya ngozi huku yakiiacha nyororo na muonekano wake wa asili.

Mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili hii ya kutunza na kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi na wafalme na malkia wengi katika historia yote ya dunia.

Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku. Unaweza pia kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kusafisha mwili ndani

7. Hutibu maambukizi

Maambukizi ya aina yote hupigwa na kinga ya mwili hasa na seli nyeupe za damu ndizo zinazohusika na kazi hiyo.

Kwa kuiongezea nguvu kinga ya mwili moja kwa moja, mafuta ya habbat soda yanausaidia mwili wako kupigana na maambukizi kutoka kwenye nywele kichani mpaka kwenye kucha.

Hii ni sifa ya pekee ya habbat soda ambayo imekuwa ikijulikana kuwa nayo katika historia yote ya dunia tangu enzi hata leo bado ni moja ya dawa za asili zenye nguvu ya kupigana na maambukizi ya aina nyingi ya mwili.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili

8. Hutibu tatizo la ugumba
Ugumba unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine nyingi, ingawa imethibitishwa pasipo na shaka kwamba mafuta ya habbat soda yamewasaidia wengi kuimarisha afya zao za uzazi.

Kwa wale wote wenye tatizo la uzazi au ugumba tambueni kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo ya ugumba kwa zaidi ya miaka 2000 sasa.

Mpaka leo bado mafuta ya habbat soda yanaendelea kuripotiwa kama ndiyo dawa bora zaidi ya asili kwa ajili ya kurekebisha tatizo la ugumba kwa watu wa jinsia zote mbili.

Wakati huo huo mafuta ya asili ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa bora zaidi ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na hutibu tatizo la nguvu za kiume hata kama mwanaume utakuwa na umri wa miaka 120. Unachohitaji ni kuyatumia kwa kipindi kirefu hata miezi miwili au hata zaidi mfululizo kama tatizo limekuwa sugu sana.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja mpaka mitatu.

9. Huotesha nywele
Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake.

Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa kabisa na huwa mazito kidogo tofauti na yale ya kunywa na kupakaa mwilini.

Matumizi: Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo nywele zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya habbat soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha hivyo hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2 kwa mwezi mmoja hadi miwili

10. Hutibu mafua na homa
Mafua na homa ni matokeo ya kushuka kwa kinga ya mwili na kadri unavyoendelea kuyavumilia magonjwa kama haya ndivyo unavyozidi kuidhoofisha zaidi kinga yako ya mwili.

Kama tulivyoona kabla kuwa mafuta ya habbat soda huongeza kwa haraka sana kinga ya mwili, huondoa haraka sumu mwilini na bakteria mbalimbali na hivyo kufanya kuwa ndiyo dawa nzuri ya asili dhidi ya mafua na homa za mara kwa mara.

Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta haya na vijiko vitatu vikubwa vya asali changanya katika glasi moja (ml 250) ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara moja kila siku.

Kitendo hiki hakitakuondolea mafua na homa pekee bali pia kitaimarisha afya yako kwa ujumla. Fanya kwa siku 7 hadi 14

11. Hutibu majipu
Liwe ni jipu moja au majipu mengi kwa pamoja, mafuta ya habbat soda ndiyo dawa nzuri kukupatia nafuu ya haraka. Hii ni kwa sababu kwa sehemu kubwa majipu ni matokeo ya maambukizi ya bakteria na mchafuko wa damu.

Na mafuta ya habbat soda ni wakala mzuri wa kuondoa bakteria na kusafisha damu na hivyo kuwezesha majipu kuwa chini ya ulinzi.

Unaweza kupakaa mafuta haya juu ya jipu moja kwa moja na wakati huo huo mengine unywe kama ilivyoelezwa kwenye namba 9 hapo juu. Hata hivyo ikiwa jipu ni kubwa sana na huoni nafuu hata baada ya kujaribu mafuta haya muone daktari kwa msaada zaidi.

12. Hutibu kikohozi na Pumu
Ile sifa yake kuu ya kuondoa vivimbe kwenye tyubu za koo, kitendo chake cha kuongeza kinga ya mwili, kuua bakteria na virusi ndiyo sababu za mafuta haya kutumika kutibu kikohozi na pumu.

Imeandikwa katika historia kuwa mababu wa zamani wa Misri walikuwa wakitumia mafuta ya habbat soda hasa kwa ajili ya kuimarisha afya ya mfumo mzima wa upumuwaji.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa wiki 3 hadi 4 hivi

13. Hutibu kuharisha
Mara nyingi kuharisha ni matokeo ya maambukizi ya virusi na bakteria na kama tulivyoona mafuta ya habbat soda hudhibiti bakteria na virusi mbalimbali mwilini na hivyo kufanya ndiyo dawa nzuri mbadala kwa ajili ya kutibu au kuzuia kuharisha.

Huweka sawa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na tumbo kwa ujumla na hivyo kuzuia mwili wako kupatwa na tatizo la kufunga choo.

Inashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha chai au viwili vya mafuta ya habbat soda na kikombe kimoja cha mtindi na utumie asubuhi na usiku kwa siku mbili hivi na kuharisha kutasimama.

14. Hutibu shinikizo la juu la damu
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya shinikizo la juu la damu ni moja kati ya matumizi makubwa ya mafuta haya kwa sasa.

Ingawa haijathibitishwa rasmi kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu lakini wagonjwa wengi wa shinikizo la juu la damu wameripoti kushuka kwa kiwango kikubwa cha mashinikizo yao ya damu wakati wanapotumia mafuta haya ya habbat soda.

Tafiti kama hizi zimepelekea wengi kuanza kutumia mafuta ya habbat soda kama dawa ya asili kwa ajili kutibu shinikizo la juu la damu.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.

Pia hakikisha unakuwa na uzito sawa kulingana na urefu wako. BP ya juu inaweza kuchelewa kupona ikiwa uzito wako upo juu ya inavyotakiwa uwe nao.

15. Huondoa tatizo la kukosa usingizi
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya asili dhidi ya tatizo la kukosa usingizi na matatizo mengine kama hayo ya kuvuruga utulivu wa usingizi kwa ujumla. Watu wengi wameripoti kupata usingizi mororo na utulivu kwa ujumla kwa kutumia habbat soda.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.

16. Huzuia mishtuko na kukakamaa kwa mishipa
Mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya kuzuia kukakamaa na mishtuko mbalimbali kwenye mishipa. Unaweza kuyanywa mdomoni au unaweza kupakaa na kuchua moja kwa moja sehemu ya mishipa yenye matatizo kwa ajili ya matokeo mazuri ya haraka.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa. Pakaa na ujichuwe pia sehemu ya mishipa yenye matatizo

17. Huondoa kichefuchefu na mvurugiko wa tumbo
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu na kuvurugika wa tumbo ni moja ya sifa nyingine kubwa ya mafuta haya.

Uwezo wa mafuta haya kutibu haya matatizo mawili unatokana na nguvu yake kuhamasisha vimeng’enya vyakula vya mwili wako na kuondoa gesi tumboni.

Matumizi: Kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu changanya kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya habbat soda na glasi moja ya juisi ya tangawizi na unywe glasi moja asubuhi na nyingine jioni kila siku kwa siku mbili tatu.

18. Dawa bora kwa matatizo ya meno
Dawa nyingine nzuri kwa matatizo ya meno kama jino kuuma, kuoza, kutoboka, kulegea nk ni mafuta ya asili ya habbat soda.

Kuondoa maumivu ya jino unachohitaji kufanya ni kunyunyiza matone kadhaa ya mafuta haya juu ya hilo jino na utulie tuli kama dakika mbili hivi kutwa mara mbili.

19. Huua seli za kansa ya damu
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda yanacho kitu mhimu sana kiitwacho kwa kitaalamu kama “thymoquinone” ambacho huziua seli za kansa ya damu (leukemia HL-60 cells).

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa

20. Hutibu saratani ya matiti
Mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuzuia seli za saratani ya titi kuendelea kujizalisha na inashauriwa kwa ajili ya kutibu saratani ya titi yatumike kwa kipindi kirefu miezi hata miwili au zaidi.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku

21. Hutibu saratani ya utumbo mpana
Kimeng’enya kiitwacho ‘thymoquinone’ kilichomo kwenye mafuta ya habbat soda na sifa yake kubwa ya kuondoa sumu ndivyo vitu viwili vinavyoyawezesha mafuta ya habbat soda kuzishambulia na kuziua seli za saratani ya utumbo mpana (colon cancer).

Yanabaki kuwa ndiyo dawa mbadala bora zaidi kwa saratani ya utumbo mpana inayosumbua watu wengi miaka ya karibuni.

Habbat soda si dawa ya magonjwa mengine mengi tu bali pia ni moja ya vitu mhimu sana katika kuzuia kukua, kujizidisha au kujizalisha upya kwa seli mbalimbali za kansa.

Uwezo wa mafuta ya habbat soda kudhibiti uongezekaji wa seli za kansa unashawishi sana kiasi kwamba madaktari wengi wamekiri kuwa ni dawa moja bora sana mbadala dhidi ya saratani ya kwenye utumbo mpana.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone

22. Hutibu fangasi ya ngozi na mapunye
Fangasi, mapunye, ukurutu na magonjwa mengi ya ngozi yanaweza kutibika kwa kutumia mafuta ya habbat soda. Fangasi na mapunye ni tatizo linalowapata watu wengi karibu kila sehemu katika nchi tajiri hata katika nchi maskini pia.

Unaweza kuyanywa mdomoni na wakati huo huo ukapaka moja kwa moja juu ya ngozi sehemu yenye tatizo kwa majuma kadhaa. Kama ni kunywa basi kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kila siku mpaka upone

23. Husaidia kupunguza uzito
Uwezo wa mafuta ya habbat soda kushusha uzito unatokana na sifa yake ya kuweza kupunguza sukari katika damu. Zaidi ya kuwa ni wakala muondoa sumu mwilini wa asili, mafuta ya habbat soda husaidia pia kuongeza nguvu katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kupunguza kiasi chako cha njaa.

Hii ya kudhibiti kiasi cha njaa ni mhimu sana hasa wakati unataka kudhibiti mfumo wa vyakula unavyokula.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa, usisahau pia kufanya mazoezi ya kukimbia (jogging kila siku)

24. Hutibu Kisukari
Kitu gani kimeyafanya mafuta ya habbat soda kuwa ndiyo dawa nzuri ya asili dhidi ya Kisukari? Ni ule uwezo wake mkubwa wa kushusha shinikizo la damu na kusaidia wagonjwa wa Kisukari wote ambao ni tegemezi au si wategemezi wa insulin.

Ni dawa nzuri kwa watu wote wenye kisukari aina ya kwanza na kisukari aina ya pili kwa wakati mmoja. Pia huboresha kwa ujumla AFYA ya damu yako.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 2 kila siku kwa mwezi mmoja hadi miwili

25. Hutibu kifafa na mishtuko ya moyo
Dawa nyingi za kisasa zinazotumika kutibu kifafa na mishtuko ya moyo huwa zina orodha ndefu ya madhara mabaya (negative side effects) pia. Bahati nzuri kwa upande wako wewe unayesoma makala hii ni kuwa mafuta ya asili ya habbat soda (black seed oil) ni dawa nzuri ya kutuliza kifafa na matokeo yaletwayo na kifafa.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha watu wenye kifafa na mishtuko ya moyo waliacha kuonyesha tabia au dalili za kifafa au mishtuko ya moyo walipotumia mafuta ya habbat soda kwa wiki 4 hadi 6 huku wakitumia sambamba na dawa walizopewa hospitalini.

Watafiti wengi wanasema hii ni kutokana na kiinilishe mhimu kilichomo kwenye mafuta haya kijulikanacho kama ‘thymoquinione’.

Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.

26. Hutibu vidonda vya kooni
Mafuta ya habbat soda yamethibitishwa kutibu vidonda vya kooni (tonsils) na kuondoa kila aina ya maumivu kooni na kuondoa uhitaji wa dawa za kuondoa maumivu (pain killers).

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa

27. Hutibu kidonda ndugu (MRSA)
Kidonda ndugu au kama kinavyojulikana kwa kitaalamu kama ‘Methicillin resistant Staphylococcus aureus (MSRA)’ ni ugonjwa unaoendelea kuwasumbua wataalamu wengi katika mahospitali maeneo mengi duniani.

Mara nyingi hutokea kama matokeo ya kudhoofika kwa kinga ya mwili. Uwezo wa kuondoa uvimbe na sumu wa mafuta haya unayafanya kuwa dawa mbadala yenye ufanisi zaidi katika kutibu kidonda ndugu.

Mafuta ya habbat soda yatakusaidia kutibu kidonda cha aina hii bila shida yoyote, yatazuia pia kuendelea kuongezeka au kusambaa zaidi kwa kidonda hiki.

Kama kuna matumizi mhimu sana ya dawa hii basi ni hili la kutibu vidonda mbalimbali ikiwemo kidonda ndugu kidonda ambacho huletwa na bakteria na kuwa sugu kutibika kwa dawa nyingi za kawaida.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku na upakae sehemu yenye kidonda mara 2 kila siku kwa majuma kadhaa.

28. Huondoa utegemezi wa madawa ya kulevya
Kutumia mafuta ya habbat soda kuondoa utegemezi (uteja) kwa madawa ya kulevya na vilevi vingine ni moja ya kazi nyingine zilizothibitika kufanywa na mafuta haya.

Katika majaribio, mafuta ya habbat soda yameonyesha kuwa msaada mkubwa kutuliza hali ya kujisikia vibaya na mauzauza mengine yatokanayo na kuacha kutumia dawa za kulevya na wakati huo huo yameonyesha kudhibiti hamu ya kutaka kurudia tena matumizi ya madawa ya kulevya baada ya mtu kuamua kuacha.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja na nusu mpaka miwili

29. Huondoa makovu
Iwe ni makovu ya upasuaji uliopita au ni makovu mengine yoyote, mafuta ya habbat soda ndiyo dawa nzuri kwa ajili ya kuondoa makovu. Ni moja kati ya dawa mbadala chache ambazo zimethibitishwa kuondoa na kutibu makovu moja kwa moja.

Matumizi: Pakaa mafuta haya sehemu yenye makovu mara 2 mpaka 3 kila siku kwa majuma kadhaa.

30. Hutibu kansa ya mlango wa kizazi
Kansa nyingine ambayo mafuta ya habbat soda yamethibitika kuitibu ni kansa ya mlango wa kizazi (cervical cancer).

Hii tena inawezekana kutokana na kimeng’enya ‘thymoquinione’ kipatikanacho kwenye haya mafuta, tafiti zinaonyesha kuwa husaidia pia kwa kuziongezea nguvu na idadi seli nyeupe za damu na kuzidhibiti seli za kansa kuendelea kujizalisha.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.

31. Huzuia madhara ya miale ya jua
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda na kukaa kwenye jua masaa mengi walipatwa na madhara machache ya miale ya jua kulingalisha na wale ambao walikaa juani muda mrefu bila kutumia habbat soda.

Kiasi kikubwa cha kinga ya mwili kilionekana kwa watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda. Kuna tafiti pia zinazothibitisha habbat soda kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa kansa walio kwenye matibabu ya mionzi.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa kama mafuta yako ya kupakaa kwenye ngozi kila siku

32. Huzuia na kutibu athari za sumu ya risasi
Sumu ya risasi (lead) ndiyo moja ya sumu zinazowapata watu wengi dunia nzima sababu ya maendeleo ya viwanda na matumizi ya madawa ya mashambani. Risasi inaweza kuleta shida na mambo mengi kuhusiana na kazi za mwili wako kwa ujumla na kuleta matatizo katika moyo, tumbo, figo, mfumo wa fahamu, mifupa na hata katika mfumo wako wa uzai.

Tafiti zimeonyesha kwamba mafuta ya habbat soda kuwa na uwezo mkubwa kuzuia na kurekebisha madhara katika ubongo yaliyotokana na sumu ya risasi.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa kichwani kila siku yale ya nywele nayo yamethibitika kuwa yanatibu maumivu ya kichwa na matatizo mengine mengi kuhusiana na kichwa

33. Huimarisha ukuwaji wa ndevu
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yanaweza kuhamasisha ubora na ukuwaji wa ndevu kidevuni.

Ingawa hii siyo kazi yake hasa ya msingi, unaweza kupakaa moja kwa moja mafuta ya habbat soda ya nywele juu ya kidevu chako na utaona ndevu zinakuwa na afya nzuri, zinakuwa haraka na kuziacha zenye unyevunyevu pia.

34. Hutibu maumivu ya kuumwa na nyuki na nyigu
Unga wa habbat soda ukichanganywa na maji kidogo ni dawa nzuri kabisa ya asili kwa maumivu au uvimbe kutokana na kuumwa na wadudu kama nyigu na nyuki. Chua sehemu iliyoathiriwa na mchanganyiko huu kutwa mara mbili kwa siku 2 au 4 hivi.

35. Huondoa msongamano kifuani
Mwagia na uchue kwa dakika kadhaa juu ya kifua chako na mafuta ya habbat soda kuondoa msongamano (makohozi, gesi nk) kifuani. Utapata matokeo mazuri zaidi kama utachanganya mafuta haya na asali kwa ajili ya hili zoezi.

Unaweza pia kuamua kunywa mdomoni kijiko kidogo kimoja cha chai kila siku badala ya kupaka juu ya kifua.
 
Mafuta ya Habbat soda au hata Habbat soda ya unga vyote vinapatikana Kariakoo hapo .Kuna mtaa ubavuni mwa soko dogo au la zamani soko la vyakula, kuna maduka mengi hapo utapata ya kila ujazo.
Mwaka jana niliwahi kununua Habbat soda ya unga hapo.

ANGALIZO: Maduka yenyewe yako kwenye Nyumba zile kongwe.Yaani nyumba za zamani ,za miti.
Ulizieni humo mtapata mahitaji yenu.
 
hebu acheni uvivu watanzania nendeni kwenye maduka ya kusuna au yale maduka yaliyopo pembeni ya misikiti ulizien bei huwa haizidi 5000 kwa chupa kulingana na sehemu uliyopo

Watanzania wamezoea kupigwa tu.
Humu Mzizi mkavu ameelezea mara nyingi ,na wadau wameelekeza mahali zinapopatikana katika hizo hizo nyuzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom