Mafuta na gesi ya Russia yaendelea kwenda kwa wingi India, China na nchi za EU. Hizo za ulaya wanayanunua kwa rubles

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,326
Sasa ni wiki sita tangu vita ya Russia vs USA inayopiganiwa Ukraine ianze. Hakuna dalili ya vita hii kumalizika siku za karibuni. Na kuna uwezekano wa kugeuka kuwa vita ya kinuklia mbaya ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.

Kabla ya vita hii, India ilikuwa inanunua asilimia 2 hadi 5% tu ya mahitaji yake ya mafuta haya kutoka Russia sawa na ambavyo USA ilivyokuwa inafanya. Asilimia kubwa iliyobaki walikuwa wanayanunua toka Saudi Arabia, Arab Emirates na Nigeria. Yale ya Iran yalipigwa ban tangia mwaka 2011 na jumuiya ya kimataifa inayoongozwa na USA.

Baada ya vita, kuanzia mwezi March mwaka huu mafuta yote ambayo India inanunua kutoka nje yanatoka Russia kwani bei yake ni zaidi ya nusu ya yale yanayotoka nchi zingine ambazo zimepandisha maradufu bei zake kwa kisingizio cha vita.

China ni wajanja zaidi. Wao wanachojali ni wapi watapata bei nafuu, hayo mengine ya kisiasa si ya muhimu hata kidogo.

Hivyo baada ya ban ya kimataifa kwa mafuta ya kutoka Iran tangia mwaka 2011 iliyopelekea mafuta ya Iran kuporomoka bei, waliendelea kuyanunua kimya kimya. China ndiyo mteja mkubwa wa mafuta ya Russia hata kabla ya vita hii. Mwaka 2021 China ilikuwa inanunua mapipa million 1.72 kwa siku. Baada ya vita mafuta yake yote inayanunua toka Russia, tena wazi wazi despite kubembelezwa na USA isifanye hivyo.

Pamoja na kelele za kisiasa zinazopigwa na nchi za Ulaya kupiga ban ununuzi wa gesi na mafuta ya Russia, ukweli ni kuwa nchi hizi zinaendelea kuyanunua kutoka Russia kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na kabla ya vita. Ukweli ni kuwa nchi hizi za ulaya haziwezi ku survive bila ya gesi na mafuta ya kutoka Russia. Zaidi ya asilimia 40% ya gesi inayotumika majumbani kwao na kwenye viwanda vyao inatoka Russia na hawana sehemu nyingine ya kuipata.

Nchi kama Ujerumani inategemea kwa asilimia 100% mahitaji yake ya gesi na mafuta toka Russia. Na kwa sababu ya kelele zao Russia imewalazimisha kununua gesi na mafuta hayo kwa pesa ya urusi inayoitwa rubles.

Hawana ujanja, wanayanunua kwa rubles kimya kimya. Bila gesi toka Russia wananchi wao watakufa nyakati za winter kwa kukosa household heating system majumbani kwao. Russia ikiamua kulifunga hilo bomba lake linalopeleka gesi na mafuta huko nchi za ulaya, viwanda vingi vya ulaya vitashindwa kufanya kazi na wananchi wao watakufa kwa baridi kwa household heating systems zao kuzimika.

Huo ndiyo ukweli. Ni jambo la muhimu na sisi tukafanya hivyo. Na tunaipongeza serikali yetu ku abstain kwenye kura huko UN security Council kama.ambavyo China na India walivyofanya kwa manufaa haya ya taifa letu.

Sasa kuna faida gani ya sisi ku abstain kwenye votes hizo? Wizara ya nishati haiwezi kukwepa kuwajibika na hali hii.

Sasa ni wiki sita tangu vita ya Russia vs USA inayopiganiwa Ukraine ianze. Hakuna dalili ya vita hii kumalizika siku za karibuni...
Hii Ban ni kama haiwezekani ukiiangalia vizuri. Ndio maana Rais wa Ukraine analalamika kusalitiwa.

Urusi anayo Gas na Mafuta, anahitaji hela/wateja. Eropean, India na China wanazo hela za kununua, wanahitaji Gas na Mafuta, sasa nani hapa anamuhitaji mwenzie zaidi?

Urusi asipomuuzia China, India, USA or European countries hatokosa wateja. Lakini na wao China, India na European countries zisiponunua kwa Urusi zinaweza kupata kwengine Kwa Bei nafuu, ukakika wa mzigo wa kutosha na kwa haraka zaidi kama ilivyo kutoka Urusi??

Fikiria Urusi kapigwa Ban lakini bado ana ujasiri wa kuweka masharti kwenye bidhaa yake, means anajua hawana ubavu wa kuikataa na "watakuja tu"

Baniani Mbaya, Kiatu Chake Dawa..!!
 
Nasubiri hawa members waje wapinge Sexer permanides brazaj , wazee wa mahaba niuwe hawa, wenyewe hata wakiambiwa na marekani/Nato mbuzi kanya dhahabu wanaamini fasta.

Umesikika Mrusi tokea pande za Buza kwa Mtogole, umewakilisha:

IMG_20220302_122620_294.jpg

Ila usisahau wengine tunapinga udhwalimu wote bila kumwangalia mtu usoni. Hii hata kama dhwalimu huyo ni Tanzania, CCM, wewe, Sirro au awaye yote.

Wapenda haki watailaani Urusi kwa uvamizi wake Ukraine

Hapo ndipo tunapoachana njia panda na chawa chawa wowote wakiwamo wa Buza.

Habari ndiyo hiyo.
 
Vita ni uchumi, vita ni pesa... bahati mbaya watu hawaangalii sana kwenye angle hii. Juzi waziri mkuu wa uingereza alikua Ukraine, pamoja na kutoa misaada pia walitoa mikopo mikubwa sana kwa Ukraine.

Vivyo hivyo USA na world bank wameikopesha pesa nyingi sana Ukraine, mara baada ya vita Ukraine itakua na madeni makubwa sana, pengine hayo madeni yatadumu miaka na miaka.

Rejea Marshall plan ya ku re boost uchumi wa ulaya toka marekani. Mpaka leo ulaya anadaia na USA... ndio maana anapelekeshwa kama mjinga.
 
Du! Wazungu ni watu wabaya sana. Watu wapo vitani wanadundwa kila kukicha wao badala ya kuwasaidia wanawakopesha!
 
Kuna kitu kidogo mleta mada hukielewi

Makampuni mengi yanayouza mafuta toka Urusi ni ya nchi za Magharibi.Asilimia kubwa ya hizo pesa zinaingia benki zao za nchi za Magharibi
Ndio maana unaona hali hiyo
Ni sawa na Sisi tuwe na gesi ya mtwara kampuni inayochimba na kuuza ni ya mmarekani kwa mfano akiwa anachimba na kuuza hiyo gesi kwa ku export Marekani. Halafu Sisi Marekani akatuwekea vikwazo si rahisi kugusa gesi

Kampuni nyingi zilizoondoka Urusi za Magharibi ni zile zilizojisajili kama local company zikifanya biashara ndani ya Urusi na kulipa kodi zote ndani ya urusi
 
Kwahio hao hawajagoma bado wanafanya biashara urusi??? Hawajasikia miongozo ya wakubwa wao??
 
Vita ni uchumi, vita ni pesa... bahati mbaya watu hawaangalii sana kwenye angle hii. Juzi waziri mkuu wa uingereza alikua Ukraine, pamoja na kutoa misaada pia walitoa mikopo mikubwa sana kwa Ukraine.

Vivyo hivyo USA na world bank wameikopesha pesa nyingi sana Ukraine, mara baada ya vita Ukraine itakua na madeni makubwa sana, pengine hayo madeni yatadumu miaka na miaka.

Rejea Marshall plan ya ku re boost uchumi wa ulaya toka marekani. Mpaka leo ulaya anadaia na USA... ndio maana anapelekeshwa kama mjinga.

Pana mambo mawili tofauti hapa:

1. Suala zima la haki kutokana na uvamizi
2. Kulipia gharama za uvamizi.

Haipo shaka kuwa Mrusi ndiye mvamizi kwenye kadhia hii. Huyu ndiye chanzo cha vita.

Imeamriwa raslimali za mvamizi huyu zinazoshikiliwa kutumika kwenye kulipia gharama za vita.

Labda kama hutaki Mrusi kuvuna alichopanda?
 
Kwahio hao hawajagoma bado wanafanya biashara urusi??? Hawajasikia miongozo ya wakubwa wao??
Wakubwa wao ndio wameamua hivyo

Ndio maana hata Russia hana ubavu wa akiwakea vikwazo vya mafuta na gesi nchi za Magharibi pamoja na yeye kawekewa vikwazo kibao sababu akiteua za kukata hao wazalishaji na wasambazaji mafuta mababe yenye pesa uwekezaji ya nchi za Magharibi ndio hiyo hiyo mizalushaji .Hivyo Urusi yenyewe itaunia.Itazima mitambo na uzalishaji na kutimka na teknolojia zao kurudi zao nchi za Magharibi kwao.Kutakuwa na chaosi ya uzalishaji gesi na mafuta Urusi penyewe

Ndio maana Russia hathubutu kufunga koki ya bomba la mafuta au gesi kwenda hizo nchi pamoja na wao kumbamiza vikwazo barabara
 
Sasa ni wiki sita tangu vita ya Russia vs USA inayopiganiwa Ukraine ianze. Hakuna dalili ya vita hii kumalizika siku za karibuni. Na kuna uwezekano wa kugeuka kuwa vita ya kinuklia mbaya ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.

Kabla ya vita hii, India ilikuwa inanunua asilimia 2 hadi 5% tu ya mahitaji yake ya mafuta haya kutoka Russia sawa na ambavyo USA ilivyokuwa inafanya. Asilimia kubwa iliyobaki walikuwa wanayanunua toka Saudi Arabia, Arab Emirates na Nigeria. Yale ya Iran yalipigwa ban tangia mwaka 2011 na jumuiya ya kimataifa inayoongozwa na USA.

Baada ya vita, kuanzia mwezi March mwaka huu mafuta yote ambayo India inanunua kutoka nje yanatoka Russia kwani bei yake ni zaidi ya nusu ya yale yanayotoka nchi zingine ambazo zimepandisha maradufu bei zake kwa kisingizio cha vita.

China ni wajanja zaidi. Wao wanachojali ni wapi watapata bei nafuu, hayo mengine ya kisiasa si ya muhimu hata kidogo.

Hivyo baada ya ban ya kimataifa kwa mafuta ya kutoka Iran tangia mwaka 2011 iliyopelekea mafuta ya Iran kuporomoka bei, waliendelea kuyanunua kimya kimya. China ndiyo mteja mkubwa wa mafuta ya Russia hata kabla ya vita hii. Mwaka 2021 China ilikuwa inanunua mapipa million 1.72 kwa siku. Baada ya vita mafuta yake yote inayanunua toka Russia, tena wazi wazi despite kubembelezwa na USA isifanye hivyo.

Pamoja na kelele za kisiasa zinazopigwa na nchi za Ulaya kupiga ban ununuzi wa gesi na mafuta ya Russia, ukweli ni kuwa nchi hizi zinaendelea kuyanunua kutoka Russia kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na kabla ya vita. Ukweli ni kuwa nchi hizi za ulaya haziwezi ku survive bila ya gesi na mafuta ya kutoka Russia. Zaidi ya asilimia 40% ya gesi inayotumika majumbani kwao na kwenye viwanda vyao inatoka Russia na hawana sehemu nyingine ya kuipata.

Nchi kama Ujerumani inategemea kwa asilimia 100% mahitaji yake ya gesi na mafuta toka Russia. Na kwa sababu ya kelele zao Russia imewalazimisha kununua gesi na mafuta hayo kwa pesa ya urusi inayoitwa rubles.

Hawana ujanja, wanayanunua kwa rubles kimya kimya. Bila gesi toka Russia wananchi wao watakufa nyakati za winter kwa kukosa household heating system majumbani kwao. Russia ikiamua kulifunga hilo bomba lake linalopeleka gesi na mafuta huko nchi za ulaya, viwanda vingi vya ulaya vitashindwa kufanya kazi na wananchi wao watakufa kwa baridi kwa household heating systems zao kuzimika.

Huo ndiyo ukweli. Ni jambo la muhimu na sisi tukafanya hivyo. Na tunaipongeza serikali yetu ku abstain kwenye kura huko UN security Council kama.ambavyo China na India walivyofanya kwa manufaa haya ya taifa letu.

Sasa kuna faida gani ya sisi ku abstain kwenye votes hizo? Wizara ya nishati haiwezi kukwepa kuwajibika na hali hii.

Naona Marekani wanajipiga vidole kwa hasira
 
Du! Wazungu ni watu wabaya sana. Watu wapo vitani wanadundwa kila kukicha wao badala ya kuwasaidia wanawakopesha!
Mzee hakuna cha bure kwenye dunia hii, pesa yao wanaipata kwa damu za wengine. Pale ukraine vita imetafutwa.. industrial military complex za USA wanahitaji kuuza bidhaa...ni lazima watu wapigane ili silaha ziuzwe. Na wamiliki wa viwanda ndio matajiri wa kutupwa, ndio wanafadhili kampeni za urais nchini marekani (fuatilia)

Kwa nchi kama marekani kuchochea vita ni pesa kwake, ila kamwe hawataki vita nchini kwao.
 
Hii Ban ni kama haiwezekani ukiiangalia vizuri. Ndio maana Rais wa Ukraine analalamika kusalitiwa.

Urusi anayo Gas na Mafuta, anahitaji hela/wateja. Eropean, India na China wanazo hela za kununua, wanahitaji Gas na Mafuta, sasa nani hapa anamuhitaji mwenzie zaidi?

Urusi asipomuuzia China, India, USA or European countries hatokosa wateja. Lakini na wao China, India na European countries zisiponunua kwa Urusi zinaweza kupata kwengine Kwa Bei nafuu, ukakika wa mzigo wa kutosha na kwa haraka zaidi kama ilivyo kutoka Urusi??

Fikiria Urusi kapigwa Ban lakini bado ana ujasiri wa kuweka masharti kwenye bidhaa yake, means anajua hawana ubavu wa kuikataa na "watakuja tu"

Baniani Mbaya, Kiatu Chake Dawa..!!
kwan Ghadaf aliwai kuwa mny'onge mpk anakata kamba ?
 
Umesikika Mrusi tokea pande za Buza kwa Mtogole, umewakilisha:

View attachment 2183360

Ila usisahau wengine tunapinga udhwalimu wote bila kumwangalia mtu usoni. Hii hata kama dhwalimu huyo ni Tanzania, CCM, wewe, Sirro au awaye yote.

Wapenda haki watailaani Urusi kwa uvamizi wake Ukraine

Hapo ndipo tunapoachana njia panda na chawa chawa wowote wakiwamo wa Buza.

Habari ndiyo hiyo.
hiko ndo wengi hawaelew , tunapokosoa uvamiz hatumaanish tunamshabikia mtu fulani bali kwa utu wa kawaida tu , alichofanya Putin ni uonevu
 
Back
Top Bottom