Mafuta machafu yarudishwa kutoka rwanda

mbutalikasu

Member
Jan 20, 2012
53
17
Wana JF kuna mafuta machafu yaliyoingizwa nchini na TPDC na kuyauza katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda yamerudishwa nchini kwasababu mafuta hayo ni machafu kupindukia na nimepita ktk mpaka wa Kabanga nimekuta kuna malori kama matano ikabidi niende Rusumo nikakuta pia malori mawili moja la kitanzania na lingine la kinyarwanda mali ya Merez la kitanzania ni kampuni ya Bridgeway na nimeambiwa yapo mengine Kampuni ya Worldoil na Liberty yanakuja.

Source mimi mwenyewe. Pia napendekeza mwandishi wa habari aje apige kambi hapa awarushie hiyo taalifa live bila chenga
Aibuuuuuuuuu tanzania aibuuuu kwa serikali aibu kwa TBS na TPDC
 
Haya mafuta machafu yatatuharibia magari sana na kuwatia hasara watu wengi ; sijui serikali itachukua hatua gani kuthibiti hali hii?
 
Kuna haja ya kuingiza kipengele cha kunyonga watu kwenye katiba mpya.
Umejichanga kununua gari wanakuja kutuharibia kwa wese batili
 
Ni nani hasa anafanya hii biashara ya kuchakachua mafuta?
 
nakumbuka ilikuwa 2005 kuna mzee mmoja aliwahi niambia, iko siku hii nchi tutatangaza tenda ya kutafuta Rais maana kila mtu anafanya anavyofikiria yeye na si kwa kufuata taratibu zilizowekwa:A S cry:
 
Ni nani hasa anafanya hii biashara ya kuchakachua mafuta?

Augusta Energy kwa kushirikiana na Ewura.
Makampuni yameshaishtaki hii kampuni kwa Ewura but hakuna hatua yoyote ya maana Ewura imechukua.

Cha ajabu uchafu huu wa sasa hata dawa inayotumika kugundua uchafu kwa kupaka kwenye "deep stick" (paste) imedunda na inausoma kama mafuta tu
 
Kuna haja ya kuingiza kipengele cha kunyonga watu kwenye katiba mpya.
Umejichanga kununua gari wanakuja kutuharibia kwa wese batili

Mbaya zaidi ni pale gari linapoharika kabla hata hujamaliza kulipa mkopo. Watu hatulali tunachezesha vichwa tukiwaza jinsi ya kujikwamua kuukimbia umasikini wanaibuka wengine wanatuvuta miguu.
 
kaka haya sasa hivi hayachakachuliwi hapa nchini bali yanaingizwa nchini yakiwa yashachakachuliwa na haya mafuta yaliletwa na na TPDC ambayo ndo serikali yenyewe na ikawauzia wafanya biashara na hapa Tanzania yamesambazwa sana ktk vituo vingi vya mafuta hasa Kobil, Mogas, Camel na Lakeoil ni hatari na inasemekana wafanya biashara wameishitaki serikali na serikali wanamtafuta mmiliki wa meli eti ndo alichakachua kweli tanzania inaliwa na wenye meno ,,,,hongera mzee wa kaya kwa kutuhalibia magari yetu maana wewe ndo unaeshindwa kutuwajibishia kina haruna masebu
 
Haya mafuta machafu yatatuharibia magari sana na kuwatia hasara watu wengi ; sijui serikali itachukua hatua gani kuthibiti hali hii?

Haki ya nani haya mafuta razima yauzwe bongo. Inchi ya kitu kidogo. Pongezi kwa wakwere wa kutupatia raisi ambaye hajawahi tokea
 
Kuna haja ya kuingiza kipengele cha kunyonga watu kwenye katiba mpya.
Umejichanga kununua gari wanakuja kutuharibia kwa wese batili



Yani hii kipengele ni muhimu sana!
Mbaya zaidi unajikuta umejinyima mambo mengi kusudi upate angalau kiusafiri halafu hawa wala rushwa wanakuja kukuharibia usafiri wako kwa sababu ya wao kujineemesha na familia yake.

Hili ktk katiba mpya ni muhimu sana kuzungumziwa.
 
Mafuta yaliyoingizwa nchini hasa petrol, yamepigiwa sana kelele na makampuni karibu yote makubwa ya mafuta kwamba yako chini ya kiwango. TBS walitoa taarifa ya kueleza haikubaliki kuingiza mafuta yaliyochanganywa na kitu kingine chochote maana inasemekana petrol ilichanganywa na ethanol.Ghafla wakasema wanaochanganya ni makampuni ya mafuta na sio supplier. Hivi nchi hii watu wanafikiria nini? Bora Ngereja na Malima wakapumzike maana kazi wameifanya kweli kweli kwenye nishati na madini.
 
kaka hili ni soo la Cyril Chami maana TBS iko chini yake na naibu wake aliwahi kumshauri kuhusu hiyo isue ya hayo mafuta pia katibu mkuu alishawahi kugoma kutia sahihi ili mafuta hayo yashushwe yeye akawazunguka mpaka yakashuahwa na ndo kilichomtimua sasa serikali inajutia
 
Mbutalikasu, ni kweli TBS ndo wenye mamlaka ya kuruhusu mafuta safi kuingia nchini. Waliruhusu mafuta machafu mara kadhaa hadi makampuni yakalalamika. Kuona hivyo, wiki mbili zilizopita TBS wakatangaza kuwa mafuta yenye ethanol hayakubaliki, katika kujikosha. Makampuni yakaijia juu kwa kusema wazi kuwa TBS ndo iliruhusu mafuta hayo na mchakato wa kisheria unatarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi wa sampuli zote kukamilika.
Ila si sahihi kusema mafuta hayo yaliletwa na TPDC. Yaliletwa kwa tenda na Augusta.
 
Sasa kazi ipo nasikia hayo magari yanazidi kujazana hapo Rusumo border na maadreva wanasema Wanyarwana wamechukia ile mbaya na uaminifu uliokuwepo unaweza kuisha na waagiza mafuta wakahamia kenya sijui serikali ina tamko gani na mie hayo mafuta nilijaribu kuyacheki yanafanana kama tope la volcano ukiyatikisa yanajichanganya fresh ila yakitulia petrol inakuja juu lile tope linakuwa chini
 
Ni nani hasa anafanya hii biashara ya kuchakachua mafuta?

Laiti tungetaka kujua hili aibu hizi zisingetukuta tumeamua kukwepa hilo swali na badala yake tukaamua kuadhibu watz wote- ishara ya utawala legelege
 
Ewura wawajibishwe na wafilisiwe, wamefumbia macho madudu na wameshanunuliwa kwa thamani ndogo sana.
 
jamani Kagame ni rais.taasisi zake hazina mzaha katika kazi!!Kagame nakupa ruhusa tawala na tanzania walau miaka 10 halafu maraisi wastaafu wajionee wenyewe discpline ya serikali itakayokuwepo
 
Back
Top Bottom