Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
ANGOLA, ambayo imo katika shirikisho la mataifa yanayosafirisha kwa wingi mafuta, OPEC na la pili kwa usafirishaji mafuta barani Afrika baada ya Nigeria, linakabiliwa na hali mbaya ya kuporomoka kwa bei ya mafuta ghafi duniani huku wananchi wakiwa hawajanufaika na rasilimali hiyo.
Usafirishaji wa bidhaa hiyo inaliingizia taifa hilo zaidi ya asilimia 90 ya fedha za kigeni, lakini kipato cha wananchi wake ni cha chini na pengo la maisha likionekana kuwa kubwa kiuchumi.
Angola inashika nafasi ya 12 kwa nchi wanachama wa OPEC katika usafirishaji wa mafuta ghafi ambapo kwa sasa asilimia 90 ya mafuta inayozalisha inasafirisha China na Marekani, na kwa mwaka 2015 inaelezwa kwamba mafuta ghafi yaliingiza kiasi cha Dola bilioni 57.61.
ZAIDI...