Mafuriko yasababisha Magari kusitisha safari barabara ya Arusha - Moshi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,323
7,963
Mvua zilizoanza kunyesha usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Aprili 3, 2023 katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro imesababisha mafaruko na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika barabara kuu ya Moshi-Arusha eneo la kwa Msomali Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa zaidi ya saa tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amekiri kutokea kwa adha hiyo na amesema maji hayo ni mengi na kwa sasa hakuna magari yanayoweza kupita kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.

"Ni kweli kwa sasa eneo la kwa Msomali halipitiki maji ni mengi kupita kiasi, magari yamesimama kwa muda na hayawezi kutoka upande wa Moshi kwenda Arusha na upande wa Arusha kwenda kuja Moshi," amesema.

Kamanda Maigwa ambaye amesema yuko njiani kelekea eneo la tukio na amewataka wananchi na wasafiri kuwa na subira wakati huu ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na mamalaka nyingine ikiwemo Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kutafuta ufumbuzi.

Meneja wa Tanroad mkoani hapa, Mota Kyando ameliambia gazeti hili kuwa wako eneo la tukio kutafuta suluhisho la tatizo hilo ili shughuli za usafiri ziweze kuendelea kama kawaida.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro (RSA), Khadili Shekoloa amesema yupo eneo hilo kushirikiana na mamlaka nyingine kuhakikisha usalama unakuwepo katika eneo hilo.

MWANANCHI
 
Kila mwaka kunakua na hiyo adha hilo eneo,

Yani nazungumzia tatizo moja kujirudia kila mwaka.

Haiwezekani kitu kile kile kijirudie kila siku as if sisi ni wanyama tunaishi porini.

Aliyetuloga Watanzania ameshafariki siku nyingi kwakwel.
 
Kila mwaka kunakua na hiyo adha hilo eneo,
Yani nazungumzia tatizo moja kujirudia kila mwaka...
We aliyekuloga ndio amekufa. Natural disaster iko kila mahali duniani. Juzi tu Marekani raia 26 walipoteza maisha na nyumba nyingi kubomolewa na mafuriko. Mijitu iliyozoea kulalamikia wenzake km wewe ni laana duniani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom