Mafuriko yanatutoa jasho, yakitokea yaliyotokea Haiti jee? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuriko yanatutoa jasho, yakitokea yaliyotokea Haiti jee?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Jan 14, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Just wondering out loud! Mafuriko ya last week yanatishia Taifa kuwa na mini budget na woga kibao na kuomba wahisani, je tukikumba na tetemeko baya kama la Haiti au Tsunami la nguvu tutafanyaje? Je tuko tayari au tutakimbilia kuuza uhuru kwa kutembeza bakuli la nguvu ingawa ni janga na ni kawaida kupata misaada wakati wa shida?

  Tumejiandaaje?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jan 14, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Yakitokea yaliyotokea Haiti tutakuwa kama Haiti. Kwa bahati mbaya hatuko karibu na Marekani...
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Yakitokea hayo kwetu ni wazi tutaangamia. Ofisi ya waziri mkuu ina kitengo cha maafa (yaani FEMA ya Bongo) lakini hakuna wanalofanya. Juzijuzi tumepoteza watu wengi sana mkoani Kilimanjaro kutokana na maporomoko ya matope na sikuona lolote lililofanywa na FEMA hiyo kusaidia wale wachache waliosalimika wakiwa wamepoteza familia na mali zao ili waanze upya.


  Hii ndiyo gharama tunayolipa kwa kukubali kutawaliwa na serikali isiyokuwa yetu (the people). Mjerumani alitutawala kwa miaka kama 30 tu, halafu mwingereza akatubeba kwa miaka kama 40 tu. Kila mmoja aliacha signature yake. Lakini leo sis tumejitawala karibu miaka 50 na bado hakuna la maana tunalojivunia.
   
 4. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Another issue ambayo nilkuwa nafikiria sana!! Hivi ni Nyumba gani bongo zenye steel reignforced concrete? Halafu wajenzi wetu hujali tetemeko wakati wana-plan ujenzi? Ikitokea tetemeko kama hili, hivi Dar is-itakuwa flat! Acha vile vibanda vya mikoani?
  Wajenzi mpo??
   
 5. kui

  kui JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  Mungu Apishe mbali. God Bless Tanzania!
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Tumwombe Mungu sana majanga yasitutokee!!!! achilia kilosa, Janga la ufisadi tu tunashindwa, je kama hili itakuwaje!
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wee acha tu, Tumwombe Mungu. It is what we can say. Dar hakuna cha kubaki. Ni machache sana yatatamalika hata kuangaliwa.
   
 8. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Dear Friends,
  I'm writing with a heavy heart, praying for the thousands in Haiti hit hard by yesterday's devastating earthquake. While more information is still coming, we now know that hundreds of thousands are without homes, hospitals and hope.
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  God forbid, ikitokea kama haiti tumekwisha ndugu zangu, kwa bongo hii hii. its high time suala la maandalizi ya majanga liangaliwe kwa upana.
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hayawezi kutokea,mungu mwenyewe huwa anaangalia anavyowalocate watu...anaangalia na uwezo wao wa kufikiri na kutatua majanga
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  apo ndio tutajua serikali ya kisanii na serikali ya kweli, kuna kitu kinaitwa disaster management, serikali makini zote zinakua nazo, hata hao haiti ndio zilezile serikali za kisanii na ubepari waliokumbatia, kipindi cha hurrican katrina ktk nchi zinazoizunguka mareknai ni cuba pekee iliathirika kidogo kuliko nchi zote kwa sababu ya good disaster management, god bless socialism and fiedel castro to recover quickly!
   
 12. O

  Ogah JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Level ya response yetu kwenye majanga kama hayo yanakupa picha kamili ni jinsi gani tutakavyokuwa
   
 13. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mh! God forbid, na hayatatokea! Mchungaji, vipi bana?
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..labda majanga hayo yapige Ikulu au bungeni kama ilivyotokea Haiti ndiyo utaona serikali inashtuka.

  ..kinyume cha hapo mimi nadhani Raisi na serikali yetu wanaweza KUUCHUNA tu kama wanavyofanya sasa hivi.

  ..janga lililotokea Haiti limemfanya Hillary Clinton akatishe ziara yake ya Asia. hapa Tanzania pamoja na mafuriko yanayozidi kutokea Raisi amesafiri kwenda Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Raisi wao kutumikia kipindi cha pili!!
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Rev. Kishoka

  Wacha kujidanganya kwanza serikali ya Tanzania ikiongozwa na Chama Cha Majambazi haijatoka jasho lolote kwa hili. Wao wanaangalia mambo ya uchaguzi tu na kama likitokea tetemeko basi fahamu itakuwa sherehe kwao kwa sababu watawaalika Mafisadi wenzao na kukomba pesa za walipa kodi kama vile wamepagawa.

  Hawajali hilo wao ni kuwaandalia akina Drog the bar lunch na vitu kama hivyo. Wakiona JF wanajikusanya basi na wao ndio wanakurupuka kwa kuona aibu.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Dear I.O

  Wajenzi tupo, tupo kabisa, kwa ajili ya taifa na wananchi

  Sijajua wangapi wamechukulia hii thread kama 'jicho' la kuangalia kila kitu hapa nchini.

  Ujenzi wa majengo(maghorofa) ya Tanzania, yako reinforced kwa kutumia steel.

  Katika ujenzi inategemea hasa data za earthquake kwa miaka 50 au 100 iliyopita. Na hizi huwa zinatumika katika ujenzi, mathalani Dar es salaam record ya juu ya earthquake let say 3.0 magnitude. hivyo majengo mengi yanakuwa designed kwa hiyo record. Jengo la kawaida kabisa ambalo limekuwa reinforced na designer haku-consider earthquake linaweza kuhimili 2-2.5 Magnitude(inategemea na aina ya ujenzi)

  Let say tunaamua leo kujenga majengo ya ghorofa yenye uwezo wa kuhimili 7.0 magnitude iliyotokea Haiti, tatizo lake ni gharama na owners wengi huwa hawataki kusikia hizo unforseen disaster zikitamkwa.

  Tanzania yapo majengo imara sana siyo tu yanaweza kuhimili eathquake kubwa, bali hata terrorism attacks! ujenzi wa Tanzania unategema nani anajenga na ana ufahamu gani, siyo majengo yote yako hatarini!

  Pili, hakuna Tanzania standard ya ujenzi wa majengo yake, we are using British(BS), Euro, USA n.k sana sana (TBS) wanajitahidi hapa na pale, japo kazi yao ni copy and paste ya BS).

  Hatuna regulation ya majengo inayoendana na hali ya Tanzania, na iliyotayari kuhimili hizo disaster.

  Wajenzi hawana tatizo( robot) tell them what to do, tena Tz civil engineers are doing very good job probably more than any other engineers. So ujenzi hauanzii kwa designer au contractor unaanzia kwa mmiliki na archtects wake, wao wanampa structural designer(yeye atawashauri kile anachoona kitafaa, msemaji wa mwisho ni archtects)

  Due to global climate change ,these disasters for sure one day we may cry, research za wenzetu wanasema developing countries ndio tutaathirika sana. Ni jukumu la serikali kuweka requlations na kuzisimamia, na kuzi-update kila mara haya matatizo yanapotokea.swali ni kuwa wata update regulation zipi? wakati hazipo!!

  Leo kwa mfano tunaweza kupitisha sheria kuwa lazima kila jengo liwe designed kwa ku-resist earthquake let say of 10.0 R , ujenzi wake ni gharama sana, sana, na wachache sana watakaoweza ku-afford, but at least yakitokea matatizo kama ya Haiti tunakuwa kwenye safe side.

  Sasa hapa key players ni serikali, mabenki yanayotoa loan, owners waelimishwe na ERB wasimamie hizo designs na ujenzi.

  Leo kwa sababu tunaringa tuna matetemeko ya ardhi madogo, nyumba nyingi zimejengwa kwa standard za hali ya sasa. We need our standard, na kutokuwa na standard ni alama tosha kuwa serikali haitumii wataalamu wake.

  we need smart leaders
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280

  Ufisadi si janga bali inatokana na kuwa na kiongozi ambaye aliingia madarakani kwa kubebwa na mabilioni ya mafisadi na hivyo kuwaogopa kuwachukulia hatua yoyote kwa kuwa na wasiwasi wa kuumbuliwa na mafisadi. Tungekuwa na Rais mchapa kazi na aliyeweka maslahi ya Taifa mbele na kaingia madarakani kwa uwezo wake mwenyewe badala ya kubebwa na mafisadi hawa mafisadi wote wangeshashikishwa adabu na sasa hivi wangekuwa ni history katika anga la Taifa letu, lakini bado wanapeta na wataendelea kupeta kutokana na yule aliyedhaniwa kuwa ni chaguo la mungu kuwaogopa mafisadi kupita kiasi.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Nani kasema majanga kama hayo yanaweza kutokea Tanzania? we are so special..
   
 19. h

  housta Senior Member

  #19
  Jan 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo unataka kusema kuwa Haiti ilivyoangaliwa na Mungu..aliona wanaweza kukabili hili janga??You are wrong in that.Hizi ni natural disasters,zinatokea.Kwa imani yangu,hizi zinaitwa end of days!Kwa Wanasayansi watasema ni mother nature ana-balance mambo(ratio ya population na resources).All in all ni kuomba Mungu yasitutokee.Mungu awasaidie waliofikwa na janga hili!
   
 20. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hizi ajali tu za barabarani zinatokea kila siku zinaua watu wengi miaka nenda rudi hatujapata solution na serikali yetu inaona kama kawaida wakati nyingi zinaweza kupata ufumbuzi tatizo hatuna umakini kwenye kushughulikia maswala mazito nchini kwetu.badala kutafuta longterm solutions serikali inachagua short term solutions.


  sasa ukizungumzia swala kama la haiti jibu tutakalo lipata ni kazi ya Mungu,sawa kazi ya mungu lakini je mmejiandaa vipi? mnajifunza nini?.tuna jeshi ambalo wala haliko vitani,je respond yao kwenye yale mafuriko yalikuwaje? ukipata jibu hapo basi ndio utaweza kujua hali itakuwaje janga kama la haiti likitokea.

  Mungu atunusuru na atupunguzie majanga yanayosababisha maafa duniani.
   
Loading...