barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
"Serikali Inashukuru..."
Jana nikiwa kijijini Kisanga, Pawaga nilipata bahati ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masanze aliyeongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
RC Amina Masanze alishukuru kwa dhati kwa misaada iliyotolewa na Wana-Iringa wakiwamo wadau wa mtandao wa Mjengwablog.com wa Nyumbani Na Diaspora. Misaada iliyokabidhiwa jana ni pamoja na magodoro 20 na mahema tisa, vyote ikiwamo nguo za watoto na watu wazima vina thamani ya shilingi milioni tatu na nusu.
Pichani katikati ni DC wa Iringa Ndugu Richard Kasesela.
( Picha zaidi: Mjengwablog.com)
source:Mjengwablog