MAFURIKO: Hali ya usafiri Dar yawa tete, makazi yasombwa!

Ndivyo ninavyoisoma taswira na mtazamo wangu kwa wanasiasa, heti kila kitu Serikali, vyama vyetu vya siasa ukiachia kuhamasisha na kuwakilisha wananchi katika kuikosoa, kudai haki, kutoa maelekezo kwa Serikali katika utendaji wake, na kutoa Elimu kwa wananchi, vyama vyetu wajibu wao uko wapi katika matatizo ya kitaifa, ambapo, si mwana CCM wala CDM, Si CUF wala UDP anakumbuka tofauti zao kisiasa na kichama wakati wa majanga, mbona vyama vinatutenga? Mnasubiri tufe mje kutoa rambirambi? Zikowapi helkopta zilizotumika kutuomba kura?? Hatuna thamani tena??

Lakini mkuu, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE. na hapo baadae kidogo tutahutubia wahanga.
 
Mkuu hapo serikali ina mkono wake. Kwani ilikua wapi mpaka raia wajenge katika vulnerable areas kama hizo? Vested political interests nazo zina nafasi,ambapo uhitaji wa kura ufanya wanasiasa kuingilia shughuli za watendaji wataalamu na hivyo kuruhusu maeneo kama Jangwani kukaliwa na raia.

Sijakata serikali ina mkono wake kwenye hilo, hii ni nchi maskini raia pia inabidi atumie akili yake mafuriko ya Jangwani ni jambo la kawaida Dar na mara nyingi sana watu wamefukuzwa pale Jangwani wanarudi tena.

Sasa leo hii kuilaumu serikali bila kuwalaumu na raia pia sio busara maana wote wanamakosa, wengi wanajienga Jangwani kukwepa nauli ya kwenda Posta au Kariakoo sasa kuishi kimjini mjini kuna madhara na kama hivyo wamepoteza mali zao.

Serikali inakuja kwenye miundo mbinu na sera zao za makazi wameshindwa kabisa.
 
mtoa mada anahoja ya msingi ila kiukweli toka moyo cdm wangeweza kufanya matakwa ya mtoa mada ila wasema ovyo wanaosema kuwa wanatafuta umaarufu katika matatizo utawaacha wapi?
 
Serikali ina wajibu wa kulinda raia na mali zake. Ndo maana inakusanya kodi mbalimbali toka kwa raia wake na kuzitumia katika kutekeleza mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa raia.
Sasa, kuna mijitu humu eti inawalaumu watu kujenga mabondeni. Ni kosa la mjengaji au serikali? Kama serikali inajua kabisa kwamba maeneo kama hayo ni hatarishi wanatakiwa kuzuia kwa nguvu yoyote ili kuepukana na hasara kama hizi zinazoweza kuepukika.
Vilevile ni lazima tuilaumu serikali kwa kutoweka tahadhali au mbadala wanapojenga miundombinu. Kwa mfano kwa sasa njia iko moja tuu ya kuelekea mikoa ya pwani, moro, dodoma mbeya, tabora nk. Kwa hiyo kama mfano tatizo lililotokea mbezi luis, kungekuwa na njia mbadala hakuna usumbufu wowote ambao ungetokea. Mie ninaamini kila kitu kinawezekana kufanyika katika serikali yetu ila tunashindwa kwa kukosa UZALENDO na kuwa na mipango mikakati isiyotekelezeka.
Kwa haya maafa yanayotokea serikali lazima tuilaumu. Tunailaumu kwa sababu tayari kulikuwa na utabiri ulioonyesha kuwepo kwa mvua kubwa. Wakati huo huo tuna kitengo cha maafa, je walichukua tahadhari gani. Matukio kama elnino, sunami etc ni natural calamity ambazo hazitokei mara kwa mara na hivyo serikali haiwezi kulaumiwa. Kwa maafa yanayotokea serikali ilaumiwe kabisa. Jambo la kushangaza ni kwamba, wanapotoa hizi huduma si kana kwamba wanatoa msaada bali ni haki yetu kwa maana tunalipa kodi! Ukiwasoma vizuri hawa watoa huduma inakuwa kama wanatoa msaada na si wajibu wao bali wanaweza kufanya au kutofanya bila ya kuhojiwa kwa nini wanafanya hivyo.
Shime wananchi tubadilike na tusidanganye kwamba serikali inatoa msaada, bali ni wajibu wao kufanya hivyo. Ni haki yetu kupewa hizi huduma!
Nakubaliana na wewe kabisa ila jambo ambalo napinga mimi ni kutomlaumu mkazi wa Jangwani kwa kujenga nyumba pale, miaka mingi tu serikali inapiga kelele watu wasijenge pale sasa kama raia hawezi kusikiliza pale anapoambiwa wajibu wake inakua ngumu .

Ndio maana nasema ukiwa unaishi kwenye nchi maskini unatakiwa kutumia sana akili yako kutatua kero zako mwenyewe la sivyo utakufa mapema, kujenga Jangwani ni uzembe wa kufikiri.
 
Vyama vyote vya siasa vimefeli katika hili.

Tunavionea vyama vya siasa na hasa vyama visivyo na madaraka. Enzi za Lyatonga alitaka kuweka lami kule kwao Marangu na alizuwiwa na kupelekea mapipa ya lami kuwa kule barabarani mpaka leo. Serikali ina jukumu la kusaidia watu wake kiushauri na kuwaokoa kutokana na majanga kama haya ukizingatia watu wale wanalipa kodi na hata mishahara ya watumishi inatoka kwa watu hawa. Cha mwisho ni kwamba, lawama ziende kwa serikali kwa kuwaacha watu hawa waendelee kuishi mabondeni ikizingatiwa siyo mara ya kwanza kupata mafuriko sehemu hizo. wakati wa ruksa ilitokea pia nakumbuka. kwa nini tusubiri watu waelee ndiyo tutake kuwaokoa? sisemi kwamba tunaweza kuzuia maafa kama haya kabisa, ila panapowezekana serikali itimize wajibu wake na tusibebeshe mzigo watu wasiohusika.
 
Hali ya usafiri Dar sasa imeendelea kuwa tete kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Kwasasa niko Mbezi kwa masaa mawili sasa nkianza safari ya kwenda Hija kama ilivyo ada kwa Desemba.

Magari zaidi ya 1000 madogo kwa makubwa yamekwama hapa mbezi luis. Maji mengi hapa bonde la mchicha kiasi barabara haipitiki. Kwa wanaofikiria kuitumia njia hii kwa sasa wafikirie mbadala. Bahati mbaya sijui kama tunayo mbadala na sidhani kama kuna wazo hilo miaka za usoni hasa ukizingatia watawala maliopo. Sijui wakati ujenzi unaendelea wa barabara zetu wataalamu wetu watanzania wazalendo wanakua wapi, au ndo kushiriki ktk keki ya ufisadi.

Kwa waajiri tafadhali muwaelewe wafanyakazi wenu watapotoa sababu hii. Sijui kama hali ikiendelea namna hii itakuaje na nani awajibike maana masaa ya kazi (man hours) yanayo potea kwa misongamano, adha na dhoruba mbali mbali ambazo naamini zingeweza zuwilika hatuwezi tegemea miujiza ili uchumi ukue.

===============
403638_286815341370489_100001260751190_920517_112236411_n.jpg

403071_343515252341423_100000488544093_1461108_1172190369_n.jpg

393435_2905938564380_1138010634_33260165_1540614176_n.jpg

381168_343548019004813_100000488544093_1461163_2104724732_n.jpg

375460_343705685645760_100000189955182_1567493_1041374402_n.jpg


12_11_vq2vh1.jpg

Kununju ebibanja byaigara, inye abazee mukairukila omumaanga ne ekyomulikukola okwo tikikumanyika! mwasigala kuekwa nka abana! mushube omukyaro!
 
Jamani mungu ni
mwema,mliomba
modarate rainfall na
yeye kaleta floods.
Watz mpewe nini
jamani?
 
Back
Top Bottom