MAFURIKO: Hali ya usafiri Dar yawa tete, makazi yasombwa!

Mhhhhh! hali inatisha sana....hii mvua ikiendelea kwa kasi kubwa kiasi hiki basi wengi wanaweza kupoteza maisha.
 
Jamani napigiwa na jamaa yangu mmoja mto kawe umepasuka maji yameanza kuingia hadi kwenye n yumba za mbezi beach tankibovu kule chini watu wameshindwa kutoka watoto wanapiga kelele tv na biashara zingine ziko ndani ya maji

kwa wenye kutoa m saada tafadhali wasiliana na huyu dada alie jiran yao 0713 40 11 00

kazi ipo kwa kweli
Nimepita mda si mrefu pale sijaamini macho jinsi maji yanavyoanza kukatiza mitaani.
 
Nyerere road.jpg
Jamani hii ni hali niliyoikuta maenao ya Karakana ya Tazara Nyerere Road. Huko mitaani hali ni mbaya zaidi.
 
Mungu atunusuru. Mimi pia nimezingirwa na maji huku Mabibo nashindwa kutoka nje! ikiendelea tu ama na huku mto ukicheua basi imekula kwangu!!!
 
barabara bara ipo tatizo waloijenga si kikwete nyie wakandarasi.
usilaumu serikali kwa kitu kinachoitwa act of god,force majuare,ilaumu kwa hatua ambazo haitachukua baada ya force majuare ,bush alilaumiwa kwa kutochukua hatua baada ya katrina
 
hali ikizidi kuendelea hiv itazidi kua mbaya mana karibia kila sehemu jijina hasa mabondeni na sehemu tunapokaa wananchi wa kipao cha chini....shime ndugu zangu tusaidiane kusaidia wenzetu.
 
duh imeanzia philipines sasa inahamia tz nini? ee Mungu tunusuru kwani hatuna uongozi wa nchi wa kuweza kutoa msaada, hela yote imetumika sherehe za miaka hamsini ya uh........

Huwa mnaandika utumbo saa zingine. "Disaster" zinapotokea si fedha zinazosaidia ni utu. Akili za watu wengine zipo kwenye "hela" tu, hebu nioneshe mmoja anaeondoka nazo hapa duniani? maji hufata mkondo na fedha hufata wenye asili nazo, kama huna asili ya fedha hata ufanye nini utazisikia tu.

Wakati wa maafa hatutizami "hela" tunatizama tusaidiane vipi.
 
Kwa hiyo ya Kawe ni ujinga na ufisadi wa watendaji wa Manispaa ya Kinondoni...wao wanauza kila sehemu wameuza huo mto kwa mafisadi flani wamejaza kifusi wamejenga nyumba sasa faida ya ufisadi ndio hiyo...hii nchi ina watu wajinga sana..sijui wakoje yani wako kama mambwa yanaimaliza nchi
 
Poleni sana wa-TZ wenzetu mliokumbwa na janga hili!! Dua zeetu wote ziko na nanyi. Serikali ya mkoa wa DSM inabidi ijipange kuwatunza watu hawa katika makambi.

Pili ifike mahali tuanze kujifunza katika majanga haya. Suala la watu waliovamia mabonde lifanyiwe kazi once and for all. Ni kweli tumekisha fanya makosa kwa kutoa hati kwa watu aliovamia mabonde, tujurekebishe tusonge mbele. Kujirekebisha inahusisha maamuzi magumu ya kuhamisha watu hawa ili kesho tusirudie huku!!!

Otherwise poleni wahanga!!
 
Hii mvua ya leo ni kubwa kuliko ya jana, kwani jeshi la uwokoaji liko wapi jamani! Kama jana ilikuwa vile leo itakuwaje, tusidanganyane polisi watapita na helkopta kutushangaa kama walivyofanya jana! Jeshi la uwokoaji hii ndo kazi yao
 
Hii mvua ya leo ni kubwa kuliko ya jana, kwani jeshi la uwokoaji liko wapi jamani! Kama jana ilikuwa vile leo itakuwaje, tusidanganyane polisi watapita na helkopta kutushangaa kama walivyofanya jana! Jeshi la uwokoaji hii ndo kazi yao

Yawezekana halina posho.
 
Back
Top Bottom