MAFURIKO: Hali ya usafiri Dar yawa tete, makazi yasombwa!

Yetu Macho

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
224
31
Hali ya usafiri Dar sasa imeendelea kuwa tete kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Kwasasa niko Mbezi kwa masaa mawili sasa nkianza safari ya kwenda Hija kama ilivyo ada kwa Desemba.

Magari zaidi ya 1000 madogo kwa makubwa yamekwama hapa mbezi luis. Maji mengi hapa bonde la mchicha kiasi barabara haipitiki. Kwa wanaofikiria kuitumia njia hii kwa sasa wafikirie mbadala. Bahati mbaya sijui kama tunayo mbadala na sidhani kama kuna wazo hilo miaka za usoni hasa ukizingatia watawala maliopo. Sijui wakati ujenzi unaendelea wa barabara zetu wataalamu wetu watanzania wazalendo wanakua wapi, au ndo kushiriki ktk keki ya ufisadi.

Kwa waajiri tafadhali muwaelewe wafanyakazi wenu watapotoa sababu hii. Sijui kama hali ikiendelea namna hii itakuaje na nani awajibike maana masaa ya kazi (man hours) yanayo potea kwa misongamano, adha na dhoruba mbali mbali ambazo naamini zingeweza zuwilika hatuwezi tegemea miujiza ili uchumi ukue.

===============
403638_286815341370489_100001260751190_920517_112236411_n.jpg

403071_343515252341423_100000488544093_1461108_1172190369_n.jpg

393435_2905938564380_1138010634_33260165_1540614176_n.jpg

381168_343548019004813_100000488544093_1461163_2104724732_n.jpg

375460_343705685645760_100000189955182_1567493_1041374402_n.jpg

12_11_vq2vh1.jpg
 
Polen wakaz wa dar. Kitaeleweka tu one day. Hawa jamaa hawajui adha ya usafiri maana wanatembelea benz na V8 wakiongozwa na ving'ora.
 
hapa hakuna ujanja kabisa..........anyeweza kupita bagamoyo kwa wanaokwenda tanga, moshi, arusha wafanye hivyo. Hata wanaokwenda moro, iringa mbeya, songea, dodoma.

Inavyoonekana barabara haitapitika kabla ya masaa matatu kuanzia sasa. Na hilo litawezekana tu kama mvua utaacha kunyesha.
 
Una maana maji ya mvua yamefunga barabara?. Kama ni hivyo kwanini unailaumu serikali?.

Al nino,Sunami na mafuriko mengine katika nchi mbalimbali ni makosa ya serikali husika?.
 
Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele
Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya
Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana
---Source: Msanii (Rais bora kuliko wote Tanganyika) Kikwete

Imefika wakati sasa inabidi tufafanuliwe juu ya hizi kauli mbiu zetu za kila siku!!
Tumethubutu na tuneweza kufanyaje?
Na kama tunasonga mbele, kuelekea wapi??
Isije ikawa tunasonga mbele kuelekea tulipotoka!!
 
....Hata huko tulipotoka waliojaliwa kuona miaka hiyo wanasema kulikuwa na ahueni kubwa sana, naona tunaelekea kuzimu.
 
hapa hakuna ujanja kabisa..........anyeweza kupita bagamoyo kwa wanaokwenda tanga, moshi, arusha wafanye hivyo. Hata wanaokwenda moro, iringa mbeya, songea, dodoma.

Inavyoonekana barabara haitapitika kabla ya masaa matatu kuanzia sasa. Na hilo litawezekana tu kama mvua utaacha kunyesha.

hapa kimenuka! badala ya kwenda kazini narudi kitandani kulala! mvua zimetuvua viraka vilivyokua vinatusitiri.
 
Mimi pia sijatoka mpaka sasa, maji ni mengi mno hapa nje, yamejaa kwenye ngazi ya kuingilia k wangu, ikiendelea kunyesha na mimi nitakuwa mhanga wa mafuriko. Naona mzungu anaelewa maana hajapiga simu mpaka sasa kuuliza kwanini nimechelewa!:lol:
 
Hali ya usafiri Dar sasa imeendelea kuwa tete kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Kwasasa niko Mbezi kwa masaa mawili sasa nkianza safari ya kwenda Hija kama ilivyo ada kwa Desemba.

Magari zaidi ya 1000 madogo kwa makubwa yamekwama hapa mbezi luis. Maji mengi hapa bonde la mchicha kiasi barabara haipitiki. Kwa wanaofikiria kuitumia njia hii kwa sasa wafikirie mbadala. Bahati mbaya sijui kama tunayo mbadala na sidhani kama kuna wazo hilo miaka za usoni hasa ukizingatia watawala maliopo. Sijui wakati ujenzi unaendelea wa barabara zetu wataalamu wetu watanzania wazalendo wanakua wapi, au ndo kushiriki ktk keki ya ufisadi.

Kwa waajiri tafadhali muwaelewe wafanyakazi wenu watapotoa sababu hii.
Sijui kama hali ikiendelea namna hii itakuaje na nani awajibike maana masaa ya kazi (man hours)yanayo potea kwa misongamano, adha na dhoruba mbali mbali ambazo naamini zingeweza zuwilika hatuwezi tegemea miujiza ili uchumi ukue.
poleni sana wakazi wa dar.
 
Taarifa za jeshi la polisi asubuhi hii zinasema kuwa barabara hiyo (Mbezi Luis) imekatika na hivyo uwezekano mkubwa sasa kwa wale wanaokwenda kuhesabiwa wakatumia barabara ya kwa ****** (Bagamoyo)

Nyie mnaopaswa kwenda makazini imekula kwenu kama helikopta ya haitafanikiwa kuja kuwachukua.
 
Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele
Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya
Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana
---Source: Msanii (Rais bora kuliko wote Tanganyika) Kikwete

Ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Tumethubutu tumeweza na tunasonga mbele.
 
Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele
Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya
Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana
---Source: Msanii (Rais bora kuliko wote Tanganyika) Kikwete

Tumethubutu, Tumeshindwa na tunazidi kuboronga.
Maisha ya fedhea kwa kila mtanzania yataendelea kuwepo.
Mpaka mshike adabu kudadadeki
 
Jamani napigiwa na jamaa yangu mmoja mto kawe umepasuka maji yameanza kuingia hadi kwenye n yumba za mbezi beach tankibovu kule chini watu wameshindwa kutoka watoto wanapiga kelele tv na biashara zingine ziko ndani ya maji

kwa wenye kutoa m saada tafadhali wasiliana na huyu dada alie jiran yao 0713 40 11 00

kazi ipo kwa kweli
 
Tatizo mkikaa na kula mnaona wengine ni wapuuzi...hebu nenda na ving'ora vyenu mbezi mwisho kama utapita!

Mkuu, mafuriko na hizi mvua ni dunia nzima...au JK anausika?
 
Back
Top Bottom