Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Mbunge wa Ilala bwana Zungu alikuwa na makazi yake pale Jangwani sijui kama na yeye ni mhanga ama la! Mwenye taarifa atuhabarishe. Nakumbuk jinsi alivyowatetea hao wa bondeni jangwani wakati mama Tiba aliposema wanatakiwa wahame. Zungu akasema serikali inataka iwahamishe ili wawe wanatoka masaki kwenda kula ice cream pale jangwani. Akasema wananchi wa jangwani waachwe waishi pale na watakuwa wakila ubuyu badala ya kufukuzwa na wa masaki kuja kulia ice cream pale jangwani. Sijui Zungu anasemaje sasa? Pale kuna wapiga kura wengi na Zungu alikuwa anaziwinda lakini madhara yake ndiyo hayo.Naweza kukuelewa labda kwa kuwa hawa jamaa wa mabondeni hawana mtetezi. Kama ni suala la utaratibu, vipi wale wa EPA? walichota na wakaambiwa warudishe? je utaratibu ulifatwa? Wabunge wameongezewa posho juzi tu na wote tunajua kuwa utjjaratibu haukufatwa lakini kuna hatua yoyote iliyochukuliwa? Hawa wananchi tokea wanaanza kuenga miaka zaidi ya 20 serikali inawaangalia na naamini hata wakati wa uchaguzi kuna vituo vya kupigia kura huwa vinafunguliwa na tume maeneo hayo. hata chama cha magamba kina watendaji wa kata maeneno hayo. Nadhani bado kuna ,maswali mengi hapo hatuwezi kusema wananchi ndo wana makosa peke yao