Opaque
JF-Expert Member
- Oct 24, 2008
- 1,359
- 719
Nadhani hamkuelewa kwa nini niliandika Dar hakuna mvua. Mleta thread (Gaza) amesema "anasikia Dar kuna mvua, mwenye taarifa atoe". Ukiangalia muda aliobandika, ni saa kumi kasoro dakika kumi na sita jioni (15.44 pm). Mvua ya Dar imeanza saa kumi na moja alfajiri (5.00 am hivi). Angalieni interval ya time kutoka mvua ilipoanza hadi jamaa anapokuja kuulizia mafuriko (saa kumi na moja asubuhi hadi saa tisa jioni). Kwa mwana JF aliyejiunga Novemba 2010 ana uzoefu wa mwaka mmoja humu. Alichotakiwa kukifanya kabla ya kuanzisha thread ni kupitia title za walau page mbili hivi za 'New Posts' ambazo kila page ina post 50, so page mbili ni post 100. Ninasema apitie titles, si lazima azifungue. Kwa kupitia title za page mbili, utapata overview ya kinachoendelea nchini na duniani, so kama utataka kuuliza kitu ambacho ni breaking news, huenda ukakuta tayari watu walishabandika na hivyo hauna haja ya kuanzisha thread just kwa ajili ya kuuliza, kwa kuwa utapata majibu.
Tukirudi kwenye topic, mkuu Gaza wakati anauliza kwenye thread yake mpya hiyo saa tisa jioni, tayari kulikuwa kuna zaidi ya thread tatu zinazozungumzia mafuriko ya Dar. Kama angepitia titles kwanza, angekuwa na haja gani ya kuuliza kama ni kweli Dar kuna mafuriko? Nilitaka nitoe fundisho kwa wanaokimbilia kuanzisha threads bila kwanza kupitia zinazoendelea; hiyo ndo nia yangu.
Najua kuna watu wameudhika kwa maandishi yangu, nawaombeni msamaha. Lakini nami niliudhika kwa kuona mathread yenye maudhui yanayofanana yakiwa yanaanzishwa tu bila watu kuchungulia waliotangulia wameweka nini. Nina akili timamu, aliyeelewa atagundua hilo akisoma vizuri haya, na atakayeendelea kuunga mkono tabia ya uanzishwaji hovyo wa mathread, aendelee tu.