Mafuriko Dar. Maneno na nasaha za MBOWE Ni funika bovu

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Kila siku huwa nasema hapa kuwa mimi si shabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mfuasi wa hoja za nguvu na maneno ya maana. Nimemuona Mh MBOWE Kupitia mlimani TV akitoa maneno na nasaha zake kuhusu janga la mafuriko Dar. Kamanda uko juu, uko juu zaidi ya nyota mbinguni, unawaka kuliko jua, wewe ni bingwa zaidi kuliko YANGA.

Unatisha zaidi ya njaa. Mkali kuliko simba kichaa, mcharuko zaidi ya nyati aliyejeruhiwa..una sumu kali zaidi ya koboko. Pamoja na mengi uliyosema, nimeukubali ushauri wako wa kutumia mbwa maalumu wa polisi kusaka maiti ambazo bila shaka zimefukiwa na vifusi VIVA KAMANDA MBOWE
 
Kha!! Job true true, hiyo misifa unaweza kujob hundred!!
 
Kila siku huwa nasema hapa kuwa mimi si shabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mfuasi wa hoja za nguvu na maneno ya maana. Nimemuona Mh MBOWE Kupitia mlimani TV akitoa maneno na nasaha zake kuhusu janga la mafuriko Dar. Kamanda uko juu, uko juu zaidi ya nyota mbinguni, unawaka kuliko jua, wewe ni bingwa zaidi kuliko YANGA. Unatisha zaidi ya njaa. Mkali kuliko simba kichaa, mcharuko zaidi ya nyati aliyejeruhiwa..una sumu kali zaidi ya koboko. Pamoja na mengi uliyosema, nimeukubali ushauri wako wa kutumia mbwa maalumu wa polisi kusaka maiti ambazo bila shaka zimefukiwa na vifusi VIVA KAMANDA MBOWE

Mh! Hapo kwenye red; huo nao ni mjadala mwingine mpana hasa kuhusiana na imani za watu. Sidhani kama Mh. Mbowe ataeleweka vyema na kila muumini na nachelea huenda wajinga wachache wakaligeuza siasa-dini.
 
Viongozi wetu wa CCM inshu ya mafuriko washageuza dili....!

Mi nalia na mkuu wa mkoa kwa kula michango ya g.mboto sasa anakula za mafuriko kwa nn watoa misaada wasipeleke kwa walengwa moja kwa moja kuliko kupitia mikono ya kina sadik na wengineo? Nasikia uchungu
 
Je, amegusia pia haya? (Sorry, niliya-post kwenye thread nyingine):

Pongezi zao wote waliojitolea kwa hali, mali, na dua kwa ajili ya wenzetu walioathirika na mafuriko. Kwa tasisi za kisiasa, CHADEMA waliotoa T.Shs. 25,000,000/= (milioni ishirini na tano) na CCM T.Shs. 4,000,000/= (milioni nne) wameonesha mfano kwamba kumbe linapotokea tatizo la kitaifa SOTE NI WAMOJA bila kujali itikadi zetu.

Hata hivyo, kutokana na hali tete ya UFISADI uliotamalaki serikalini na kutokana na AGIZO la Mh. Rais na viongozi wengine mbalimbali wa serkali kuwataka wananchi husika wahame, nilitegemea CHADEMA waende mbali kidogo na kama hawakufanya hivyo nawashauri:-

(i) Kuitaka serikali, na kimsingi huu ni wajibu wake, kuhakikisha wananchi wote waliopoteza makazi yao wanapatiwa makazi mapya na serikali katika maeneo salama. Haitoshi tu kusema hameni au kuwapatia viwanja "maporini" bila kuwezeshwa na ukizangatia hali halisi ya wananchi kiuchumi. Tafadhali toeni tamko linaloeleweka.

(ii) Endapo wananchi kweli watahama maeneo yao "natabiri" mafisadi na "wawekezaji" watapatiwa maeneo husika mara moja tena kwa kasi ya ajabu. CHADEMA na taasisi nyingine mnao wajibu wa kulitaka Bunge (bahati mbaya hatuna Bunge makini zaidi ya umakini kwenye posho) kutunga sheria kali ya KUHIFADHI MAENEO HUSIKA DHIDI YA UVAMIZI WA MAFISADI.

(iii) Endapo Bunge litashindwa kutunga sheria na serikali kuuza maeneo husika mnao wajibu wa kuuambia umma mapema nini cha kufanya leo na kama ikishindikana leo basi hapo baadaye endapo mtapata ridhaa ya kushika dola. Hili ni muhimu na kusiwe na mzaha. Inapaswa kueleweka tangu sasa kwamba SHERIA ZOTE ZA KIPUUZI zitakazomilikisha maeneo haya kwa mafisadi ZITATENGULIWA ili kila fisadi aelewe hivyo kungali mapema.

Nawasilisha kwa CHADEMA na taasisi nyingine makini za kiraia.
 
Kila siku huwa nasema hapa kuwa mimi si shabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mfuasi wa hoja za nguvu na maneno ya maana. Nimemuona Mh MBOWE Kupitia mlimani TV akitoa maneno na nasaha zake kuhusu janga la mafuriko Dar. Kamanda uko juu, uko juu zaidi ya nyota mbinguni, unawaka kuliko jua, wewe ni bingwa zaidi kuliko YANGA. Unatisha zaidi ya njaa. Mkali kuliko simba kichaa, mcharuko zaidi ya nyati aliyejeruhiwa..una sumu kali zaidi ya koboko. Pamoja na mengi uliyosema, nimeukubali ushauri wako wa kutumia mbwa maalumu wa polisi kusaka maiti ambazo bila shaka zimefukiwa na vifusi VIVA KAMANDA MBOWE
Daah!Mkuu,huku kusifia kwingine ni too much!
 
Yaani kutoa dazeni mbili za maji ya kunywa na biskuti ndio funika bovu?

Mbona watu wengi tu wamejitolea vitu vya thamani ujasema funika bovu!

Chadema walichofanya ni kawaida tu kama walivyofanya wanamuziki wa bongo fleva!
 
Dah aisee, mbona umekurupuka? Sijaongea kuhusu misaada ndugu. Nimesema kuhusu nasaha alizotoa, nasaha, nasaha, nasaha, au maoni kama huelewi maana ya neno nasaha, maoni, maoniiiii.
 
Dah aisee, mbona umekurupuka? Sijaongea kuhusu misaada ndugu. Nimesema kuhusu nasaha alizotoa, nasaha, nasaha, nasaha, au maoni kama huelewi maana ya neno nasaha, maoni, maoniiiii.

Nasaha ndio nini?
 
Kila siku huwa nasema hapa kuwa mimi si shabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mfuasi wa hoja za nguvu na maneno ya maana. Nimemuona Mh MBOWE Kupitia mlimani TV akitoa maneno na nasaha zake kuhusu janga la mafuriko Dar. Kamanda uko juu, uko juu zaidi ya nyota mbinguni, unawaka kuliko jua, wewe ni bingwa zaidi kuliko YANGA. Unatisha zaidi ya njaa. Mkali kuliko simba kichaa, mcharuko zaidi ya nyati aliyejeruhiwa..una sumu kali zaidi ya koboko. VIVA KAMANDA MBOWE
Dah...!!! hii misifa nimecheeeka hadi kojo limetoka.
 
Dah aisee, mbona umekurupuka? Sijaongea kuhusu misaada ndugu. Nimesema kuhusu nasaha alizotoa, nasaha, nasaha, nasaha, au maoni kama huelewi maana ya neno nasaha, maoni, maoniiiii.

Tupe basi alichosema kamanda Mbowe!
 
Back
Top Bottom