Mafuriko Dar es Salaam: Nani alaumiwe kati ya Meya Mwita (CHADEMA) au RC Makonda(CCM)?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,758
141,622
Kwa kweli leo nimepita mitaa ya Tandale kwa Mtogole na mwananyamala msisiri hali ya mafuriko imenisikitisha sana.

Hivi kwa kadhia hii inayosababishwa na miundombinu ya hovyo nani tumtupie lawama au tumpelekee malalamiko kati ya Mkuu wa mkoa mh Makonda au yule mstahiki meya Mwita?

Wakuu hali ni mbaya na ukizingatia ukweli kuwa jiji la Dsm limekumbwa na ugonjwa wa dengue basi mashaka kwa binadamu yanazidi kuongezeka.

Kwa hasira naomba niishie hapo

Maendeleo hayana vyama!
 
Sijapata connection ya uliowataja kwenye title na maelezo yako aisee!
 
Natural Disaster huwa hakuna wa kulaumiwa... Ukizingatia Makusanyo yote ya Jiji yanapokelewa na Hazina kuu na mtoaji ni jumba jeupe... Ndege kwanza
 
Ukienda tandale ndio utaelewa!
Yaaap, miundo mbinu inaweza kuwa miongoni mwa chanzo cha mafuriko ingawa sehemu kubwa ya dar ni mabondeni, mabwawa au mashamba ya mpunga. Hivyo mafuriko kwa miundo mbinu yetu mibovu na makazi holela hayaepukiki na sio tuwalaumu hao viongozi ambao hiyo hali wameikuta
 
Mazuri huwa niya Makonda mabaya huwa ni ya Chadema.

Ule mradi wa maji uliletwa na Magufuli haya mafuriko tufanya yamesababishwa na Mwita.
 
Natural Disaster huwa hakuna wa kulaumiwa... Ukizingatia Makusanyo yote ya Jiji yanapokelewa na Hazina kuu na mtoaji ni jumba jeupe... Ndege kwanza
Tena hizi za Dar ni kidogo tu, natural disaster zimejaa America na Asia huko ndo ukisikia mafuriko ujue mji mzima uko majini
 
Wakulaumiwa ni JK kuruhusu ujenzi wa kituo cha mabasi ya mwendo kasi eneo la jangwani
 
Kwa kweli leo nimepita mitaa ya Tandale kwa Mtogole na mwananyamala msisiri hali ya mafuriko imenisikitisha sana.

Hivi kwa kadhia hii inayosababishwa na miundombinu ya hovyo nani tumtupie lawama au tumpelekee malalamiko kati ya Mkuu wa mkoa mh Makonda au yule mstahiki meya Mwita?

Wakuu hali ni mbaya na ukizingatia ukweli kuwa jiji la Dsm limekumbwa na ugonjwa wa dengue basi mashaka kwa binadamu yanazidi kuongezeka.

Kwa hasira naomba niishie hapo

Maendeleo hayana vyama!
Jiwe
 
Viongozi wakipamga mikakati inakuwa SMART
Specific goals
Measurable
Assignable
Relevant
Time measurable
 
dhambi zetu ndio za kulaumiwa, yanapokea hayo tunakumbushwa dhambi zetu zimezidi kuuchafua uso wa dunia hivyo Mungu anatoa hiyo kama adhabu
 
Aliyetengeneza kituo cha mwendo kasi jangwani ndio wa kulaumiwa na aliyejenga station ya bus ya mwendokasi katikati ya mto msimbazi ndio wa kulaumiwa.. Huwezi jenga kituo kikubwa cha ma bus ya mwendokasi ktk mto na ukajenga kituo cha abiria ambao hawapandi katikati ya mto msimbazi, inashangaza sana.. Pale jangwani ingetakiwa culverts kubwa kubwa kama 16 hv au zaidi na kubomoa kile kituo cha ma bus na kituo cha abiria pale
 
Ukienda tandale ndio utaelewa!
Sema ukweli tuu mafuriko ya jangwani kwa mfano ni uzembe usio na kifani wa watendaji wa serikali. Pale jangwani watu walihamishwa lakini la ajabu serikali ikajenga kituo cha mwendokasi!! Huu si ujinga na ufisadi? Pili bonde la kutoka Magomeni mpaka fire linajulikana kujaa maji but very strange badala ya barabara hiyo kuinuliwa juu iwe kama daraja kwenye hicho kipande wao wakajenga kawaida tuu, sasa unategemea nini?
 
Back
Top Bottom